Angelina Malembeka Ashangazwa Askari Barabarani Kujificha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943
ANGELINA MALEMBEKA ASHANGAZWA ASKARI USALAMA BARABARANI KUJIFICHA

1685449281996.png

Agelina Malembeka, Mbunge wa Viti Maalum

Mbunge wa Viti Maalum Angelina Malembeka akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amehoji sababu za Askari wa barabarani kujificha porini badala ya kukaa barabarani na kuwasaidia Madereva.

Malembeka amesema “Kuna maeneo ambayo Polisi wanatupa kero wanaanza na king’amuzi wakishika mmoja wenye 90 yatapita magari hata 20 yataoneshwa magari yote 90 kama ving’amuzi vibovu vikatengenezwe au vinunuliwe vipya”

“Lingine wana mchezo wa kujificha utaona tu ghafla kakurupuka kwenye Mihogo sasa wewe ni Bwana shamba na kwenye Mihogo ulifuata nini, kaa barabarani tukuone kama kuna tatizo tusimame tukwambie kuna mwingine anamtaka Trafiki amuulize lingine wana ucheleweshaji usiokuwa na sababu anaweza kusimamisha magari halafu yeye anachati anasubiri Konda au Dereva aje sasa mnawatia hasira Madereva”
 
Waulize maswali ya maana kama kwa nini wizara ya mambo ya ndani huhitaji uthibitisho wa safari kwenye kutoa passport dunia hiinya leo ambako paspoti huhitajika kufanya mitihani ya kimataifa mfano ya Kingereza cha Kimataifa British Council nk pia huhitajika unapoomba vyuo vya kimataifa online au tenda au kuomba ajira za kimataifa online ukiwa ndani ya nchi ya Tanzania

Huo uthibitisho wa Safari mfano mtu anataka kuomba scholarship akijaza form online anakutana na sehemu anatakiwa aweke passport number na yeye hana akienda kuomba anaambiea kalete uthibitisho wa safari si kituko hicho

Traffic kujificha sahihi na hujificha maenro korofi unakuta vibao vya onyo viko kibai kuanzia spidi limit nk mtu hajali anakanyaga moto tu kitu ambacho ni hatari kwake na wengine

Naunga mkono Traffic waendelee kujificha machakani huko wamwibukie mvunja sheria asiyejali speed Limit wala vibao vya tahadhari

Sehemu isiyo na vichaka nashauri jeshi la polisi lijenge vichaka vya Traffic kujificha
 
Trafic ni watu wa hovyo sn, waondolewe vifungwe vifaa
Tii sheria za barabarani bila shuruti

Hata Traffic atoke kichakani atakukuta huna hatia unaogopa nini Traffic kuwa kichakani wakati si mhalifu

Kuendesha kwa peace of mind tii sheria za barabarani bila shuruti kuendesha utakufurahia
 
Peleka ujinga wako huko wewe mama, usumbufu tunaupata barabarani ni wakijinga na rushwa tupu
 
Mimi niko upande wa huyu mbunge. Kiukweli askari wetu wa barabarani hawana mchango wa kueleweka kwenye kupunguza ajali.

Maana madereva wengi, na hasa wale wa mabasi ya abiria, wamekuwa wakicheza mchezo wa paka na panya na hawa askari!

Na hiki ndicho chanzo kikuu cha hao askari kujificha juu ya miti, kwenye mashamba ya mihogo, maporini, na kutumia kila aina ya mbinu! Ili tu kutafuta namna ya kutengeneza mazingira ya kupata rushwa.
 
Zinahitajika road signs mahali panapostahili
Unakuta sharp corners au bend lakini hakuna sign yoyote, wanataka tuotee

Kama wanaiba wekeni tena na tena kama zimeoza wekeni zingine sio zikianguka mnaacha tu halafu ajali ikiuwa mnasema ilikata break

Sababu huwa wanatoa bila kusema ukweli kuwa kulikuwa hakuna sign yoyote
 
Ajali zimepungua wameshaanza kuwasemasema polisi tena. Fuata sheria wewe mbunge, haijalishi askari amejificha au yuko wapi, ukifuata sheria za barabarani hakuna atakayekusumbua.
 
