Angekuwa mkeo ungemfanyaje??sad news

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Zainabu matatani kwa kutupa kichanga chooni

6186954.jpg

Tuesday, January 10, 2012 11:21 AM
BI.ZAINABU SAID [24] mkazi wa Kiwalani jijini dar es Salaam, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kutupa mtoto wake mchanga chooni.

Taarifa hiyo ilisema mwanamke huyo alitupa kichanga hicho cha siku moja choooni

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema kuwa kichanga hicho kilitupwa chooni na mwanamke huyo kwa sababu ambayo haijafahamika hadi sasa

Kamanda huyo amesema kuwa, majira walioposhitukia tukio hilo waliweza kutoa taarifa kituo cha polisi, na Jeshi hilo kufika eneo hilo kwa ushirikiano walifanikiwa kukiopoa kichanga hicho ambacho tayari kilikuwa kilishakufa

Amesema kichanga hicho kilichukuliwa na kwenda kuhifadhiwala katika Hospitali ya Amana huku mama huyo akiwa anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi kubaini alifanya tukio hilo kwa makusudi ama alikuwa na matatizo ya akili
 
Nahakikisha amefungwa maisha! yaani asione jua tena na wala asipate fresh air tena, makazi yawe kwenye chuma cha 5X6 for the rest of her life!
 
Pumbavu zake alipokuwa anapanua mapaja hakujua,kwamba anapanda mbegu,funga jela miaka 40 na bakora 12 kila siku monie 6 na jioni 6.
 
post natal depression. Ndo kwa maana huchargiwa na infanticide na sio murder. Na omba radhi kwa kiswahili changu. Nime join forum hii ili ni ongeze umarufuu kwa lugha. Mimi ni mkenya
kwani hapa ni shule ya kiswahili?
 
MUNGU AMSAMEHE dhambi aliyofanya ni kubwa na yakutisha sana. Naimani sheria itamsweka jela 50 yrs
 
madaktari wanasema mwanamke anapojifungua akili yake humruka kwa hivo hata kisheria kama alivosema mwenzetu wa kenya na hata kwetu hawezi kushtakiwa kwa kosa la mauaji bali infanticide kiswahili kigumu, penal code imeainisha mazingira gani ya namna hiyo
tusimlaumu sana wacheni mahakama ithibitishe pasi shaka kama ana hatia. hivi hamjawahi kusikia visa vya mama kuwalalia watoto wao bahati mbaya hadi kufa wakiwa usingizini mara wanapojifungua? kwani hamwoni vituko wanavokuwa navo kina mama wajawazito?
someni hapa kwa maelezo zaidi na picha, http://www.drabruzzi.com/infanticide.htm na
http://en.wikipedia.org/wiki/Infanticide
Post natal depression. Ndo kwa maana huchargiwa na infanticide na sio murder. Na omba radhi kwa Kiswahili changu. Nime join forum hii ili ni ongeze umarufuu kwa lugha. Mimi ni mkenya
 
Asee na maumiv yooote
ya kudeliver na kutemamate
anathubutu kutupa mtoto?my god kunawamama wanavizia hospital kuiba watoto
ajil wanawasaka bila mafanikio af ye anatupa?kwel alirukwa na akil loool
 
katika hali ya kawaida, hakuna binadamu anaweza akatupa au kuua mtoto wake. Mwanamke aliyebeba mimba kwa miezi 9, ametapika, ameshindwa kulala, amepitia mengi sana, na kwa hali ya kawaida HAWEZI KUUA mtoto. Hebu tujiulize, ni wanawake wa aina gani wanatupa/kuua watoto? Utakuta kwamba wanawake wengi walio kwenye ndoa huwa hawatupi watoto. Mara nyingi wanawake wanaotupa watoto ni wale waliopata ujauzito wao kwenye mazingira ya kutatanisha, labda ni wanafunzi au wasichana wamedanganywa na wanaume na hawaoni njia mbele, ndio maana wanafanya maamuzi magumu, WAKATI AKILI ZAO ZIMEWARUKA.
Nakumbuka story ya mama mmoja, mwenye watoto 6, na alikuwa amekimbiwa na mumewe. Maisha yake yalikuwa ni ya kuunga unga sana, anauza genge ili kuweza ku support watoto wake. siku moja badala ya kuhangaika sana, alipata tshs 500 na mwanae mmoja akaiiba. Yule mama kwa hasira, alimpiga mwanae na kumuua. Jugde alimwachia yule mama kwa kuzingatia mazingira ya maisha yake; 500 ndio pesa aliyotegemea kulisha wanae 5, kwa maana hiyo ilipoibiwa, hakuweza kustahimili!

Jamani, ni rahisi sana kuwalaani wanaotupa watoto, ila ni vema to READ BETWEEN THE LINES.
Hakuna mwanamke mwenye akili timamu anayeweza kutupa mtoto aliyemweka tumboni miezi 9.
 
Thread inasema angekuwa mkeo ungefanyaje?

Lakini habari yenyewe imekaa kama taarifa tu, mhusika hakuwa na mume yawezekana alipata ujauzito bila matarajio yake na huyu aliyempa ujauzito hajamfahamu na ugumu wa maisha imani imemshinda kaona atampa shida kichanga chake alichokizaa.

Serikali yetu ingekuwa na huruma ingekuwa inawasidia hawa wamama waliopata ujauzito kwa bahati mbaya kutokana na hali zao ngumu kimaisha haya yasingekuwa yanatokea. kuna nchi zingine zinawasaidia hawa kina mama.

Tatizo ni Serikali yetu hii nchi inahitajika iongozwe kimajimbo ili iweze kuwa serikali ya kuhudumia watu wake na si mafisadi peke yao
 
Post natal depression. Ndo kwa maana huchargiwa na infanticide na sio murder. Na omba radhi kwa Kiswahili changu. Nime join forum hii ili ni ongeze umarufuu kwa lugha. Mimi ni mkenya
Karibu sana. Utajifunza tu, wako wengi walikuja hawawezi hata kuandika kama wewe.
Hiyo PND ni mbaya sana, mi nina binam yangu alijaribu kujiua mwenyewe, alipo ulizwa kulikoni akasema anajiskia vibaya sababu alipo kua mzito attention yote ilikua kwakee, mara baada tu ya kujifungua attention ikashift kwa mtoto, basi anaona awapishe walimwengu wakae na mtoto yeye ajifie tu... Ingekua mimi mshirikina haki ya nani tena ningejua ni pepo limemkaba!
 
Sioni maana ya kumtetea. Mbona wanao zaa ni wengi? tusubiri kwanza tuone majibu ya hospitali. Ukute alitaka kuficha tu kua hana mtoto... Mungu amlaze malaika wake mahala pema na amsamee huyu mwanamke kwa maakosa makubwa alio yafanya.
 
Post natal depression. Ndo kwa maana huchargiwa na infanticide na sio murder. Na omba radhi kwa Kiswahili changu. Nime join forum hii ili ni ongeze umarufuu kwa lugha. Mimi ni mkenya

Umarufuu
= umahiri wa lugha
Nimejoin=nimejiunga
Murder=mauaji
Infanticide = mauaji ya watoto wachanga

Turudi Kwenye topic: huu ni unyama mkubwa kutupa kiumbe asiye na hatia
 
huyo mama hana adabu kwani alipokua anastarehe kwenye kitanda alikuwa hajui kama dudumimba ataingia?afungwe jela na aekewe gesi ya nitrogen dioxide aone raha!
 
Back
Top Bottom