Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Yule mshenzi alifanya nchi hii kama koloni lake. Sasa anavuna alichopanda mbuzi na nusu!!!
 
Watu wengi hawajui. Prof. Asad alifanyiwa unyama mwingi. Kutekwa kutishwa, na marehemu akasema kwamba, 'anajifanya mjanja, ngonja uchaguzi upite, atapotea'. Lakini Asad hakuyumba katika msimamo wake wa kutomlamba nyayo ili apate ulaji.

Katika watu wenye misimamo thabiti, hakika Asad ni mmoja wao. Si wengi ambao wana uwezo wa kuhimili aliyoyapitia. Tangu kuondolewa kwake ameishi maisha ya kawaidia sana, maisha ya chini, ilhali angekubali kulamba tu nyayo za mfalme, angeishi kwa starehe.

Sijui kwa nini, marehemu hakuwa na amani, kila mara alimtafuta kwa simu. Baadaye Asad alimblock. Marehemu Kijazi akawa anatumika kumlainisha lakini Asad hakubadili msimamo wake.

Mungu hamtupi mwenye haki.
 
Utawala wa Jombe Pombe ulikuwa ni utawala wa kishenzi sana, Ni utawala wa kijinga mnoo, ni utawala uliokuwa haujui hata unafanya nini, haukujua hata kesho kutatokea nini, haukuwa na uwezo wa kuona mbali, ilikuwa ilimradi tu panakucha na script mpya, Kauli zake hazizkuwa za kiuongozi, zilikuwa ni kauli za majivuno na ujuaji mwingi. kwa kifupi Mungu ameamu kutupa pumzi mpya.
kwa kutokujua nini wanafanya ndo maana kifo kuugua kwa mpaka kifo walificha na wakaendeleza kupambana eti mi anapiga kazi(Pm majaliwa)
 
Ndio naiona hekima ya kukatazana kumsema marehemu,kwa sababu kinachoendelea ni sawa na kusikiliza kesi upande mmoja tu na kisha kutoa hukumu.
Wanasema mwosha huoshwa. Marehemu alipokuwa hai, alizuia vyama vya upinzani kuongea, aliwazuia critics wake kuongea, sasa na yeye amezuiwa kuongea, huku aliowazuia wakipata nafasi ya kuongea.

Jambo hili liwe fundisho kwetu sote kuwa hata tuwe na nguvu kiasi gani, zina ukomo maana juu yetu kuna mamlaka isiyobishaniwa, na ukuu wake haujadiliwi.
 
Nchi hii haikuwai na haitakuja kupata kiongozi mshenzi na fedhuli Kama Magufuli. Kati ya sehemu ambayo nitawalaumu milele CCM na TISS yao ni hapa , iweje walazimishe watanzania tuongozwe na mtu mshenzi Kama yule??
Akawa anatuongopea eti yeye ni mzalendo, kumbe ni mwizi, jambazi na liporaji la fedha za umma!
Hili dubwana limeila sana nchi
 
Wanasema mwosha huoshwa. Marehemu alipokuwa hai, alizuia vyama vya upinzani kuongea, aliwazuia critics wake kuongea, sasa na yeye amezuiwa kuongea, huku aliowazuia wakipata nafasi ya kuongea.

Jambo hili liwe fundisho kwetu sote kuwa hata tuwe na nguvu kiasi gani, zina ukomo maana juu yetu kuna mamlaka isiyobishaniwa, na ukuu wake haujadiliwi.
Sasa ukizungumzia hiyo mamlamka ya juu ni kwamba wengine imani zao zinakataza kumzungumzia vibaya marehemu hayo ni maelezo kutoka hayo mamlaka ya juu kwa baadhi ya imani, lakini pia kumzungumzia maiti ina faida gani hebu niambie ni funzo gani tunalolipata kwa jinsi tunavyomzungumzia maiti? sana nachokiona ni watu kutoa hasira zao tu basi.
 
Sasa tangu lini kibao kikamgeukia maiti? ushawahi kuona maiti anashtakiwa au kuwajibika kwa lolote?

Sasa hivi haya madudu yaliyofanyika kwenye serikali ya awamu ya tano yote anatwishwa Maiti ambaye hawajibiki kwa lolote halafu viongozi walewale waliyokuwepo kwenye hiyo serikali ndio hao hao bado wapo kwenye madaraka na wapo kimya hawatii hata neno kwenye hayo madudu yaliyofanyika kwenye serikali ambayo wao ndio walikuwepo, sasa hivi wanasisitiza kuwa hii ni serikali ya awamu ya sita hivyo hawana cha kuwajibika zigo katwishwa maiti.
Ni kweli maiti hawezi jitetea, lakini hili ni fundisho tunalolipata sisi tuliyo hai, bora mtu usemwe wakati upo hai kuliko usemwe wakati umeshakufa.
Mzee Mwinyi alisema, namnukuu "Maisha ni kama hadithi tu, basi ewe ndugu yangu kuwa hadithi nzuri kwa hao watakaosimuliwa".
Utawala ni kama unywaji wa pombe, ukinywa sana utakulevya na kuanza kufanya mambo yasiyo na ungwana, mlevi habadiliki mwili lakini vitendo vyake hubadilika kutokana na POMBE. Hivyo ndugu yangu watu wakipata madaraka wasiwe kama walevi kwani kuna hadithi itakayosimuliwa dhidi yao.
Na huwezi kuuzungumzia utawala bila ya kumzungumzia mtawala.
 