Mimi niko upande wa huyu mbunge. Kiukweli askari wetu wa barabarani hawana mchango wa kueleweka kwenye kupunguza ajali.

Maana madereva wengi, na hasa wale wa mabasi ya abiria, wamekuwa wakicheza mchezo wa paka na panya na hawa askari!

Na hiki ndicho chanzo kikuu cha hao askari kujificha juu ya miti, kwenye mashamba ya mihogo, maporini, na kutumia kila aina ya mbinu! Ili tu kutafuta namna ya kutengeneza mazingira ya kupata rushwa.
Hizi zinaitwa 'mbinu za medani' na 'ujanja wa porini', mimi niko na askari wetu, fanyeni kazi yenu kwelikweli. Madereva wa Tanzania wengi wao ni watu wa hovyo sana, askari wakilegeza kamba kidogo tu basi ni ajali kila kukicha.
 
ANGELINA MALEMBEKA ASHANGAZWA ASKARI USALAMA BARABARANI KUJIFICHA

View attachment 2640334
Agelina Malembeka, Mbunge wa Viti Maalum

Mbunge wa Viti Maalum Angelina Malembeka akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amehoji sababu za Askari wa barabarani kujificha porini badala ya kukaa barabarani na kuwasaidia Madereva.

Malembeka amesema “Kuna maeneo ambayo Polisi wanatupa kero wanaanza na king’amuzi wakishika mmoja wenye 90 yatapita magari hata 20 yataoneshwa magari yote 90 kama ving’amuzi vibovu vikatengenezwe au vinunuliwe vipya”

“Lingine wana mchezo wa kujificha utaona tu ghafla kakurupuka kwenye Mihogo sasa wewe ni Bwana shamba na kwenye Mihogo ulifuata nini, kaa barabarani tukuone kama kuna tatizo tusimame tukwambie kuna mwingine anamtaka Trafiki amuulize lingine wana ucheleweshaji usiokuwa na sababu anaweza kusimamisha magari halafu yeye anachati anasubiri Konda au Dereva aje sasa mnawatia hasira Madereva”
Huyu mbunge kwanza huwa sio makini anapokuwa barabarani huwa anaingia tu kwenye barabara kubwa bila kujiridhisha kama kuna usalama. Alishawahi kupata ajali mahala akajaribu kumhonga askari trafiki aliyesimamia uchunguzi mwisho wa siku akajiuta amegonga mwamba baada ya kubainika tukio lilibadilishwa maana aliyegongwa alipiga picha baada ya tukio kabla gari halijasogezwa pembeni atapata aibu akalipa faini mahakamani. Na yeye azingatie sheria za barabarani kuliko kuwashambulia askari kwamba wanajificha
 
Hizi zinaitwa 'mbinu za medani' na 'ujanja wa porini', mimi niko na askari wetu, fanyeni kazi yenu kwelikweli. Madereva wa Tanzania wengi wao ni watu wa hovyo sana, askari wakilegeza kamba kidogo tu basi ni ajali kila kukicha.
Hakuna kitu kama hicho. Askari wa barabarani wana mchango mdogo sana kwenye kuzuia ajali. Mimi nawaona kama watu wanaofikiria kula rushwa tu kutoka kwa madereva.
 
Hakuna kitu kama hicho. Askari wa barabarani wana mchango mdogo sana kwenye kuzuia ajali. Mimi nawaona kama watu wanaofikiria kula rushwa tu kutoka kwa madereva.
Maumivu ya kutoa hizo rushwa ndio yanawafanya madereva watii sheria. Acha polisi wale tu.

Madereva wa Tanzania wanachoelewa ni matuta na tochi.
 
Back
Top Bottom