Amekasirika. Kisa...nimemuuliza "wataondoka lini"

mitishamba

JF-Expert Member
Dec 21, 2011
697
111
Baada ya majonzi ya takriban wiki nzima ya mpendwa wetu RM, ndugu yenu mitishamba nimerudi tena.
Huwa siishiwa mikasa, na mara nyingi huwa naongelea mambo yaliyonikuta ama kuyashuhudia.

Mimi na mke wangu tumekuwa tukiishi maisha ya kawaida ya ndoa (furaha, huzuni, mikasa na kutoelewana wakati mwingine).
Nyumbani kwetu huwa tunapokea wageni mbalimbali kwa nyakati tofauti. Kuna wakati wanakuja ndugu/marafiki zake na kuna wakati wanakuja ndugu/marafiki zangu.

Mara nyingi wakija ndugu zake huwa simuulizi kuwa lini wataondoka kwani najua kwa kufanya hivyo huenda ikafikirika vibaya na sikupenda iwe hivyo. Tatizo linakuja kwamba nduguze wanapokuja huwa hawatoi taarifa siku ya kuondoka hadi inapokaribia siku chache sana kabla ya kuondoka ndo wanatoa taarifa. Hii mara nyingi huniletea matatizo makubwa kwani kama ujuavyo masuala ya kiuchumi...wakati mwingine hunipasa kukopa ili niwapatie nauli kwani huwa ni short notice.

Hivi karibuni alikuja mama yake na mdogo wake. Baada ya kukaa kwa muda fulani ilibidi nimuulize "wataondoka lini"? Nia ilikuwa ni kunipa muda wa mimi kujiandaa kwani kwa wakati huo nilikuwa pia na majukumu ya kulipia ada ya shule takriban watu wanne, hivyo ni vema nikajiandaa mapema.

Nilijuta kuuliza hilo swali....
Akakasirika, akavimba, misonyo kibao, haongei......yaani kisirani mtindo mmoja.
Hadi najuta kwa nini niliuliza swali hilo.
Hadi sasa no mawasiliano.
 
Mke wako sio muelewa.

Sasa hapo tatizo liko wapi? Hata angehangaika kukuuliza kwanini unauliza basi ili aelewe. Mwache aendelee kununa kama anataka, alafu siku mama yake mdogo akiaga unamwita mkeo pembeni unamwambia huna namna ya kumpatia nauli kwasababu umetumia pesa yote na mkopo umekosa. Akianza kulalamika mwambie kwamba asingekuona mjinga kwa kumuuliza swali la msingi ungetenga hiyo nauli. . . akishakuelewa ndio utoe hiyo nauli. Na next time atakwambia mwenyewe bila kumuuliza.
 
Nashukuru sana Lizzy kwa mawazo yako.
Sababu ya kumwuuliza nimemwambia, kuwa nimemuuliza kwa nia nzuri tu (na kiukweli nilikuwa na nia nzuri tu) lakini bado hataki kuelewa. Tena anasema kuwa (kwa mimi kuuliza hivyo) ni kuwa siwapendi ndugu zake...eti ataawaambia wasije tena. Na mimi sitaki kumuudhi basi nimebaki nimejinyamazia tu. Hata salamu hapokei, haki pia sipati....
 
haya mambo yanaboa,sasa kanuna ya nini?mtu inapaswa aelewe hela haiokotwi na hata kama unayo basi imeshafanyiwa mipango.kuna jamaa aliniambia yeye anawatoza kodi ndugu zake na wale wa wife kwa kisingizio cha gharama kubwa za maisha.hawakai zaidi ya siku mbili kwake
 
Basi fanya hivyo nlivyokwambia akitaka nauli ili mama aende nyumbani. Pole kwa masahibu.
 
haya mambo yanaboa,sasa kanuna ya nini?mtu inapaswa aelewe hela haiokotwi na hata kama unayo basi imeshafanyiwa mipango.kuna jamaa aliniambia yeye anawatoza kodi ndugu zake na wale wa wife kwa kisingizio cha gharama kubwa za maisha.hawakai zaidi ya siku mbili kwake

Mkuu ukifanya hivyo, upande wa pili watakuchukia.
 
Mkuu haya mambo ya familia ni magumu sana na yapaswa uende nayo kwa akili sana
na haswa linapokuja swala la ndugu wa mke
Ni balaa sana na usipokuwa makini utajikuta kila wakati unaingia kwenye mgogoro na wife wako
Pia litaleta matatizo hata kwa ndugu zako wewe watakapokuja kwako
Kwa kuwa amenuna na hataki kuongea we ngoja hasira zake zipungue au hao ndugu zake wakiondoka ndipo umkalishe chini umueleze sababu ya wewe kumuuliza kitu kama hicho na kama ni mtu mwelewa ataelewa kosa lake
Ila kama ndio kaamua kuvaa uso wa mbuzi ni pagumu sana
 
jibu ni rahisi mkuu.siku wakiaga waambie wataondokaa mwisho wa mwezi na watakua wameelewa kua mfuko hauko sawa.hata kama itakua ndio tarehe 3!then salary ikitoka unawasafirisha.mimi siafiki kukopa ili kutoa nauli kwa mtu aliyekuja kutembea kwa raha zake hata kama ni ndugu yako wewe.
 
Pole mkuu,
Sijui mambo ya ndoa lkn,mbona hilo linaeleweka tu,
Ongea naye vizuri labda kuna lingine na hiyo ni sababu tu!
 
w.ke wengine jamani,si angalau umempa sababu za kuuliza.yeye mwenyewe kwani maisha hayajui?aache kununa nuna ovyo.iliyobaki wewe mpe muda,baadae atakuwa ok.au hiyo ni tabia yake ya kununa nuna.mwambie awe muelewa.pia ashukuru nauli unatoa wewe.
 
usipanic,we tulia ila siku wakiaga waambie wasubiri utafute nauli,ndo uwaweke had wakome ili kusud mkeo akil imsogee.yeye haon km hali ni ngumu kwa sasa.
 
huko ni kumuendekeza mke wako

unapaswa kabisa kumuuliza wataondoka lini
hata kama wamekuja na nauli yao kabisa....

wewe ndo baba mwenye nyumba lazima ujue wageni wako wataondoka lini

tena hilo swali ungeuliza siku ya kwanza kabisa....

tena ungewauliza wenyewe...bila kuogopa.......

ni vizuri kuuliza wataondoka lini?
wamekuja kusalimia tu au wana shida nyingine?
wagonjwa?
au kuna pesa wanataka kutoka kwako?
au wana safari nyingine hapo ni transit?.......
 
Akiendelea kuzingua namna hiyo tafuta nyumba ndogo uwe unaenda kutoa stress huko..maisha ya siku hizi haya yalivyo na ndoa tete halafu unapata wageni kila mara duh ! aisee hata raha ya ndoa hautaiona maana kila wakati nyumbani tension na hujui wanaingia lini, bro una kazi sana POLE!!
 
Huu ushauri wako mkuu ni balaa
Yaani aachane na stress za home akatafute tena nyingine mtaani huko
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom