Anayepinga kuboreshwa kwa maslahi ya Mwalimu ni Mwalimu, hii ni ajabu sana

Ukitoa mapendekezo juu ya masilahi kwa walimu wanaopinga Ni Walimu wenyewe hivi kwanini lakini, mfano... mapendekezo ya kuwepo kwa;

1. Teaching allowance.
2. Mafunzo kazini Mara mbili kwa mwaka.
3. Kuwekwa muundo wa Shahada ya Pili (masters) kwenye utumishi.
4. Shule za hostel kuwe na shift ya mwl kulala na watoto kwa uangalizi
Najubaliana, ila hilo la mwalimu kulala hosteli hapana. Kazi ya mwalimu i kufundisha na siyo kulea watoto. Acha ubwege.
 
Vipi kwa walimu walio na PhD? serikali ingeona umuhimu wa kuwajali kimaslahi watumishi waliojiendeleza na kupata Masters na PhD maana hadi kutunukiwa hizo shahada kuna juhudi kubwa wamefanya (msoto hasa na wengine wanaambulia patupu)......hii itafanya hata wawapo kazini wazitendee haki hizo shahada zao maana watahisi kuthaminiwa. Tofauti na sasa ambapo uwe umesoma Masters au PhD wanaku treat sawa na wale wenye shahada moja mlio anza nao kazi kwenye kupanda vyeo na hata mshahara mnalingana tu.​
 
Hii inaweza kuwa njema lakini isiwe na tija sana kwa sababu wengine wanasoma kufikia hizo rank za PhD kwa ajili ya kupata heshima au kwa ajili ya wao kuonyesha profiles zao (Gomez and Gomez, 1984).

Kwenye hili nadhani walimu wasome kutokana na hitaji la fani yake kufikia ngazi hiyo ya elimu kwa lengo la kurudi kutumikia kile kilichodhamiriwa.

Kwa upande wa maslahi, wapinga maslahi ni wale wenye elements za uchawi tu maana kwenye maendeleo ndo wachawi wengi 😎
 
Huwezi kulipa taeching allowance kwa walimu ambao ndo idadi kubwa ya watumishi,,makusanyo yetu bado madogo hii kulipa allowances labda kwa Askari ambao ni wachache kwa idadi yao,,,ukisema ulipe walimu woooote allowances hizo utajikuta bill ya mishahara na posho inafika trillion 1 kwa mwezi huku makusanyo ni trilion 1.9 hivyo labda cha kupigania ni kuongezwa mishahara kila mwaka na madaraja yasicheleweshwe
Zungumzia bajeti ya magari ya serikali na ghalama za misafara ya viongozi pia
 
Niliwahi pendekeza hapa kuiomba serikali iweke muundo wa kiutumishi na kimasilahi kwa Walimu wenye Masters, Walimu walikuwa wanapinga tu Uzi wangu🤣🤣
Walimu sijui wanachuki binafsi au ni shida ya mtu binafs
Walimu wengi hawajitambui.
Watu wa hivyo lazima wawe na chuki, fitina na uchawa mwingi!
In the end wanakuwa hawajui hata wanachokipigania!
Huamini utaona wanapigana vikumbo kupata nafasi za ukarani wa sensa au kura, chanjo n.k. Au utaona wanapanga foleni kupewa vishikwambi... Wakipata Roho kwatu kabisa hawana shiiidaaaa!
 
Back
Top Bottom