Angekuwa yule mnadhani angefanya kama anayoyafanya huyu?

Kwa timu ile ya mabepari na mabwenyenye waliokua wanampa pesa za nauli ya kwenda magogoni angeuza hata Mlima Kilimanjaro
 
Nauliza tu.

Na nauliza kwa nia njema kabisa.

Hivi rais angekuwa Lowassa, kupitia chama chochote kile, iwe CCM au CHADEMA, mnadhani angekuwa hata na uthubutu wa kuyafanya kama haya anayoyafanya rais Magufuli, kwa mintarafu ya hizi taarifa za tume ya kuchunguza mchanga wa madini?

Nani humu anayeamini kwa moyo wote kabisa kwamba Lowassa angeweza kuyafunua mambo ambayo kwa kweli yanaiweka CCM pabaya?

Nani humu anayedhani kuwa huyo poster boy wa ufisadi Tanzania angekuwa na uhalali wa mamlaka ya kimaadili kufanya kama anavyofanya sasa rais Magufuli?

Najua wengi wenu humu mnampinga Magufuli.

Pamoja na mapungufu yake, mimi naamini historia itakuja kumhukumu katika mwanga ulio chanya kwa kuwa rais mzalendo na mwenye uchungu na Tanzania.

Kama Kikwete watu mshaanza kumkumbuka basi sina kabisa shaka lolote lile kuwa hata Magufuli naye atakumbukwa vizuri tu.

Haya sasa kazi kwenu nyie wafia vyama na ukabila. Rusheni kejeli na tuhuma zenu kuwa mimi ni CCM na mkabila.
Mwaka 1995 Nyerere alionya Ubinafsishaji Wa NBC kuwa haiwezi kushindana na Mabenki makubwa mkampuuza.

Waliompuuza wapo na Leo wanajaribu kujifanya waganga .

Mwaka 2000 waliona watanzania wakishughulikiwa na viongozi wao waliowachagua kisa wanapinga uwekezaji.

Mwaka 2005 - 2015 walishuhudia watanzania mikataba ya gesi ikisainiwa haraka kwa wingi wa kura za kishindo.

Walipoambiwa kuwa tuichunguze mikataba na mirahaba ya madini walifukuzwa bungeni.

Leo waliojadili mikataba ndani ya Baraza la mawaziri,waliopiga makofi na kuunga hoja miamia,leo wanakuja na hoja" tumeibiwa na kutiwa hasara ya mabilioni"

Mganga hajigangi
 
Mimi ingekuwa ni wewe ningeuliza:-
HIVI KWANINI SISI CCM TULISHINDWA KUYAFANYA YOTE HAYA TOKA UHURU..?? LABDA LEO TANZANIA TUNGEKUWA DONOR COUNTRY......!!!! AU LABDA NCHI ILITAKIWA WAPEWE WAPINZANI TOKA MWANZO...!!!
Tatizo sio CCM wala upinzani, tatizo letu kama nchi ni hulka ya upigaji na deal, kama jamii tumeoza kimaadili
 
Kwanza watu wa kaskazini wangetumaliza aisee. Wangetuibia mpaka tujute. Walikuwa washajipanga namna ya kutumaliza Watanzania. Lile kundi lake wamekaa kama mafisi (wana uchu sana na mali). Hapa Rais aliekuwa anatufaa ni huyu huyu JPM. Mungu azidi kumlinda na kumuongoza atufikishe pazuri.
 
Hakuna kiongozi yoyote kutoka upinzani ambaye angeweza kuyafanya anayofanya Jpm, hilo hata wao wanalijua na ndiomana wapo kimya mpaka sasa.kwanza hawakuamini kama jpm angeweza, ndiomana akina tundu lissu walikuwa wakipiga kelele na kutaka kuuaminisha umma kuwa anachofanya jpm ni makosa, leo toka report imetoka ameufyata:D
Hawaamini. Walimchukulia poa sana.
 
Nauliza tu.

Na nauliza kwa nia njema kabisa.

Hivi rais angekuwa Lowassa, kupitia chama chochote kile, iwe CCM au CHADEMA, mnadhani angekuwa hata na uthubutu wa kuyafanya kama haya anayoyafanya rais Magufuli, kwa mintarafu ya hizi taarifa za tume ya kuchunguza mchanga wa madini?

Nani humu anayeamini kwa moyo wote kabisa kwamba Lowassa angeweza kuyafunua mambo ambayo kwa kweli yanaiweka CCM pabaya?

Nani humu anayedhani kuwa huyo poster boy wa ufisadi Tanzania angekuwa na uhalali wa mamlaka ya kimaadili kufanya kama anavyofanya sasa rais Magufuli?

Najua wengi wenu humu mnampinga Magufuli.

Pamoja na mapungufu yake, mimi naamini historia itakuja kumhukumu katika mwanga ulio chanya kwa kuwa rais mzalendo na mwenye uchungu na Tanzania.

Kama Kikwete watu mshaanza kumkumbuka basi sina kabisa shaka lolote lile kuwa hata Magufuli naye atakumbukwa vizuri tu.

Haya sasa kazi kwenu nyie wafia vyama na ukabila. Rusheni kejeli na tuhuma zenu kuwa mimi ni CCM na mkabila.
Hangekuwa na ujasiri wa kutoa maboko live namna hii!!!
Mtu kizungu tu kinaleta shida!!
Elimu Elimu Elimu.

No mikurupuko.

Mkapa na Kikwete wangesajiliwa ukonga au Isanga. (maximum security prison)
 
Hakika rais Magufuli anastahili pongezi kubwa sana kwa sababu ya walau kuanzisha mjadala wa kitaifa kuhusu hizi rasilimali za nchi.

Historia itamhukumu vizuri sana, naamini.
Ashakum sii matusi, Nyani Ngabu ukimpapasa mkeo unatengeneza mazingira kwa masela kumkuna kiulainiiii.

Hili neno "angalau amethubutu" ndio nalilinganisha na kumpapasa my wife wako.
 
Hakika rais Magufuli anastahili pongezi kubwa sana kwa sababu ya walau kuanzisha mjadala wa kitaifa kuhusu hizi rasilimali za nchi.

Historia itamhukumu vizuri sana, naamini.
Wa kwanza kushughulikiwa angekuwa JPM kuhusu kivuko na nyumba za serikali.
 
Suala la mikataba mibovu liliamshwa na upinzani kwa hiyo angekuwa Rais kwa kupitia upinzani angerekebisha tu. Kama angekuwa Rais wa CCM basi ingekuwa ni fait accompli tu.
Acha utani. Yani Lowassa asikilize anachoambiwa na Lissu, Mbowe, Mnyika?!! Unachekesha. Wote hawa aliwanunua, sasa wangekuwaje na say kwake! Nchi ingeendeshwa na Lowassa pamoja na rafiki zake (wenye uchu na rasilimali zetu, madaraka, 'madeal' na wakwepa kodi, wauza unga..). Mlishabikia 'usanii', bahati nzuri Mungu anatupenda Watanzania.
 
Back
Top Bottom