Ansbert Ngurumo: Wabunge wadhalilishWe, DC alindwe??

SERIKALI YA CCM INATAKA TUAMINI HIVI;
binadamu ni ccm asiye ccm ni mnyama.
wanaodhalilishwa ni ccm wasiyo ccm hawadhaliliki,
wanaposwa kulindwa na polisi ni ccm wasiyiyo ccm hawana haki hiyo,
wasiyo vunja sheria ni ccm wengine wanavunja,
walio juu ya sheria ni ccm wengine wapo chini ya sheria,
wanaopaswa kushinda chaguzi zote ni ccm wengine hawatakiwi kushinda,
ccm itatawala milele.
MIMI NASEMA "HAPANA" NA MWISHO WA CCM UMEFIKA TAYARI.mia
 
Another objective masterpiece from Ansbert Ngurumo.....READ ON!

===============================================================================
Wabunge wadhalilishwe, DC alindwe?

By Ansbert Ngurumo

TUSEME ukweli. Yaliyompata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, akiwa kwenye “uhalifu wa kisiasa” juzi si mazuri hata kidogo.

Lakini ni vema ukweli wetu uvuke hapo. Tumtazame kama kiongozi wa serikali katika eneo lake, na tumuulize: alijiingizaje katika siasa za vyama vya watu?

Alitarajia akisaidia hujuma za Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya wapinzani, wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wangemshangilia na kumpaka mafuta?

Mikakati ya ushindi wa CCM ilikuwa inamhusu nini? Hakujua kuwa kwa kitendo cha kujifungia ndani na makada wa CCM, alikuwa anahujumu haki na kuhatarisha amani yake na wengine?

Na kama alitaka kuwahujumu CHADEMA, ilikuwa lazima awafuate katika eneo walikokuwa wamepangiwa mkutano wa hadhara? Haiwezekani ameponzwa na ubabe na jeuri ya cheo na ukada usio mahali pake?

Kama alikuwa katika mkutano halali wa kikazi, kama watetezi wake wanavyodai, yeye kama mwakilishi wa rais katika eneo husika, kwanini hakuwa na ulinzi wowote hadi vijana wa CHADEMA walipomwokota na kumpa kibano?

Kama alivyohoji mtu mmoja jana, kama DC huyo asingewafuata CHADEMA huko walikokuwa, wangemtoa wapi “kumdhalilisha”? Na kama wao wangekuwa wanatendewa haki huko nyuma, na hata katika uchaguzi wenyewe wa Igunga sasa hivi, wangepata wapi hisia na sababu za kuhoji kazi aliyokuwa anafanya kwenye mkutano wa ndani, na hata kumtia mbaroni?

Bila kujadili uhalali au uharamu wa hatua waliyomchukulia vijana hao, nilipoona picha magazetini, DC akiwa ameshikiliwa kama mwizi, huku akiangua kilio hadharani, na baadhi ya wananchi wakishangilia, kumbukumbu zangu zilinipeleka katika tukio la aina hiyo Januari 5, mwaka huu mkoani Arusha.

Na baada ya kusikia viongozi makada, wanachama na mashabiki wa CCM wakilalamika kwamba Fatuma amedhalilishwa; na hasa baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kujiapiza jana kwamba “sasa liwalo na liwe, na kitakachotokea wasilaumiwe,” nikalazimika kukubaliana na usemi wa wahenga kwamba mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.

Katika tukio la Arusha, polisi – mbali ya kujeruhi kwa risasi na kuua raia watatu – waliwatendea vibaya baadhi ya washiriki wa maandamano, wakiwamo wabunge na wake za watu.

Kwa mfano, polisi wa kiume walimpiga ngwara Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya, akadondoka na kudunda kichwa chini kwenye barabara ya lami. Hakuna mwana CCM hata mmoja aliyeguswa na udhalilishaji huo.

Walimtwanga vitako vya bunduki dereva wa mbunge mwingine, Grace Kiwelu, wakavunja vioo vya gari na kumshambulia tumboni na kifuani.

Askari wa kiume walimshika vibaya na kumshusha suruali kwa nyuma, Josephine Mushumbusi, mchumba wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa. CCM walishangilia matukio hayo kwa sababu aliyedhalilishwa hakuwa mwenzao!

Leo polisi Igunga wanahaha kusaka waliomshughulikia DC, lakini hawajamtia mbaroni polisi hata mmoja aliyemdhalilisha Lucy na Josephine miezi minane iliyopita.

