Hali hii inauma sana pindi unapokutana mayo, cos ulikuwa umeshaweka mipanho Yote sawaHello wanajamvi
Mimi ni kijana wa miaka 30, ninaishi mkoa x kikazi.. nimekuwa na mahusiano na mwanamke kwa muda wa miaka 5 tumekuwa tukiishi pamoja, mwaka jana nilikwenda kwao na kutoa mahali
Mwezi uliopita niliomba likizo moja ya vitu tulivyotarajia kuvifanya kipindi hicho cha likizo ni pamoja na kurudi nyumbani mkoa Y kwa ajili ya kusalimia wazazi na kuweka mipango ya ndoa.
Baada ya kulifikisha swala hili kwa mpenzi wangu yeye aliniomba kuwa aende mara moja kwao mkoa Z kumsalimia bibi yake then baada kama ya siku kama 3 atarudi kuungana na mimi..
Nilimpa ushirikiano wote katika safari yake hiyo pamoja na kufanya shopping, na kumlipia nauli, na kuwa na mipango mingi ya kufanya baada ya yeye kurudi na kuungana na mimi...
Cha kushangaza baada tu ya kufika kwao tu nikaanza kunotice hata pattern ya mawasiliano yamebadilika, hanijulii hali, nikimpigia simu anadai yupo busy. Nikimuuliza atarudi lini hanipi majibu ya uhakika.
Baada ya siku kama nne akanipigia simu kuwa anataka kurudi ila atapitia mkoa T kwa rafiki yake ninayemfahamu before kuja kuungana na mimi na kuniomba nimtumie nauli nikafanya hivyo...
Siku ninayotarajia kuwa atakuwa safarini anakuja kuungana na mimi akanitumia sms kuwa anaumwa sana, baadaye akaniambia kuwa amekosa magari ya kuja huku nilipo, ukimpigia simu hapokei lakini wakati wa jioni nikampata kwenye simu katika kumuuliza kuwa anaendeleaje ana mpango gani na hiyo safari akaniambia kuwa kuna ujumbe amenitumia kwenye simu.. kucheki ule ujumbe alikuwa ameandika kuwa anaona ni wakati umefika wa kumaliza mahusiano yetu...
Hivi sasa hapa nyumbani walikuwa wanamsubiria kwa ajili ya kudiscuss naye kuhusu swala la ndoa na tayari nimekwishalipa mahari kwao...
Hapa nipo kwenye dilema sijui la kufanya nimezungumza na mama yake na yeye anashangaa anajaribu kuwasiliana naye ila hapokei simu zake.
Huyu mpenzi wangu sijawahi kuwa na ugomvi wowote mkubwa tumekuwa tukiishi vizuri tu...
Kikubwa hapo heshimu mawazo yake maana kashaamua..Na hapo kashaweka DOA, kwenye hayo mahusiano maana ndio ulikuwa kwenye finalisation stage YA kuwa mwili mmoja
Kwakuwa kashaamua Na wakati Jambo analijua lililopo mbele ni harusi..nakushauri move on..japo inauma saana tena sana Ila ndio mdada huyo kashaamua kutoka kwenye maisha yako
Nenda ukae Na familia yako waeleze kila kitu,Kisha funga mkanda Anza upya maisha yako pasipo yeye kuwepo kwenye maisha yako Na funga Vioo tinted dhidi yake
Hivi inawezekana mahari kurudishwa..au kiendacho Kwa mganga hakirudi, Kaa na familia Yao wabane warudishe hiyo mahari..over