Anne Makinda: Sitogombea tena ubunge 2015

Mama hata usingejisumbua kutangaza kitu, wewe haumo kabisaaaaaaa hata katika vile viti 78 vya ubunge tunavyokusudia kubakishia CCM hapo 2015!!!!!!!

Kwa mtaji wa utendaji wako dhaifu na upendeleo uliokithiri huko bungeni, hata kwa dakika hii watu tunajiuliza kwamba ni lini tutautua huu mzigo mzito kidemokrasia kwa jina la Anne Makinda.

Yaani kura tutakayopiga 2015 na kuilinda vilivyo ni zaidi ya Tsunami mama usipime!!!!!!!!!!!!!!!!
 
.......nenda kaone ghorofa leke pale NJOMBE njia inayoteremka kwenda power station. Kuhusu, mkopo; Watu wengi wanaficha mali zao zilizopatikana kwa njio isiyo halai kwa KUKOPA; Mwisho wa siku mtasema amepata kwa ule mkopo. kumbe ni changa la macho tuu. NINAWASILISHA..
 
kina Zitto Kabwe walishawahi kusema hawagombei tena na wakagombea kama kawaida, si jipya hili kulisikia kwa mwana siasa
 
Mh. Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano amesema kuwa hato gombea ubunge chaguzi mkuu ujao. Amesema anataka kukopa pesa arudi kujenga nyumba.

Sorce: ITV, HABARI YA SAA MBILI

mama alikuwa anatoka mapovu huyo...eti wabunge wamejaa umaskini...eti anataka achukue mkopo ajenge nyumba...kufuru nyingine ...!
 
Alisema amegombea mara nane na mara zote ameshinda zidisha kwa tano ndo umri wake katika bunge.
 
Sishangai sana kuwa anakopa ili ajenge manake hata Pinda alidai ana mil 25 kwenye account yake
 
Tunamkaribisha mitaani kwetu. Hata hivyo posho kuzuiliwa zimewadhoofisha kwani lilikuwa ndilo tumaini lao.Pia amegundua 2015 ni mwaka ambao tuna msiba mkubwa wa furaha kwa kifo cha CCM na kamata kamata na kutaifisha mali za walioifikisha nchi hapa ilipo.
Kina JK wameshasoma alama za nyakati na hata bwana Nape ameshachungulia kifo cha CCM na hivyo wamesita kukifanyizia chama tawala cha 2015 CDM ili wakiwa madarakani wasije wakalipiza kisasi
 
Mwacheni akapunzike. Speed ya bunge la sasa lazime imemfanya aone siku zake mara nne kwa mwezi!
 
Jf funguka kwa upana kingereza wanasema read between lines. Ana maanisha tutegemee appartments zenye majina kama makinda tower, semamba tower anna makinda tower, ama majina ya wanawe hela aliyopewa na rostam bilion moja cha mtoto kumbuka amepindisha mengi zao lake ni ufisadi
 
Nenda mwanakwenda. Nani anahitaji fisadi kumwakilisha? Laiti ungekuwa na familia huu ungekuwa wakati mzuri wa kwenda kucheza na wajukuu. Hata hivyo wanasiasa wetu hawaaminiki. Atasema hivi kesho anabadilisha. Kwa uchu na tamaa ya pesa unadhani ataacha kugombea na kuchakachua uchaguzi?
 
Na ile nyumba aliyojenga halafu akafunga njia kiasi kwamba wananchi wa eneo lake wakawa wanalalamika?
 
Back
Top Bottom