CHADEMA walipolalamikia unyanyaswaji huo, na mengine ya kukamatwa kwa wabunge wao wengine, CCM wakasema huo ni ulalamishi tu.

Nina hakika, kama DC angekuwa kwenye kazi halali, hata angetaka kuhudhuria mkutano wa hadhara wa CHADEMA, wasingemdhuru. Hata katika uchaguzi mkuu mwaka jana, wenzake kadhaa walifanya hivyo, wakapewa heshima kama viongozi wa serikali.

DC huyu amepatwa na masaibu haya kwa kuwa alijiingiza katika kampeni za kuibeba CCM; na bahati yake mbaya amenaswa katika mazingira yenye utata, akiwa na makabrasha yanayoonyesha dalili za hujuma za kisiasa dhidi ya wapinzani wa CCM.

Kwa watu walioonewa kwa muda mrefu, hakukuwa na hatua mbadala isipokuwa kumtia mbaroni na kumwondoa katika eneo husika. Yaliyoambatana na hatua hiyo ni mjadala mwingine ambao utatafutiwa nafasi yake.

Hoja hapa ni kwamba vijana wa CHADEMA wamepata ushahidi wa kuonyesha kwamba malalamiko yao ya siku nyingi si kulalama tu. CCM inataharuki kwa sababu aliyechukuliwa hatua ni kada wao.

Jeshi la Polisi linamwaga FFU mjini Igunga, kwa maelezo ya kulinda amani, lakini iwapo vijana watagundua nalo halitendi haki, hiyo amani haitalindika kirahisi – maana lazima wanaolindwa waone haki katika ulinzi huo.

Uhalifi hauchagui cheo cha mtu. Unaweza kufanywa na DC, polisi au wafuasi wa vyama. Na katika kauli hizi za “tusilaumiane kwa yatakayotokea,” ni dhahiri kwamba dalili za amani ya Igunga haziko karibu.

Lakini haya ni matukio yaliyoasisiwa zamani na watu wale wale waliokuwa wanashangilia matukio ya Arusha, huku wakibeza wanaolalamika.

Hawakuona ubaya wabunge “kudhalilishwa” lakini sasa wanaona haifai kwa mkuu wa wilaya kudhalilishwa. Nadhani, kama hawakumtuma, wangepaswa kumhoji kabla ya kumtetea.

Alikuwa anafanya nini katika siasa za wenye vyama vyao, yeye akiwa kiongozi wa serikali inayopaswa kutoa haki kwa vyama vyote?

Na sisi tunajiuliza, kama Nape ana huruma na anajali utu na heshima wanayostahili waheshimiwa hawa, kwa nini hakujitokeza Januari 5, kuwatetea wabunge waliodhalilishwa na polisi?

Na hili jeshi la vijana wa CCM wanalotaka kuliondoa kambini na kulimwaga mitaani dhidi ya CHADEMA, huku FFU wakiwa tayari wanarandaranda mitaani; lina hakika kwamba litalinda amani iwapo CHADEMA nao watatunisha misuli kwa nguvu waliyonayo ambayo hatujui mapana yake? Ndiyo amani na utulivu tunaoimbiwa?

Je nilitarajia kitu tofauti kutoka kwa Ngurumo? Jibu ni hapana. Yeye ni mlalamikaji na mkosoaji wa kila kitu kinachofanywa na serikali au vingozi wake. So far hakuna ushahidi kwa DC alikuwa kwenye mipango ya hujuma na wala hakatazwi kutembelea popote katika wilaya yake. Lakini kwa vile waliofanya hivyo ni wale wale waliozoea kuzua na ambao wanadhani kuzua pekee ndiyo mtaji wa kushinda uchaguzi. Ni kama walivyozua habari ya makontena yenye kura kule Tunduma kumbe hamna kitu.

Sishangai kwa mhariri msaidizi wa gazeti la CDM kutetea uhalifu wa chama anachokitumikia lakini haya yote yanamshushia hadhi kama mwandishi anayefahamika kwa weledi mkubwa kwa taaluma hii.
 
Another objective masterpiece from Ansbert Ngurumo.....READ ON!

===============================================================================
Wabunge wadhalilishwe, DC alindwe?

By Ansbert Ngurumo

TUSEME ukweli. Yaliyompata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, akiwa kwenye “uhalifu wa kisiasa” juzi si mazuri hata kidogo.

