Apigishwa mbizi kwenye dimbwi la maji ya barabarani kwa kukutwa katinga sare za jeshi

hata mimh nashangaa sana,,
Watanzania sijui tuna nini. Hili ilibidi limake headlines. Mzalendo kavaa jezi za jeshi kuonye uzalendo. WATANZANIA wako pembembeni wanashuhudia anavyodhalilishwa.
Akija OBAMA mama NTILIE wanatimuliwa wote.

SIJUI.
Nchi za wenzetu kama Marekani bendera na jezi za jeshi lao, huvaliwa kizalendo na fahari. Kwetu ni mwiko ni sawa na watengeneza silaha vichochoroni hukamatwa kama waharifu na si wanasayansi. Tumelaaniwa
 
Haki za binadamu,kitendo hiki kwa watu wastaarabu wangem-subject kwenye sheria. Wanajeshi wetu wengi na darasa la saba na form four. Sifa za kijinga sana hizi.
 
Nchi za wenzetu kama Marekani bendera na jezi za jeshi lao, huvaliwa kizalendo na fahari. Kwetu ni mwiko ni sawa na watengeneza silaha vichochoroni hukamatwa kama waharifu na si wanasayansi. Tumelaaniwa

Hii yote inatokana akili fupi za viongozi wetu (MARAISI) wa AFRICA. Always wako subjecteted to INFERIORITY , wakipanda ndege kwenda ulaya wakifika huko ni kucheka cheka tu.

Ilhali huku sisi tunapotizama MOVIE za WEST, mwisho tunaona STARRING akipandisha bendera za wakoloni na tunafurahiaaa..
Wazungu wameyaandaa majesh yetu kututesa sisi wenyewe, ILHALI MAJESHI YAO YANA USIFU UBEBERU WAO.

SAD.
 
Na angekula kweli *****.... tunapata mateso ya hali juu kuwa souljers.... tukikupa bunduki raia usia na mafunzo utaua kila mtu... lakin sisi tunawagalagaza tu

Mateso gani wakati mnakula bure tu huko makambini
 
Utavaaje nguo zinazofanana na sare za jeshi,inamaana kakosa nguo kabisa huko kwenye mitumba?
 
Huyu mwanajeshi anatakiwa kufukuzwa kazi na kushitakiwa kwa kudhalilisha raia.
 
Nchi za wenzetu kama Marekani bendera na jezi za jeshi lao, huvaliwa kizalendo na fahari. Kwetu ni mwiko ni sawa na watengeneza silaha vichochoroni hukamatwa kama waharifu na si wanasayansi. Tumelaaniwa

Tatizo Waarika wakiruhusiwa watatumia kufanyia uhalifu.
 
Tatizo Waarika wakiruhusiwa watatumia kufanyia uhalifu.

Waharifu wa ufisadi wa BOT na mengineyo wao wanavaa jezi gani? Kwani waharifu wa leo wanavaa mavazi gani? Ni kutaka utukufu tu, ili waonekane wao tu with no apparent reason
 
Ni lini Tz sheria zinafuatwa!!? Ila kwa huyu mwanajeshi ndo imekuwa nongwa, tatizo lenu mpo biased kweli, ingetokea kama mdau mmoja alivyoleta picha ya Nchemba ndo kapigizwa mbizi wengi wenu mngefanya sherehe ili tu kwa sababu imetokea kwa huyu mnapiga makelele, hivi unafikiri wakati huyu jamaa anafanyiwa yote haya si watu walikuwepo!!? Hawa watu walikuwepo kwa nini hawakutoa ripoti polisi ili huyo mtoa adhabu mwanajeshi achukuliwe sheria unayoiongelea!! Nyie ndo mnafuga maovu eti kisa sheria, huyu mwenzio katia adabu harudii tena

Basi msiwe mlalama kuwa watawala hawafuati sheria.

Tena mkae kimya kabisa maana nchi hii hakuna kufuata sheria.

Sawa?
 
Ha Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha haaaaaaah, sasa ndo unagundua kuwa ni kuvunja sheria

Nisome vizuri kichwa kibovu wewe.

Kuna tofauti kati ya mtu kuvunjwa sheria na kuadhibiwa.

Hapa hatuzungumzi mtu kuvunja sheria bali nani anayetakiwa kumwadhibu.

Je, ni mwanajeshi? If, so kwa sheria gani?

Lakini umeshasema Tanzania hakuna kufuata sheria anyway.

Kwa hiyo sikushangai sana kunishauri nivunje sheria.
 
