Anayefahamu Tiba hii, Anisaidie.

Madame B

JF-Expert Member
Apr 9, 2012
29,437
30,932
Habari zenu wana Jf,
Nina tatizo la kuwashwa sana ukeni,kuvimba uke na kupata vijipele vidogo vidogo visivyouma, iwapo tu nitajamiiana kwa kutumia Kondomu,
Ila nikijamiiana bila kutumia Kondomu tatizo hilo silipati,hivyo basi
Kama kuna daktari atakaesoma mada hii naomba unisaidie tatizo langu,aidha kwa ushauri au vyovyote vile,
La kama unafahamu namba ya simu ya daktari bingwa wa magonjwa ya uzazi,tafadhali naomba unipatie.
Asante.
MADAMME B.
 
Unaweza kuwa na tatizo linolitwa Simplex herpers! Huwa ni gumu sana kuonekana kwa urahisi! Kama uko Dar nenda Agakhn Hospital ukamwone Dr. Shafiq au pale Regency kuna Doctor wa akina Mama ambaye ni bingwa kwa uchunguzi na Matibabu. Fanya haraka kupata matibabu maana unaweza kupata madhara makubwa kwenye Kizazi!!
 
Asante mdau,ila nilishafanyiwa vipimo pale IMTU,Agha Khan pamoja na Massana Hsptal na kote huko walinipiga Ultra Sound kuangalia aidha kizazi kimeathirika au la, na jibu likaja kwamba niko ok,ila nikapewa cream ya kupaka ukeni kabla ya kujamiiana, wiki 3 za mwanzo sikupata muwasho wala vijipele,ila baada ya kufunga mwezi tatizo lile likarudi upya,sasa ndo nikashindwa kuelewa,
Ni mafuta yaliyopo ktk kondomu yananidhuru au uke wangu una matatizo.
Ila nashukuru kwa msaada wako Aura,nitaufanyia kazi.
 
Kondomu bwana zina mambo kwelikweli hasa hizi za bei rahisi, kapime kama una aleji/mzio au badili aina ya mipira unayotumia mara kwa mara, kusema ukweli mi kondomu sizipendi kabisa kabisa. lakini aina nyingine ya mpira au angalia kama utakuwa na fangasi. ukiweza ni-PM nikuulize maswali mengine zaidi.

Mwanzo | maajabu ya maji
 
Habari zenu wana Jf,
Nina tatizo la kuwashwa sana ukeni,kuvimba uke na kupata vijipele vidogo vidogo visivyouma, iwapo tu nitajamiiana kwa kutumia Kondomu,
Ila nikijamiiana bila kutumia Kondomu tatizo hilo silipati,hivyo basi
Kama kuna daktari atakaesoma mada hii naomba unisaidie tatizo langu,aidha kwa ushauri au vyovyote vile,
La kama unafahamu namba ya simu ya daktari bingwa wa magonjwa ya uzazi,tafadhali naomba unipatie.
Asante.
MADAMME B.

Pole sana madame B. Kuna watu wachache huwa wana-react kwa material ya rubber inayotengenezewa condom za aina nyingi zilizo sokoni. Pengine nawe ni mmoja wao. Jaribu kutafuta condom mbadala kwenye maduka makubwa ya dawa mjini DSM( mfano JD, The Pharmacy etc). Ukiona problem inaendelea, tafuta doctor specialist wa kinamama.
 
Naweza kusema me ni mmoja wapo,lakini kabla ya kwenda hosptal,nilijaribu kubadilisha mipira ili nipate ule ambao hautaniletea madhara,ila sikufanikiwa na mbaya zaidi,nilikuwa nahs muwasho mpaka ndani ya uke ktk mlango wa kizazi,na nilidhani ni mipira ya kiume tu,kwani hata nilipojaribu kutumia mipira ya kike hali ilikuwa vilevile.
Ila nashukuru sana kwa ushauri ndg, MkandaBoy.
 
Acha kutumia kondom. Uwe na mpenzi mmoja mwaminifu mliyepima afya zenu. Panga uzazi kwa kutumia njia nyingine

Mpenzi wangu nahs si mwaminifu hvo cwez acha kutumia mpira,na yeye anafahamu kuwa nafahamu si mwaminifu,na kuhusu kupanga uzazi,bado sijapanga kupata mtoto na vilevile sihitaji kutumia njia yoyote ya kuzuia mimba.
 
Yanin kua na mpenzi sio mwaminifu? Kama umegundua ukifanya luv kwa mpira unapata muwasho acha kuutumia na tafuta mupenzi mwaminifu kusolve hilo ttzo.
 