Lakini ni vema ukweli wetu uvuke hapo. Tumtazame kama kiongozi wa serikali katika eneo lake, na tumuulize: alijiingizaje katika siasa za vyama vya watu?

Alitarajia akisaidia hujuma za Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya wapinzani, wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wangemshangilia na kumpaka mafuta?

Mikakati ya ushindi wa CCM ilikuwa inamhusu nini? Hakujua kuwa kwa kitendo cha kujifungia ndani na makada wa CCM, alikuwa anahujumu haki na kuhatarisha amani yake na wengine?

Na kama alitaka kuwahujumu CHADEMA, ilikuwa lazima awafuate katika eneo walikokuwa wamepangiwa mkutano wa hadhara? Haiwezekani ameponzwa na ubabe na jeuri ya cheo na ukada usio mahali pake?

Kama alikuwa katika mkutano halali wa kikazi, kama watetezi wake wanavyodai, yeye kama mwakilishi wa rais katika eneo husika, kwanini hakuwa na ulinzi wowote hadi vijana wa CHADEMA walipomwokota na kumpa kibano?

Kama alivyohoji mtu mmoja jana, kama DC huyo asingewafuata CHADEMA huko walikokuwa, wangemtoa wapi “kumdhalilisha”? Na kama wao wangekuwa wanatendewa haki huko nyuma, na hata katika uchaguzi wenyewe wa Igunga sasa hivi, wangepata wapi hisia na sababu za kuhoji kazi aliyokuwa anafanya kwenye mkutano wa ndani, na hata kumtia mbaroni?

Bila kujadili uhalali au uharamu wa hatua waliyomchukulia vijana hao, nilipoona picha magazetini, DC akiwa ameshikiliwa kama mwizi, huku akiangua kilio hadharani, na baadhi ya wananchi wakishangilia, kumbukumbu zangu zilinipeleka katika tukio la aina hiyo Januari 5, mwaka huu mkoani Arusha.

Na baada ya kusikia viongozi makada, wanachama na mashabiki wa CCM wakilalamika kwamba Fatuma amedhalilishwa; na hasa baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kujiapiza jana kwamba “sasa liwalo na liwe, na kitakachotokea wasilaumiwe,” nikalazimika kukubaliana na usemi wa wahenga kwamba mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.

Katika tukio la Arusha, polisi – mbali ya kujeruhi kwa risasi na kuua raia watatu – waliwatendea vibaya baadhi ya washiriki wa maandamano, wakiwamo wabunge na wake za watu.

Kwa mfano, polisi wa kiume walimpiga ngwara Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya, akadondoka na kudunda kichwa chini kwenye barabara ya lami. Hakuna mwana CCM hata mmoja aliyeguswa na udhalilishaji huo.

Walimtwanga vitako vya bunduki dereva wa mbunge mwingine, Grace Kiwelu, wakavunja vioo vya gari na kumshambulia tumboni na kifuani.

Askari wa kiume walimshika vibaya na kumshusha suruali kwa nyuma, Josephine Mushumbusi, mchumba wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa. CCM walishangilia matukio hayo kwa sababu aliyedhalilishwa hakuwa mwenzao!

Leo polisi Igunga wanahaha kusaka waliomshughulikia DC, lakini hawajamtia mbaroni polisi hata mmoja aliyemdhalilisha Lucy na Josephine miezi minane iliyopita.

CHADEMA walipolalamikia unyanyaswaji huo, na mengine ya kukamatwa kwa wabunge wao wengine, CCM wakasema huo ni ulalamishi tu.

Nina hakika, kama DC angekuwa kwenye kazi halali, hata angetaka kuhudhuria mkutano wa hadhara wa CHADEMA, wasingemdhuru. Hata katika uchaguzi mkuu mwaka jana, wenzake kadhaa walifanya hivyo, wakapewa heshima kama viongozi wa serikali.

DC huyu amepatwa na masaibu haya kwa kuwa alijiingiza katika kampeni za kuibeba CCM; na bahati yake mbaya amenaswa katika mazingira yenye utata, akiwa na makabrasha yanayoonyesha dalili za hujuma za kisiasa dhidi ya wapinzani wa CCM.

Kwa watu walioonewa kwa muda mrefu, hakukuwa na hatua mbadala isipokuwa kumtia mbaroni na kumwondoa katika eneo husika. Yaliyoambatana na hatua hiyo ni mjadala mwingine ambao utatafutiwa nafasi yake.

