Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 975
- 47
siku za nyuma nibahatika kutembelea magereza ya Zanzibar....na moja ya historia kwa nini magereza zanzibar inaitwa chuo cah mafunzo ilikuwa ni hii story hapa juu. ni kwamba baada ya mtoto huyu wa karume kuua baba yake alimpeleka gerezani ili kumfunza adabu kwa muda na toka wakati huo magereza zanzibar yakawa yanitwa chuo cha mafunzo. je, historia hii inatoposha au ally karume anasema uongo? nisaidieni wadauAnayeutaka urais SMZ akana kuua
Salma Said, Zanzibar
MWANADIPLOMASIA maarufu nchini Balozi Ali Karume amesema hana rekodi ya aina yoyote inayohusiana na mambo ya uhalifu yakiwemo ya kuua msichana enzi za ujana.
Balozi Karume alisema yeye ni msafi na yanayosemwa na watu ni uzushi mtupu wenye lengo la kuharibu jina lake kimataifa.
Balozi Karume alikuwa akijibu baadhi ya shutuma ambazo ziliandikwa katika vipeperushi mbalimbali na kusambazwa katika mji wa Unguja vikimtaja kwamba hana sifa za kugombea urais wa Zanzibar kwa madai ya kwamba alihusika katika mauaji ya msichana Asha Ismail Ahmed miaka ya 1970.
"Nawajibu watu hao, kwamba ninazo sifa zote za kuwa rais katika nchi hii, mimi sihusiki na tuhuma hizo ambazo watu wamekuwa wakinizushia,"alisema balozi.
Karume alisema shutuma hizo zilizoandikwa kupitia vikaratasi ambavyo vilisambazwa mjini hapa vikiwa na maandishi yaliyodai alihusika katika kifo cha msichana huyo ni za uongo na zinalenga kumchafua.
Vipeperushi hivyo vilisema Ali Karume katika miaka ya 60- 70 alitumia vibaya madaraka ya baba yake kwa kusababisha mauaji ya msichana huyo ambaye mwili wake ulitupwa katika uwanja wa Teniss hapo Maisara.
Kipeperushi hicho kilidai kwamba mara baada ya Ali Karume kufanya unyama huo, alikimbilia nje ya nchi, huku baba yake akipeleka ubani wa Sh 15,000 ambao ulikataliwa na ndugu wa familia.
"Huo ni uongo na uzushi....kama kweli basi nisingekubaliwa kuwa balozi na kuziwakilisha nchi mbalimbali nje ya nchi,"alisema balozi
Mwanadiplomasia huyo alikuwepo nchini kwa ajili ya maandalizi ya ziara ya rais wa Uturuki Abdallah Gul ambaye alizuru Tanzania akiwa mgeni wa rais Jakaya Kikwete.
Balozi Ali Karume ambaye ni ndugu yake rais wa Zanzibar Abeid Amani Karume alitangaza nia yake ya kuwania urais wa Zanzibar tangu mwaka jana wakati wa mkutano wa mabalozi wote wa Tanzania waliopo nje ya nchi.
Hivi karibuni alipokuwepo Zanzibar alisema nia yake ipo, lakini anatafanya utafiti na kushauriana na watu mbali mbali kuhusu suala hilo.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na tabia ya kusambazwa vikaratasi kwa watu mbali mbali ambao hutajwa kwa njia moja au nyengine nia ya kuchukuwa fomu kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Baadhi ya watu ambao tayari wameandikiwa vikaratasi hivyo na kusambazwa mjini hapa ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mohamed Seif Khatib pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk Hussein Mwinyi.
Last edited: