Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,258
- 34,205
Acha kumfananisha lowassa na mambo kipuuziSabalkheri wanaJF na Alhamisi njema kwenu nyote na popote pale mlipo pembe ya dunia hii.
Sasa leo hebu tulonge kidogo ki-nadharia tete. Nimekaa kwa muda mrefu sana sasa nikijiuliza juu ya swali hili bila kupata jibu la uhakika.
Tuseme ingetokea mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA ndo angeibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha urais mwaka jana.
Halafu baada ya kuanza kazi akafanya mengi kama aliyoyafanya rais wetu wa sasa MTUKUFU Dkt. John Pombe Joseph Magufuli...
Yaani akapiga marufuku safari za hovyo hovyo za nje ya nchi, akaagiza baadhi ya sikukuu za kitaifa tubadili namna tunavyozisherehekea kitaifa, akawa ni mtu wa kukaa nchini muda mwingi na kutuma wawakilishi pale inapobidi, akatumbua majipu hadharani na faraghani, akanunua ndege mpya kwa lengo la kufufua shirika letu la ndege, na kadhalika na kadhalika.
Swali ibuka ni je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?
Au wangemmiminia sifa kemkem na kusema kwamba acha awanyooshe maana walikuwa wamezoea?