Hoja hapa ni kwamba vijana wa CHADEMA wamepata ushahidi wa kuonyesha kwamba malalamiko yao ya siku nyingi si kulalama tu. CCM inataharuki kwa sababu aliyechukuliwa hatua ni kada wao.

Jeshi la Polisi linamwaga FFU mjini Igunga, kwa maelezo ya kulinda amani, lakini iwapo vijana watagundua nalo halitendi haki, hiyo amani haitalindika kirahisi – maana lazima wanaolindwa waone haki katika ulinzi huo.

Uhalifi hauchagui cheo cha mtu. Unaweza kufanywa na DC, polisi au wafuasi wa vyama. Na katika kauli hizi za “tusilaumiane kwa yatakayotokea,” ni dhahiri kwamba dalili za amani ya Igunga haziko karibu.

Lakini haya ni matukio yaliyoasisiwa zamani na watu wale wale waliokuwa wanashangilia matukio ya Arusha, huku wakibeza wanaolalamika.

Hawakuona ubaya wabunge “kudhalilishwa” lakini sasa wanaona haifai kwa mkuu wa wilaya kudhalilishwa. Nadhani, kama hawakumtuma, wangepaswa kumhoji kabla ya kumtetea.

Alikuwa anafanya nini katika siasa za wenye vyama vyao, yeye akiwa kiongozi wa serikali inayopaswa kutoa haki kwa vyama vyote?

Na sisi tunajiuliza, kama Nape ana huruma na anajali utu na heshima wanayostahili waheshimiwa hawa, kwa nini hakujitokeza Januari 5, kuwatetea wabunge waliodhalilishwa na polisi?

Na hili jeshi la vijana wa CCM wanalotaka kuliondoa kambini na kulimwaga mitaani dhidi ya CHADEMA, huku FFU wakiwa tayari wanarandaranda mitaani; lina hakika kwamba litalinda amani iwapo CHADEMA nao watatunisha misuli kwa nguvu waliyonayo ambayo hatujui mapana yake? Ndiyo amani na utulivu tunaoimbiwa?
Jamani wana CDM tupo wenyewe hatuna ulinzi wa dola wala mama yake JK. Tuwe pamoja sasa ni kipindi cha nguvu ya UMMA kufanya kazi hakuna kuogopa kwa sababu hata mkilala mtafuatwa vitandani mchapwe tufanyeje! PEOPLES POWER!!
 
kama ilivokuwa Tarime, ambako wafuasi wa CDM walicharangwa mapanga kwa nia ya kuwachokoza, ili amani ivunjike watumie nafasi hiyo kuiba ushindi, sasa hayo yanayofanyika ni maksudi ili kupata sababu ya kuwepo taaruki itakayowapa nafasi CCM kuiba ushindi. ni vema kama ccm inapenda amani kama inavyoubiri iache vitendo vya kichokozi na vitisho, maana amani ikivunjika haichagui, vinginevyo ni vema wakaangalia libya na misiri pamoja na mabavu ya watawala hatimaye wameng'olewa, isifike mahala tukalazima kuwapandisha kizimbani watawala wa ccm kwa kauli na matendo yao pale nguvu ya umma itakaposhinda
 
Jeshi la polisi na viongozi wasio weledi waliojaa uoga dhidi ya viongozi wa ccm ndio chanzo kikuu cha matatizo.
 
Ngurumo inatakiwa aelewe tofauti hapa; hao viongozi wa CHADEMA wamedhalilishwa na polisi wakati DC amedhalilishwa na viongozi wa chama cha siasa.

Hiyo ni tofauti kubwa sana. Chama cha siasa sio chombo cha dola na kina viongozi ambao wanatakiwa kulinda amani hata pale wanapokosewa.
 
Ngurumo inatakiwa aelewe tofauti hapa; hao viongozi wa CHADEMA wamedhalilishwa na polisi wakati DC amedhalilishwa na viongozi wa chama cha siasa.<br />
<br />
Hiyo ni tofauti kubwa sana. Chama cha siasa sio chombo cha dola na kina viongozi ambao wanatakiwa kulinda amani hata pale wanapokosewa.
<br />
<br />
Ok ni kifungu gani cha sheria kinachoruhusu police kunyanyasa raia?au na wewe ni walewale waliokunywa uji wa mgonjwa?
 
Back
Top Bottom