Anaezijua ofisi za precision air kwa Dar zilipo, msaada tafadhari

Zero7

Member
May 27, 2012
36
1
Kuna mzigo nataka niutume kwenda Mwanza,sasa ofisi za precision sizijui zilipo naomba anaejua anisaidie tafadhari.

UPDATE:
Ahsante nyote mliochangia hapa na kunielekeza vizuri....kwan nimeweza kufika vizuri kabsa bila was was na hofu ya kupotea
 
Naenda Samora Avenue, jengo la shirika bima. Ni karibu na habari maelezo. Ukifika hapo kuna wauza magazeti waulize. Ni jengo la bima makao mkuu opposite na NMB bank house.
 
Kuna mzigo nataka niutume kwenda Mwanza,,,sasa ofisi za precision sizijui zilipo naomba anaejua anisaidie tafadhari……

Unajua kingereza,wasi wasi wangu usije sweka lock up kwa kosa la kujaribu kusafirisha mzigo kwa kutumia kiswahili-heri tafuta mkalimani akusindikize
 
Acha kupoteza muda nana kakwambia pw ni curior,hawasafirisha mizigo nenda kidongo chekundu au dhl,
 
Kuna mzigo nataka niutume kwenda Mwanza,,,sasa ofisi za precision sizijui zilipo naomba anaejua anisaidie tafadhari……

Wapo kwenye jengo la Quality Plaza, Nyerere road.Kama unatokea K'koo ama Posta mpya panda magari ya Gongo la Mboto then shuka kituo kinaitwa Ngozi.Ni kituo kinachofuata baada ya mataa ya Chang'ombe.Kama sehemu uliyopo kuna magari ya Tandika ama Temeke wewe panda hayo hayo shukia kituo cha veta then tembea kwa mguu kama unayafuata mataa ya Chang'ombe pinda kushoto nyosha mbele na barabara ya lami mkabala na Nyerere road then kwa mbele utaona jengo la Quality Plaza ndo uingie humo.Kumbuka ni Quality Plaza na SIO Quality Center maana wabongo wengi wanachanganya majengo haya mawili
 
Wewe mwanaJF unaetaka kutuma mzigo uko pande ipi ili wakuelekeze ofisi ya kupeleka mzigo wako, si agent wote wanaopekea mizigo na kuituma kwa wakati ni bora uende makao makuu.
 
Wapo kwenye jengo la Quality Plaza, Nyerere road.Kama unatokea K'koo ama Posta mpya panda magari ya Gongo la Mboto then shuka kituo kinaitwa Ngozi.Ni kituo kinachofuata baada ya mataa ya Chang'ombe.Kama sehemu uliyopo kuna magari ya Tandika ama Temeke wewe panda hayo hayo shukia kituo cha veta then tembea kwa mguu kama unayafuata mataa ya Chang'ombe pinda kushoto nyosha mbele na barabara ya lami mkabala na Nyerere road then kwa mbele utaona jengo la Quality Plaza ndo uingie humo.Kumbuka ni Quality Plaza na SIO Quality Center maana wabongo wengi wanachanganya majengo haya mawili

Mliman city

Hawa wote wanakudanganya...
 
Naenda Samora Avenue, jengo la shirika bima. Ni karibu na habari maelezo. Ukifika hapo kuna wauza magazeti waulize. Ni jengo la bima makao mkuu opposite na NMB bank house.

Posta karibu na Nmb kama unaelekea life house bima upande wa kulia kama sijakosea utaiona ofisi ya precision

Hawa wapo sahihi na kwa maelezo ya ziada ni kwamba ofisi za Precision zipo ndani ya jengo la Shirika la Bima (NIC House) kwenye ghorofa ya chini (ground floor).

NIC House inapatikana kwenye makutano ya barabara ya Pamba na Samora, na ofisi hizi za Precision zipo upande wa barabara ya Pamba na zinatazamana na kituo cha mafuta kama sikosei ni Gapco wale au Oryx.
 
Nakushauri uende quality Plaza au pale posta maana kwingine ni agents wakutoa cha juu
 
Back
Top Bottom