Angalia mkataba wa Sweden na UAE ulivyotoa haki na wajibu kwa pande zote mbili. Ulinganishe na wa kwetu

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,521
74,292
Ukiusoma, kila upande umelinda maslahi yake. Arbitration, wanaanza wao wanaohusika, then wakishindwa wanamtafuta msuluhishi kwa kila upande kuleta mtu wao wakisimamiwa na third party ambaye watamchagua wao wawili. Ikishindikana hapo wanakwenda ICSDI...unaona kabisa hakuna aliye dictate terms kwa mwenzake!


Wanasheria wetu walikwama wapi, kwanini hawakupata ushauri toka kwa watu ambao walishaingia mikataba kama hii ya kimataifa!

Read! Erythrocyte
 

Attachments

  • SWEDEN UAEMIRATES CONTRACT.pdf
    645.7 KB · Views: 5
wanasheria wetu walikwama wapi, kwanini hawakupata ushauri toka kwa watu ambao walishaingia mikataba kama hii ya kimataifa!

Read! Erythrocyte
Nasikia sisi tuligoma kufanya evolution

Wenzetu wapo stage ya 6 sisi bado tupo stage ya pili
 

Attachments

  • mqdefault.jpg
    mqdefault.jpg
    8.8 KB · Views: 2
Tumeshindwa hata kupenyeza wawekezaji wetu wa mnyama mbuzi kupeleka nyama UAE bila kuelezea mazao mengine kama parachichi, matofali ya dhahabu, mawe ya almasi, mazao ya matunda n.k
 
Mnacomment bila hata kuusoma msichotaka ni migogoro kwenda kusuluhishwa na third part na hapo mbona mkataba huu ulioleta tena wa mwaka 90 na wamesema wazi migogoro itaenda kushughlikiwa kwenye mahakama ya kimataifa nje ya sweden au emirati na wahusika kwenye hio mahakama ikiwemo wanatoka katika nchi hizi zinazoingia mkataba hawataruhusiwa kusuluhisha kwenye arbitration atateuliwa mwingine. Mbona imefanana tu na huu. Japo umesema muda ni miaka 20 hata huu wetu hicho kinarekebishika kiufupi lugha ni ile ile na huu wetu.
 
wanasheria wetu walikwama wapi, kwanini hawakupata ushauri toka kwa watu ambao walishaingia mikataba kama hii ya kimataifa!

Read! Erythrocyte
Hii ndiyo IGA Ile yetu ni transformed and distorted specific project contract introduction between two governments, kwani inahusu bandari na logistics corridors upande mmoja tu.
Marekebisho yakiwa bilateral investments hakuna shida.
Ni muhimu IGA iwe bilateral na siyo unilateral.
 
Mkuu natamani niufungue Ila nahc uvivu balaa km unavyotujua black people , kwan PDF hii ina page ngp kwanza?
Ziko page 13..

Ni rahisi mno kuusoma na kuelewa..

It quite different from ours in almost all aspects, Examples;

1. Huu unajenga mahusiano ya kijamii na kiuchumi kwa usawa kwa kila nchi kulinda investors wa pande zote mbili wanaokwenda kuwekeza ktk nchi hizi rafiki zilizosaini mkataba huu wa mahusiano haya i.e UAE na Kingdom of Sweden. Kinyume chake, huu wa kwetu unatoa jukumu ktk aspects zote kwa upande mmoja wa pili tu yaani TZ kutekeleza lolote inachotaka Dubai. Kwa kifupi mkataba kati ya TZ na Dubai ni mkataba wa kinyonyaji na uliojaa hila ndani yake

2. Mkataba kati Dubai na TZ una contradictions kibao. Kuna maeneo unaitaja TZ kama imeingia mkataba huu na Dubai kama nchi na maeneo mengine inaonekana kama vile TZ imeingia mkataba huu na kampuni ya DP World kama kampuni..

3. Mkataba kati ya UAE na Kingdom of Sweden hautaji eneo specific la kiuchumi bali unasema kuwa watashirikiana ktk eneo lolote la kijamii na kiuchumi Kwa kadiri watu au shirika au kampuni za nchi husika zitapoona fursa ya kufanya ktk nchi rafiki. Huu wa kwetu hawa Dubai kupitia kampuni yao ya DP World wamekuja wakilenga eneo la bandari tu huku mkataba ukiwa kimya kwa Watanzania kwenda kufanya chochote huko nchi Dubai..!!