Kwa dunia ya leo,kumpata mwanaume ambaye ni wa kwako peke yako kwa uaminifu cjui atoke wapi!
Cha umuhimu ni kupata tiba tu.
 
wapo dada

Rose,lakini mpaka umpate,utahangaika sana,sababu mwanaume mwingine akiwa kwako anajitoa kwa kila kitu lakini akiwa nje ya nyumba tu,lazima atende uovu,
Na wanaume zetu hawa wa kuingia night-shift,sidhani.
Atakusaliti tu hata kwa asilimia ndogo.
 
kuwa mwaminifu pai uwe na mpenzi moja.nenda kapime tena.kuepuka tatizo kuwa mwaminifu

Kaka'angu, kuhusu suala la kuwa mwaminifu nadhani mimi naongoza,sababu nakumbuka tangu niingie ktk uhusiano namaliza mwaka,sijawahi kumsaliti mpenzi wangu na sifikirii kama itafika siku nikamsaliti,either kwa kutoka nje au vyovyote vile,japo naletewa vielelezo vya mtu wangu kunisaliti, na ndo huyohuyo tu.
Na nikisema nisitumie mpira,huoni kama nahatarisha afya na maisha yangu pia?
Cha umuhimu kama ulivyonena,nikafanyiwe uchunguzi wa kina.
Asante Erick
 
Nawashukuru wana Jf kwa Mawazo yenu,Maoni yenu na Msaada wenu kwangu ktk tatizo hili linalonisumbua,
Aminini nitayafanyia kazi,na sitayaweka kapuni.
Asanteni,
MADAME B.
 
Utakua unapata reaction kutokana na rubber ktk condom au ile lubricant ktk condom..na kama zamani ulikua hupati tatizo hili basi inawezekana una infection inayoongezea hiyo hypersensitivity/ allergic reaction
 
Mpenzi wangu nahs si mwaminifu hvo cwez acha kutumia mpira,na yeye anafahamu kuwa nafahamu si mwaminifu,na kuhusu kupanga uzazi,bado sijapanga kupata mtoto na vilevile sihitaji kutumia njia yoyote ya kuzuia mimba.
Madame B pole sana kwa tatizo ulilonalo. sasa nafiiri wewe una allergy na hydrocarbons hizi ni ina ya rubber materials ambazo ziko katika condoms aina zote. ushauri wangu kwako ni acha kabisa kuzivaa kwani zitakufanya uppate herpes na baadae utaoza kizazi. ishu hapa ni kwamba yawezekana tatizo lako likawa kwenye acute stage sasa usitake liwe chronic.

kwakua huyo mpenzi wako siyo mwaminifu basi mweleze kuwa hauko tayari kushirikiana naye tena kwasababu ya hii shida, kama hatabadili tabia na kwakua pia n ngumu kwa wewe kuhakikisha kama amebadili tabia basi. hebu kaa pembeni jitibie kisha tafuta mpenzi mwingine.
 
Madam utaumia, kipi bora kuendelea kujamiana au kuacha mpaka pale utakapopata aliye sahihi, jiangalie usije ukaanguka, na si mara zote ukianguka unaweza kusimama, unaweza kuanguka na usisimame.
 
Madame B pole sana kwa tatizo ulilonalo. sasa nafiiri wewe una allergy na hydrocarbons hizi ni ina ya rubber materials ambazo ziko katika condoms aina zote. ushauri wangu kwako ni acha kabisa kuzivaa kwani zitakufanya uppate herpes na baadae utaoza kizazi. ishu hapa ni kwamba yawezekana tatizo lako likawa kwenye acute stage sasa usitake liwe chronic.

kwakua huyo mpenzi wako siyo mwaminifu basi mweleze kuwa hauko tayari kushirikiana naye tena kwasababu ya hii shida, kama hatabadili tabia na kwakua pia n ngumu kwa wewe kuhakikisha kama amebadili tabia basi. hebu kaa pembeni jitibie kisha tafuta mpenzi mwingine.

Ushauri wako mkuu naukubali ila sasa tatizo linakuja kuwa mimi pamoja na huyo mpenzi wangu tumeshatambulishana kwa wazazi wa pande zote,na nikichukua uamuzi huo wa kuachana nae,itakuwa si jambo zuri.
Pia kujamiiana bila mpira naogopa sana,yani ndo mana natafuta tiba.
Kumbuka kuwa tatizo hlo analijua na amenipeleka hospital! So anaufanya uzinzi huku akitambua afanyacho.
Asante mkuu kwa ushauri.
 
pole sana kwa hilo tatizo. Unahitaji ujijue vizuri na uzingatia kuwa maisha yako ni muhimu kuliko kutambulishana kwa wazazi. Kama jamaa yako siyo mwaminifu na ndiyo maana mnatumia kondom, je mkioana mtatumia condom milele! Plz think big Lady!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom