Anne Makinda: Sitogombea tena ubunge 2015

MBUFYA

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
445
68
Mh. Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano amesema kuwa hato gombea ubunge chaguzi mkuu ujao. Amesema anataka kukopa pesa arudi kujenga nyumba.

Spika wa bunge Mh Anna Makinda amesema ifikapo mwaka 2015 hatogombea tena ubunge. Ameyasema hayo leo alipokuwa anaongea na wapigakura wake katika jimbo la Njombe somewhere.

Amesema ameshikilia kiti hicho cha ubunge kwa miaka 17 na sasa amechoka na anahitaji kupumzika.

Source: ITV, HABARI YA SAA MBILI
 
Ubunge hauna maslahi, ni sehemu masikini ataka kufanya shughuli nyingine.
 
huyu mama anapaswa apelekwe mirembe akapimwe akili nimemsikia anasema miaka kadhaa ijayo watu kama maprofesa na wafanyakazi wengine hawata kua wanaacha kazi zao kwa kuwa bungeni kunawafanya watu kuwa masikini.....kwa nini wasiache sasa kugombea ubunge hadi wasubiri miaka kadhaa ijayo. Na amezidi kuzitetea posho mpya za wabunge.
 
Spika wa bunge Mh Anna Makinda amesema ifikapo mwaka 2015 hatogombea tena ubunge. Ameyasema hayo leo alipokuwa anaongea na wapigakura wake katika jimbo la Njombe somewhere.

Amesema ameshikilia kiti hicho cha ubunge kwa miaka 17 na sasa amechoka na anahitaji kupumzika.

Swali langu ni je, mama ameangalia alama za nyakati na kugundua hana tena mvuto kwa wapiga kura wake na Tanzania kwa ujumla au ameona chama chake cha CCM kinachungulia kaburi?
 
Asitufanye watoto wadogo,akakope hela akajenge nyumba na hizo asante toka ma mfsd alizopewa hazikutosha kujenga nyumba.?bora hasigombee tu tumemchoka
 
Hana jipya!
Amechoka akili na mwili, na anaelewa wazi kuwa changamoto za Bunge la sasa hatakaa aziweze!...Watu kama akina Tundu Lisu ni mwiba sana kwake, na anajua kuwa 2015 wataingia vijana matata zaidi na wabishi mno!
Namsifu kwa kuona zaidi ya pua yake!
 
Ni uamuzi wa busara sana. Amefika mahala ambapo si wengi wanafika. Ni mwanamke wa kwanza kuwa spika Tanzania, ameweka historia, umri nao umekwenda. Mimi nangoja mwaka wake wa mwisho nipeleke posa, atanifaa sana kumtazamia pesa atazokopa.

Nikichukuwa ngoma hiyo, itabidi niende kwa kuomba miongozo.
 
huyu keshagundua keshakuwa kero, hata akigombea hawezi kuchaguliwa, hata mimi nampongeza, ameshachangia kukidhoofisha chama sasa anasepa. MAKINDA OYEEEEEEE......
 
pia amesema bunge lipo frustrated kwa sasa!kisa kunyimwa posho!wanajimbo wamemwambia hata panadol hakuna wabunge posho
 
Huuu unafiki mkubwa kweli anasema akakope ili ajenge haya ni ya kweli au kutudharau tunasubiri mikopo ili tujenge? Makinda ni kweli hadi leo hana hata nyumba? alishakuwa mkuu wa mkoa,mbunge na leo spika.....kweli bibi kiroboto ameamua kututukana....Na hili ndilo lifanywalo na viongozi wa Tanzania wakidhani kuwa sisi hatuna akili......mi nimeona kama yule mama sasa kachanganyikiwa...
 
Back
Top Bottom