4. Huu hauna ma - complications ya kimitego tego kama vile instrument of full powers na Saini za ajabu ajabu. Huu wa jamaa hawa uko simple and clear na hauna vimitego vya ajabu ajabu vyenye viashiria vya hila na ulaghai..
 
Mnacomment bila hata kuusoma msichotaka ni migogoro kwenda kusuluhishwa na third part na hapo mbona mkataba huu ulioleta tena wa mwaka 90 na wamesema wazi migogoro itaenda kushughlikiwa kwenye mahakama ya kimataifa nje ya sweden au emirati na wahusika kwenye hio mahakama ikiwemo wanatoka katika nchi hizi zinazoingia mkataba hawataruhusiwa kusuluhisha kwenye arbitration atateuliwa mwingine. Mbona imefanana tu na huu. Japo umesema muda ni miaka 20 hata huu wetu hicho kinarekebishika kiufupi lugha ni ile ile na huu wetu.
Kwani hapo wamesema wanawekeza kwenye nini? Sisi tunatetea sheria yetu ya Ulinzi wa Mali Asili za nchi ya mwaka 2017 inasema.

1. Mikataba yoyoteinayohusu Rasimali Asili za Taifa itakayosainiwa na serikali lazima ikaidhinishwe na Bunge.

Kipengere hiki kinaenda kinaondolewa automatic na Mkataba huu wetu na Dubai cos mkataba umetamka mikataba hiyo itakuwa ni siri, na ndiyo maana serikali inapeleka marekebisho Bungen mwezi 9 kifungu hicho kinaenda kueditiwa mikataba iishie kwenye Baraza la Mawaziri.

Historia ya uwepo wa kifungu hiki inatokana na mikataba ya madini iliyosainiwa huko nyuma mpaka kuja kufukuzana na Acacia Mining cos ilikuwa mikataba mibovu kwaiyo kipindi hiko ikaona iweke kipengere hicho ili umma ujie Viongozi wao wanafanya nini katika rasimali zao.

2. Sheria pia inasema migogoro yoyote inayohusu Rasimali asili za nchi itasuruhishwa katika mahakama zetu za ndani.

*Sheria inasema hivi alafu waliosaini mkataba wamesaini usuruhishi ufanyike Africa Kusini! Hii ni kinyume na sheria zetu na ndiyo maana umeona Mahakama inasema imekubaliana na walalamikaji juu mkataba huu kuvunja sheria zetu.

Kwaiyo tunaotetea, tunatetea kwa mujibu sheria yetu inavyotaka.

Huo mkataba wa Sweden na UAE wala haujaelekeza Kampuni fulani ndiyo inaenda huku tu! Na ndiyo mkataba wa ushirikiano kati ya nchi na nchi na ndiyo maana haujaweka eneo specific kama Bandari etc.

Ila we tu una maeneo specific kabisa na kampuni imetajwa kabisa, sasa jiulize tumesaini mkataba wa ushirikiano kati ya nchi na nchi au nchi na kampuni?
 
wanasheria wetu walikwama wapi, kwanini hawakupata ushauri toka kwa watu ambao walishaingia mikataba kama hii ya kimataifa!

Read! Erythrocyte
Wananchi wamesema sana kwamba IGA yetu ni ya upande mmoja. Ushauri wa wazee wa CCM ka.a akina Butiku na Waryoba hawataki kuusikia wala kufuata. Sasa wanaenda kufuta sheria ya ulinzi wa rasilimali zetu badala ya sheria hiyo kuiweka kwenye katiba ya nchi kama tulivyofanya kwenye ile sheria ya kuhamishia Dodoma makao makuu ya nchi.

Madhara yake yatakuwa makubwa kwa CCM, mwaka 2025 haitakuwa rahisi kwao kushinda uchaguzi mkuu. Huu ndiyo ukweli, ccm imeamua kujimaliza (committee suicide) yenyewe. Wahenga walisema ngoma ikilia sana hupasuka yenyewe. Hatupendi hili litokee.
 
.


Ibara ya kwanza Article (1)
Definition ya Investors inawapa nguvu wa sweden kuwepo nyuma ya D P.W yaani inaweza kutuchapa ikibidi. Hatari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom