mitishamba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2011
- 697
- 111
- Thread starter
- #61
Nipo nafatilia ushauri.
mke wako sio muelewa.
Sasa hapo tatizo liko wapi? Hata angehangaika kukuuliza kwanini unauliza basi ili aelewe. Mwache aendelee kununa kama anataka, alafu siku mama yake mdogo akiaga unamwita mkeo pembeni unamwambia huna namna ya kumpatia nauli kwasababu umetumia pesa yote na mkopo umekosa. Akianza kulalamika mwambie kwamba asingekuona mjinga kwa kumuuliza swali la msingi ungetenga hiyo nauli. . . Akishakuelewa ndio utoe hiyo nauli. Na next time atakwambia mwenyewe bila kumuuliza.
ha haaaaaaaaaaaaaa, watatuambia tumekuwa wazungu. kibongobongo mgeni anakuja atakavyo, na anaondoka atakapo, tena kwa nauli yako na hela ya kulipa mkopo wa nauli aliyokupa kujia kwako, kama ulimuita vilehuko ni kumuendekeza mke wako
unapaswa kabisa kumuuliza wataondoka lini
hata kama wamekuja na nauli yao kabisa....
wewe ndo baba mwenye nyumba lazima ujue wageni wako wataondoka lini
tena hilo swali ungeuliza siku ya kwanza kabisa....
tena ungewauliza wenyewe...bila kuogopa.......
ni vizuri kuuliza wataondoka lini?
wamekuja kusalimia tu au wana shida nyingine?
wagonjwa?
au kuna pesa wanataka kutoka kwako?
au wana safari nyingine hapo ni transit?.......
ha haaaaaaaaaaaaaa, watatuambia tumekuwa wazungu. kibongobongo mgeni anakuja atakavyo, na anaondoka atakapo, tena kwa nauli yako na hela ya kulipa mkopo wa nauli aliyokupa kujia kwako, kama ulimuita vile
Nashukuru sana Lizzy kwa mawazo yako.
Sababu ya kumwuuliza nimemwambia, kuwa nimemuuliza kwa nia nzuri tu (na kiukweli nilikuwa na nia nzuri tu) lakini bado hataki kuelewa. Tena anasema kuwa (kwa mimi kuuliza hivyo) ni kuwa siwapendi ndugu zake...eti ataawaambia wasije tena. Na mimi sitaki kumuudhi basi nimebaki nimejinyamazia tu. Hata salamu hapokei, haki pia sipati....
Pole yako....amepata sababu ya kujipa likizo...:lol:!
May be unaweza kurudia tena maneno yako kuwa, uliuliza kwa nia njema tu. Na pia labda anataka ubembeleze....si unajua wanawake wengine wanapenda kudeka.....:lol:
Au nichepuke kidogo?
Una maana uondoke??!! hapana...hiyo ndo itaonyesha umewakimbia ndugu zake. Kama amenuna kwa siku 2, zinatosha sasa, ukimsemesha tu,..atakujibu! unaanza na ka-utani hivi...
Namanisha smolu farm...
Hayo ni maamuzi yako mwenyewe! Mimi sikushauri hilo...........tatzo dogo hivyo umeshaanza kuwaza hayo!...mhhhh!! Usitafute kisingizio na wewe!
Wee naye huna dogo!
mkeo ana elimu gani?au bado ni mdogo sana?hana mipango kabisa ya familia
Baada ya majonzi ya takriban wiki nzima ya mpendwa wetu RM, ndugu yenu mitishamba nimerudi tena.
Huwa siishiwa mikasa, na mara nyingi huwa naongelea mambo yaliyonikuta ama kuyashuhudia.
Mimi na mke wangu tumekuwa tukiishi maisha ya kawaida ya ndoa (furaha, huzuni, mikasa na kutoelewana wakati mwingine).
Nyumbani kwetu huwa tunapokea wageni mbalimbali kwa nyakati tofauti. Kuna wakati wanakuja ndugu/marafiki zake na kuna wakati wanakuja ndugu/marafiki zangu.
Mara nyingi wakija ndugu zake huwa simuulizi kuwa lini wataondoka kwani najua kwa kufanya hivyo huenda ikafikirika vibaya na sikupenda iwe hivyo. Tatizo linakuja kwamba nduguze wanapokuja huwa hawatoi taarifa siku ya kuondoka hadi inapokaribia siku chache sana kabla ya kuondoka ndo wanatoa taarifa. Hii mara nyingi huniletea matatizo makubwa kwani kama ujuavyo masuala ya kiuchumi...wakati mwingine hunipasa kukopa ili niwapatie nauli kwani huwa ni short notice.
Hivi karibuni alikuja mama yake na mdogo wake. Baada ya kukaa kwa muda fulani ilibidi nimuulize "wataondoka lini"? Nia ilikuwa ni kunipa muda wa mimi kujiandaa kwani kwa wakati huo nilikuwa pia na majukumu ya kulipia ada ya shule takriban watu wanne, hivyo ni vema nikajiandaa mapema.
Nilijuta kuuliza hilo swali....
Akakasirika, akavimba, misonyo kibao, haongei......yaani kisirani mtindo mmoja.
Hadi najuta kwa nini niliuliza swali hilo.
Hadi sasa no mawasiliano.
Kwa namna flani atakuwa amefikiri umewachoka ndugu zake, ilopo mweke wazi nia yako ya kumuuliza hivyo na baada ya hapo umpe shua kabisa kuwa unapo mkera suluhisho siyo kusonya ama kununa na kukata mawasiliano bali kukueleza ulichomkera nacho ni vyema ili uwe na fursa ya kujirekebisha usijerudia tena kama ni kosa kweli