Anachofanya Rais Samia huko Zanzibar ndicho alichokifanya Hayati Magufuli kule Chato

Swali la kujiuliza haya yote smz inaiwezo wa kuyatekeleza??kwa bajeti yake??
Hapana haiwezi hiyo miradi mengine ni mikopo mfano ujenzi wa barabara za kilomita 800 unguja na pemba pamoja na uwanja wa ndege wa kimataifa pemba ni mkopo wa masharti nafuu wa serikali ya uingereza 400£
 
Ulinzi na usalama ZANZIBAR wanalipia nnini SAMIA na Mbarawa nani anamlipa? NA wabunge 50 wanakuja Dodoma nani anawalipa? Ni Tanganyika
Mji wa Zanzibar town Wabunge na Wawakilishi 20 kwa ukubwa sawa Kigamboni tu. Mara mbunge wa Amani, Kwerekwe, Mpendae, Kikwajuni, Mtoni nk hiyo ni mitaa tu kula ntaa na Mbunge wake.
Ndio ujue mnavyonzwa Twanganyika🤣
 
Marehemu Magufuri enzi za uongozi wake alinuia kuibadilisha Chato kuwa kama Nyuyoku na wengi tumeona miradi mingi ambayo ilifanyika maeneo hayo ikiwemo ujenzi wa uwanja wa ndege, barabara za lami zenye ubora wa hali ya juu kabisa, hospital kubwa ya kanda nk, bahati nzuri au mbaya kifo kikamchukua na sasa imebaki historia.

Kwa upande wa Zanzibar kipindi hiki Kuna miradi mingi sana inaendelea tena kwa mkupuo mfano ujenzi wa barabara kuu mpaka zile za vichochoroni kwa lami, ujenz mkubwa wa bandari ya Malindi, Mwanga Pwani, ukarabati wa uwanja wa amani ( 50bil), ujenzi wa flyovers maeneo ya amani na Mwana kwerekwe, ujenzi wa soko kuu la mwanakwerekwe na mombasa , ujenzi wa hospital za rufaa Kila wilaya na mkoa,upanuzi wa uwanja wa ndege wa Amani Abeid Karume, kiufupi Kuna miradi mingi inafanyika kwa wakati huu ndani ya Zanzibar kuliko wakat wowote ule toka mapinduzi, na hayo yote yanafanyika Samia akiwa Rais wa Tanzania na Mwinyi kule Zanzibar na sote tunajua vizur uwezo wa kukusanya mapato wa SMZ kwa mwaka.

Cha kujiuluza pesa zote hizi za kufanyia miradi yote hii tena kwa pamoja Zanzibar wanazitoa wapi na hapo kumbuka wote hao ndio kwanzaaa wana miaka mi3 madarakani jiulize baada ya miaka 10 ni kiasi Gani Cha pesa kitakuwa kimetumika kuijenga Zanzibar na je hizo pesa zitakuwa zinachotwa kutokea wapi?
Wacha kupotosha watu. Juzi raisi Mwinyi amechukua commercial loan ya NMB na CRDB ya 450bil Tsh kwa ajilinya ku finance miradi hiyo. Na zinajengwa 200km tu. Sasa mama Samoa amehusikaje hapo?
 
Kuhusu deni la tanesco musahau hata Raisi wa Zanzibar awe nani hilo deni halipi wanasema hawawezi kumlipa wanae mdai mdaiwa halipwi
Mengine hili. Tanesco ilikuwa ikiuzia umeme huku ikiitoza VAT tunajua yankuwa VAT analupa mtumiaji wawisho. Lakini tenesco haijasamehe Deni bali lile semi la VAT ambalo ZEKO imegoma kulipa. Elimu ji muhimu sana
 
wavunje wakai wananufaika? wanatuibia na kujenga kwao
Lissu amesema Samia ni mwizi kuna watu wameoji anaiba wapi na anafanya nini kuthibitisha kwamba anaiba,kwa Comment hii nna uhakika kila mtu kashajua kwamba Tunaye raisi Mwizi anaiba Tanganyika anajenga kwao...wakati huo wanataka kujitenga na sisi.
 
Back
Top Bottom