Ana mimba yangu, cha ajabu anataka tuachane

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,449
Wadau habari zenu?

Nina msichana ambaye kwa bahati mbaya siku ya kwanza tu tumeonana nakumbuka alilala kwangu tulifanya mapenzi bila condom . Sasa huyo binti anadai ana mimba yangu ambayo sasa ni miezi minne.

Kilichonistaajabisha ni kwamba ananiambia tuachane na hataki habari za mapenzi na mimi na hadi kliniki kaenda peke yake. Sina amani najiuliza ni kweli mimba ni yangu?
 
Nakushauri utunze mawasiliano yenu (texts, emails) kwa ajili ya huko mbeleni akija badilisha mawazo. Vile vile kwa ajili ya kuja kuhakiki kama mtoto ni wako. (Kimahakama ).
Pia anaweza kuwa yeye mwenyewe hana uhakika ni ya nani (alikuwa na mwanamme mwingine).
Ukichanganya na mabadiliko ya mwili akawa hana maamuzi ya kuaminika.
Usimweke mbali sana kimawasiliano japo amesema hataki mawasiliano.
 
Yaani hii inajidhihirisha wewe ni mtu wa aina gani, fikiria mpaka mdada mwenye ujauzito wako ameamua ni kheri akae mbali na wewe. Mkuu hembu jichukunguze kidogo:D:D:D
 
Keshamkumbuka baba wa mtoto wake, ingekuwa ni wewe asingekuwa harsh kiasi hicho!
 
Kwani mlifanya matusi gizani au? km jibu ndiyo,basi itakuwa ulipizi upepo nae alisikia kabisa ila aliamua kukupa bichwa ujione kidume.
 
Ukiona hivyo ujue wewe sio mwenye mimba, mwenye nayo ndio anaenda naye clinic
 
Mimba ni yako asilimia 100, sema kichaa cha mimba yake hakilandani na wewe, kama ingekuwa siyo yako angekunyofoa matumizi, harafu kadi ndio ingekuwa na jina tofauti na lako, chamsingi ishi nae kwa busara na usipanick maana ni kipindi cha mpito.. Hakuna aliye sahihi.. Ila majibu ndio uthibitisha usahihi.
 
Kwani mtu kua na mimba yako lazima mgandane hakutaki endelea na yako mwache alee mimba kwa amani pengine unampa stress tu ndo mana kaona hajitenge nawewe
 
Wadau habari zenu?

Nina msichana ambaye kwa bahati mbaya siku ya kwanza tu tumeonana nakumbuka alilala kwangu tulifanya mapenzi bila condom . Sasa huyo binti anadai ana mimba yangu ambayo sasa ni miezi minne.

Kilichonistaajabisha ni kwamba ananiambia tuachane na hataki habari za mapenzi na mimi na hadi kliniki kaenda peke yake. Sina amani najiuliza ni kweli mimba ni yangu?
Sio yako iyo mimba!
 
Back
Top Bottom