Binaadamu wote tuna mapungufu yetu sasa sijaelewa ni funzo gani tunalolipata kwa kumzungumzia vibaya marehemu? kinachofanyika ni kumzungumzia vibaya marehemu na kibaya zaidi madudu yote anabebeshwa yeye peke yake ila wale aliyekuwa nao kwenye hiyo serikali yenye madudu wako kimya kama hawahusiki na lolote vile.
 
Ikiwa wewe huoni ni funzo mimi naliona ni funzo, Hitler anazungumzwa kwa vitendo vyake, Iddi Amini anazungumzwa kwa vitendo vyake, Sokoine anazungumzwa kwa vitendo vyake. Ikiwa wewe ni kiongozi juwa ya kuwa unachukua masuuliya ya wale unawaoongoza ukifanya vizuri utasifiwa na ukivuruga utakosolewa. Huenda wewe hujaguswa na foul treatment lakini waulize wale waliyotendewa na kupitia katika utawala uliyopita.
 
Tofautisha kukosolewa na kusemwa vibaya, unamwita mtu shetani halafu ndio unasema kukosoa huko? halafu nimesema mbona hawa aliyokuwa nao kwenye hiyo serikali yenye madudu hawasemwi? Kuanzia Mama samia nae alikuwepo kwenye hiyo serikali yenye madudu hayo mabaya yote yaliyotendwa kwenye utawala wa Magufuli Mama Samia ndio alikuwa makamu katika huo utawala ila hadi sasa kanyamaza kimya kama hakuwepo kwenye hiyo serikali na wala ninyi sioni kuwazungumzia hawa viongozi ambao walikuwepo kwenye huo utawala.

Mimi hata angekuwa amenifanya sijui nini ila ndio ameshakufa hivyo hakuna cha kufanya sana sana ndio hivyo kumuongelea vibaya kwa sababu ya hasira tu ila hakuna cha maana.
 
Watu wengi hawajui. Prof. Asad alifanyiwa unyama mwingi. Kutekwa kutishwa, na marehemu akasema kwamba, 'anajifanya mjanja, ngonja uchaguzi upite, atapotea'. Lakini Asad hakuyumba katika msimamo wake wa kutomlamba nyayo ili apate ulaji.

Katika watu wenye misimamo thabiti, hakika Asad ni mmoja wao. Si wengi ambao wana uwezo wa kuhimili aliyoyapitia. Tangu kuondolewa kwake ameishi maisha ya kawaidia sana, maisha ya chini, ilhali angekubali kulamba tu nyayo za mfalme, angeishi kwa starehe.

Sijui kwa nini, marehemu hakuwa na amani, kila mara alimtafuta kwa simu. Baadaye Asad alimblock. Marehemu Kijazi akawa anatumika kumlainisha lakini Asad hakubadili msimamo wake.

Mungu hamtupi mwenye haki.
Sasa kwanini wengine wasingekuwa kama Assad pengine tusingefika huku, Mama Samia na waziri mkuu kama wasingekubali kulamba nyayo pengine mambo yangebadilika hata Assad mwenyewe alisema hili kwamba hata kama huwezi kumkosoa kiongozi wako wazi wazi mtumie hata message umueleze kuwa jambo fulani umekosea.
 
Tofautisha kukosolewa na kusemwa vibaya, unamwita mtu shetani halafu ndio unasema kukosoa huko? halafu nimesema mbona hawa aliyokuwa nao kwenye hiyo serikali yenye madudu hawasemwi? Kuanzia Mama samia nae alikuwepo kwenye hiyo serikali yenye madudu hayo mabaya yote yaliyotendwa kwenye utawala wa Magufuli Mama Samia ndio alikuwa makamu katika huo utawala ila hadi sasa kanyamaza kimya kama hakuwepo kwenye hiyo serikali na wala ninyi sioni kuwazungumzia hawa viongozi ambao walikuwepo kwenye huo utawala.

Mimi hata angekuwa amenifanya sijui nini ila ndio ameshakufa hivyo hakuna cha kufanya sana sana ndio hivyo kumuongelea vibaya kwa sababu ya hasira tu ila hakuna cha maana.
Hasira ni mbaya, ukiwa na hasira unaweza sema chochote au kufanya chochote, hebu vaa viatu vya mtu ambaye ndugu yake aliokotwa kwenye kiroba kwenye fukwe ya bahari, hebu vaa viatu vya mtu ndugu yake amepigwa risasi, vaa viatu vya mtu baba yake ametekwa na kusulubiwa, vaa viatu vya mtu amechukuliwa pesa zake kwa nguvu n.k. Hivi wewe utakuwa na tafsiri gani ya huyo mtu anaye angalia haya mambo yafanyike tu bila kukemea? Haya yote yamefanyika inaonyesha yamepata baraka kutoka kwa kiongozi mkuu. Waache waathirika waponye majeraha yao kwa kutoa dukuduku zao. Lakini ninaungana na wewe si vizuri kumsema marehemu kwa mabaya yake.
 
Hivyo ni masuala ya kutoa dukuduku hivyo ni mambo binafsi, ni kama leo JK afe halafu Dr Ulimboka atoa dukuduku lake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom