TANZIA Anna Elisha Mghwira afariki dunia akipatiwa matibabu Hospitali ya Mount Meru

Aliyekuwa mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira amefariki dunia leo July 22, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha. Mama Mgwira alistaafu ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mei mwaka huu na alikabidhi ofisi kwa mrithi wake, Kigaigai Mei 27 mwaka huu wa 2021

Taarifa zaidi zinakuja

====

UPDATES:

====

Anna Elisha Mghwira (alizaliwa 23 Januari 1959) ni mwanasiasa. Alikuwa Mwenyekiti wa Alliance for Change and Transparency (ACT) aliyegombea urais wa nchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, alihamia chama cha CCM mwaka 2017.

Maisha ya awali na elimu

Anna Elisha Mghwira alizaliwa tarehe 23 Januari 1959 katika Hospitali ya Mkoa wa Singida, Kata ya Mungumaji - Kitongoji cha Irao katika Manispaa ya Singida-Mjini. Alikuwa mtoto wa nyumbani kwa sababu ya shida ya kiafya ambayo ilichelewesha uwezo wake wa kutembea.

Alijiunga na shule ya msingi ya Nyerere katika miaka ya 1968- 1974. Kisha akasoma shule ya Sekondari Ihanja kutoka 1975 hadi 1978 kabla ya kujiunga na Seminari ya Kilutheri kwa masomo ya A-level 1979 hadi 1981.

Alipata shahada yake ya kwanza katika theolojia kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipoongeza shahada ya sheria (LLB) mnamo 1986. Kwenye Chuo Kikuu cha Essex huko Uingereza aliendelea kusoma shahada ya uzamili ya sheria (LLM) mnamo 2000.

Mghwira alifanya kazi kwa mashirika ya kimataifa na ya Kitanzania yanayoshughulikia uwezeshaji wanawake, maendeleo ya jamii na wakimbizi.

Baba yake alikuwa diwani kupitia TANU. Anna alijiunga na umoja wa vijana wa chama cha TANU. Katika miaka ya 1970 alipunguza kazi yake ya kisiasa ili aweze kuzingatia masomo yake na familia.

Mnamo 2009 alirudi katika siasa alipojiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA. Bi Mghwira alishikilia nyadhifa tofauti kama katibu wa wilaya wa chama na baadaye mwenyekiti wa wilaya wa chama.

Mnamo mwaka wa 2012, alishindwa na Joshua Nassari katika uteuzi wa Chadema kwa uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki. Alifanikiwa kugombea kiti cha Bunge la Afrika Mashariki mwaka huo huo, lakini bila kuchaguliwa.

Mnamo Machi 2015, alihama Chadema kwenda chama kipya cha ACT-Wazalendo, ambapo baadaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa kitaifa wa chama wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa chama. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 aligombea urais wa Tanzania.

Mwaka 2017 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akaacha ACT-Wazalendo akahamia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Apumzike kwa amani sana.

Wajumbe tuendelee kuchukua tahadhari
 
Tumaini hakikuwa chuo kikuu miaka ya Mama Anna. Hata sisi watoto wake wakati tuko chuo kikuu, Tumaini bado hakikuwa university.
Alipata shahada yake ya kwanza katika theolojia kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipoongeza shahada ya sheria (LLB) mnamo 1986.
 
Back
Top Bottom