Angalizo: Tusilalamikie RUSHWA ni Msingi uliojengwa ndani ya CCM

Magimbi

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
1,434
1,210
Nilimsikiliza vyema mwenyekiti wangu wa Chama Jpili Tarehe 2/2/2014 hasa juu ya suala zima la rushwa ndani ya Chama. Kwa kifupi rushwa imo ndani ya mishipa ya Chama tena imejengeka kwa dhati katika ngazi ya chini zaidi ya Chama. Nazungumzia uzoefu wangu kwa maeneo niliyowahi kuishi na kushuhudia haya. Imefikia hata kiasi kwamba ukishutumu watendaji wa chama juu ya kukithiri kwa rushwa miongoni mwa viongozi wetu katika ngazi ya kijiji, wanakuita eti wewe upinzani. Hata ukiwaelewesha agenda ya kuchukia rushwa iko katika miiko ya uongozi ya CCM iliyorithiwa toka TANU..hawaelewei wanakuona unapotoka ni wachache mno watakao kuelewa. Ndio nikagundua kuwa wanachama weeengi tena mamilioni wa CCM hawajaisoma katiba ya Chama na hawaijui ama wanaipuuza kwa wanaoijua ndio maana wanadhani RUSHWA ni msingi wa kuimarisha CHAMA. Kwa sababu hiyo ndio maana inatolewa kwa uwazi hasa kipindi cha uchaguzi wa ndani hata nje ya Chama. Na wanaokemea hawana dhati ndani ya mioyo yao!!!

Rushwa ilikuwepo toka awamu ya kwanza lakini katika awamu ya tatu ilienea kwa kasi sana kwenye mishipa ya chama hasa baada ya kutungwa kwa ile sheria ya "TAKIRIMA" hapo ndipo kansa hii imeshindwa kabisaa kutoka kwenye mishipa ya wanaccm katika ngazi zote za uongozi. Kwa kweli suala la rushwa katika CCM halitaweza kuisha wala kumalizika kabisa na ishakuwa ni kasumba. Na kwa minajili hiyo basi itakuwa ni ngumu tena saana sana kukirudisha Chama kwa wananchi wa kawaida yaani sisi wa Jembe na Nyundo. Matajiri waliovamia CCM kuanzia awamu ya PILI ya Utawala hawawezi kuachia CHAMA kirudi katika misingi yake asilani sababu wanakihitaji kuliko wanavyokihitaji wakulima na wafanyakazi wa NCHI hii.

Hapa GREAT THINKERS bila kupoteza muda ni afadhali tuanze kushauri jinsi gani tunaweza kuiondoa rushwa ndani ya CCM na baadae tukikabidhi kwa walee wakulima na wafanyakazi kama katiba yetu inavyosema. Kama huna ushauri tafadhali usitamke maneno ya maudhi..Mods muwe macho na watu wa aina hiyo!!! CCM sio mbaya kwa misingi na miongozo yake (KATIBA) ila wanaokiendesha chama wengi wao ni walafi na wanafiki mnoo na wanatumia mazoea kukiendesha!!

CC: CCM fellows JF
 
Magimb
CCM ni majanga kwl, yaan imetufanya wananch tuwe maskin kwl, mtu akiishabikia ccm atakuwa hana akili pia anahitaji maombi, ukiishabikia ccm ni kama unashabikia shrtan
 
Ommy255
Mimi hata sioni aibu kuipenda CCM siwezi kuishabikia hivi ni vitu viwili tofauti kabisaa. Nitaipenda kwa sababu Katiba yake ni miongozo mizuri mno kwa maisha ya watanzania amini hilo. Sema kushabikia viongozi wake waliokipotosha chama sintoweza. Kwa kupenda madaraka wakawa wanawahoga wananchi vijijini wawapigie kura ktk chaguzi za ndani za uteuzi mwishowe wananchi wamejijengea utamaduni wa nipe nikupe..wameimarisha rushwa kwa makusudi sababu wawahi kufanya biashara kupitia CCM..Nooo haiwezekani lazima tutafute namna..endeleeni kushauri wadau!!
 
Back
Top Bottom