Mkuu dawa ya moto ni moto,ukijifanya unajua kuvunja sheria ujue kuna wanaume wanajua kuvunja sheria zaidi yAko.

So, what are trying to suggest?

Kweli Tanzania ina vichwa vya panzi.
 
No wonder siku wakikuambia inama utawainamia tuu wewe.

Kuna tofauti ya kumwogopa na kumheshimu mtu.

Kati ya watu ambao sikuwahi tegemea kama wangekuwa na akili kama iliyoandika hayo maneno basi ni wewe. Ila ndo binadamu tulivyo, unafikiria upuuzi tu
 
Jeshi lishakataza raia kuvaa nguo za jeshi au zenye alama ya jeshi anayejifanya kichwa maji sharti afunzwe kazi.

Siyo jeshi limekataza bali sheria za nchi ndo zimekataza watu kuvaa mavazi yanayofanana na sare za jeshi.

Elimu ya uraia imewapitia mbali sana kiasi cha kudhani sheria zinatungwa na jeshi shenzi type wewe.

Afterall hii nchi haiko chini ya utawala wa jeshi na ndo maana kila mara mnaomba eti jeshi lichukuwe nchi kwa sababu mliowapa nchi wanavunja sheria kama alivyofanya huyo mjeda na huyo anayepiga mbizi.
 
Haya, wale wanaotetea haki za binadam, tuwaone mkitetea haki ya huyu kijana kwa kuvunjiwa heshima na kuadhibiwa bila hukumu ya kisheria.

Siyo mnashobokea siasa tu.

Angekuwa polisi wa kawaida amefanya hayo mbona wangekuwa wameshajitokeza.

Hata kama tungekuwa kwenye vita sheria za kivita zinakataza wanajeshi kuwa-treat prisoners of war kama alivyofanya huyo mwanajeshi.
 
Kama kila kosa litaenda mahakamani unafikiri magereza yatatosha,

Kwa hiyo, huyo mjeda alifanya aliyofanya kuokoa magereza isijae?

Kwa nini mnaemtetea huyo mwanajeshi reasoning zenu ziko poor hivyo?

Acheni kuliabisha jeshi kwa kulitetea kwa reasoning za kijinga kama hii.

na isitoshe wengine ni vijana wadogo ujana tu unawasumbua,wakionywa wanarekebishika,sasa we unataka huyo jamaa akanyee debe,na huko jela ikiamuriwa na mahakama kuwa afungwe unafikiri kuna raha.Acha mambo mengine yaishie hukuhuku mtaani.

Oh dear. Kweli Watanzania IQ hakuna kabisa.
 
Nakumbuka niliwahi gongana na mwanajeshi eneo la Mailimbili Dodoma,karibu na kambi ya Makutupora jirani na chuo cha Mipango.
Alinikamata shingo akaniinamisha kwenye boneti,kama dakika mbili hivi huku akinigonga gonga kunitisha,alinikunja kama samaki. Hasira zilinipanda nikapoteza uoga,niliuchomoa mkono ule na kumsukuma,lakin hakurudi nyuma hata hatua moja,alikuwa kapangika misuli kwelikweli yule jamaa. Akavua helment ya pikipiki na akaanza nitupia ngumi mfululizo,nyingi zilinipata nyingi nilizipangua na kuna baadhi nilizirudisha. Nilikumbuka kuwa kwenye gari kuna Jeck na Rod/chuma cha kunyenyulia Jeki kwa gari dogo,nilikimbilia gari maana tulikuwa tumesogea mbali kulingana na ugomvi. Alipoona naenda kwenye gari alinikimbilia,bahati nzuri kile chuma kilikuwa nyuma ya kiti cha driver hivyo nilikiwahi na kufungua mlango na kukitoa,wakati huo jamaa amenikaribia basi nilimpiga na ile Rod shingoni na kichwani,alivuja damu pale pale na tukabaki tunazungukana kwa muda. Baada ya muda alianza kupiga simu kwa wenzake watu walikuwa wamejaa eneo lile. Alitokea mzee ambae ni mwanajeshi alivaa kiraia ndie alieamuru twende polisi,yule mwanajeshi alikataa kupanda gari langu,akasema ataenda kwa pikipiki,niliondoa gari tukiwa na yule mzee,njiani yule mzee akanambia kijana nishushe nenda nyumbani. Namkumbuka sana yule mzee aliniambia anaitwa Mayala,nilimpa namba ya simu ila hakunitafuta.
 
Back
Top Bottom