Ananipenda, ninampenda...ila kuna mambo tunatofautiana....ushauri tafadhali.

Mimi ni Kijana mwenye umri wa miaka 24 na nipo Chuoni nikisomea ngazi ya stashahada(Diploma) na nipo mwaka wa tatu(mwisho).Katika maisha yangu nilipanga kuwa nitaoa nikiwa na miaka kama 35 hivi na hii inamaanisha kuwa nitakuwa nimepata fursa pia ya kujiendeleza kimasomo katika ngazi ya shahada(Degree) na pengine masters.Ila nimebahatika kukutana na msichana ambaye tumetokea kupendana na kwa sasa yeye yupo mwaka wa pili chuoni katika ngazi ya shahada(Degree) na umri wake ni miaka 23. Katika kushauriana juu ya maisha yetu nimegundua kuwa yeye anataka tufunge ndoa miaka mitatu kuanzia sasa, yaani mimi nikiwa na miaka 27 huku yeye akiwa na miaka 26.Pia akasema kama hilo halitawezekana basi angalau kwa muda huo awe amepata mtoto na ndoa itafuata baadaye kama nilivyopanga. Anasema anaamini atakuwa tayari kumtunza mtoto na wala hataleta pressure kwangu wakati ninaendelea na masomo yangu. Hilo nimelipinga kwa nguvu zote kwa kuwa mimi ninaamini sana juu ya dini na imani yangu hainiruhusu kuwa na mtoto nje ya ndoa kwani atakuwa mtoto aliyepatikana baada ya TENDO LA USINZI na sio TENDO LA NDOA. Pia binafsi kinachonifanya nifikirie kuoa muda amabao nilioupanga ni kuwa nadhani nitakuwa tayari vya kutosha kulea wanangu nikishirikiana na mama yao kwa ukaribu zaidi. Nimewaza sana juu ya hili, je niendelee kuwa naye, au ndio penzi letu lifikie mwisho kwani falsafa zetu zinatofautiana? Naombeni ushauri wenu wadau, kwani ninampenda sana na ninaamini ananipenda sana na vigezo vyote anavyo isipokuwa kutofautiana kwa falsafa zetu na mitazamo yetu juu ya MAISHA.
Ninashukuru sana kwa wale ambao wamenipa ushauri hapa, kwa wale walioponda vilevile nashukuru kwa sababu ndani yake nimeona point za msingi tuu. ASANTENI SANA, na nitaufanyia kazi ushauri wenu pia nikiongezea na kile ninachofikiri huku nikiamini kuwa mawazo yenu yatanisaidia sana.
 
Back
Top Bottom