Amana Benki ya Kiislamu yaanzishwa Tanzania

Boko haram

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
3,253
1,229
Benki ya Kiislamu yazinduliwa Send to a friend
Thursday, 24 November 2011 19:30
0digg

Geofrey Nyang'oro
WAFANYABIASHARA wanaofuata misingi ya dini ya Kiislamu wameanzisha benki mpya ya Kiislamu (Amana Benki L.T.D) itakayoendeshwa kwa kufuata sheria na taratibu za dini hiyo nchini.

Benki hiyo imezinduliwa jijini Dar es Salaam jana baada ya kupata leseni ya muda kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT)Februari 4 mwaka huu na kusajiriwa ikiwa na mtaji wa Sh100 bilioni ulioidhinishwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Amana Benki, Haroon Pirmohamed aliwaambia waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi kuwa benki hiyo itawawezesha wafanyabiashara na makundi mbalimbali ya dini hiyo kufanya shughuli zao za kifedha bila kuathiri misingi ya imani yao.

"Hili ni jambo la imani, hivyo huduma hii itawasaidia wafanyabiashara na watu wa makundi mbalimbali kuendesha biashara zao za kibenki bila kuathiri imani yao,"alisema Pirmohamed.

Alifafanua kuwa pamoja na huduma zitakazotolewa na benki hiyo kufuata misingi ya dini ya Kiislamu, zitawahusu pia watu wa makundi yote wakiwamo wa dini nyingine wanaoamini katika mfumo wa kibenki unaofuata sharia.

Alitaja moja ya misingi iliyomo katika mfumo wa sharia za Kiisilamu kuwa ni kuendesha benki isiyotoza riba.

Parimohamed alizitaja huduma zitakazotolewa na Benki hiyo kuwa ni akaunti za akiba, akaunti ya watoto, wanawake, Hijja, hundi, biashara na akiba kwa ajili ya akiba pia na nyumba za ibada zilizosajiliwa.



Hatimae waislam wameanzisha benki yao iliyo chini ya sharia za kiislaam huu ni ukombozi mkubwa kwa waislaam hapa Tanzania benki yenyewe inaitwa AMANA BANK kwa mtaji wa bl 100 nawakilisha
 
Hatimae waislam wameanzisha benki yao iliyo chini ya sharia za kiislaam huu ni ukombozi mkubwa kwa waislaam hapa Tanzania benki yenyewe inaitwa AMANA BANK kwa mtaji wa bl 100 nawakilisha

Kwa hiyo Waislamu walikuwa chini ya "utumwa" hadi baadaye wakakombolewa?
 
alhamdulillah afadhal tutakua na benki isiyo kua na unyonyaji hamna riba.wote mnakaribisha nibenki inayofuata sheria za kiislam ila hata mkristo unaweza kufungua account
 
Ikitokea makafiri wamefungua akaunti kwa wingi kuliko waisilamu, hapo ukombozi unakuwa uko kivipi?
 
tahadhari!
kama hii bank yetu tutaiendesha kama tulivyofanya kwa taasisi nyingine mfano ile shule ya al haramain.................
tutakua tumejiua!
Tujaribu kuwa makini kwa hilo
 
Dah, na kweli kina James wakijazana huko kwa Amana Bank sijui itakuwaje!!!
 
mimi nauza kiti fire,je nitaweza kuweka hela zangu huko ?
 
Hatimae waislam wameanzisha benki yao iliyo chini ya sharia za kiislaam huu ni ukombozi mkubwa kwa waislaam hapa Tanzania benki yenyewe inaitwa AMANA BANK kwa mtaji wa bl 100 nawakilisha

Nice move!!
May almighty GOD keep it rolling..
 
Hivi makafiri ni akina nani?

Kutoka kwenye Urban Dictionary neno kafiri (kaffir) lina maneno yafuatayo;

1-The Afrikanns (South African) hili neno lina maana ya nigger
Mfano:
-Zulu: Yo, howzit my kaffir
-Xhosa: It's good, kaffir, it's good
-Venda: YO my kaffir heffers
-Boer: You, my kaffir brus, howzit?

2-Also spelled 'kafir', kaffir is a highly Arabic term used to refer to non-Muslims, though it is usually directed less against "People of the Book" (Christians and Jews) and more against others (Hindus, Buddhists, Shintoists, etc)

Kwahiyo:
Huenda mchangiaji alimaanisha "Marafiki" au Wasio waislamu
 
Yeah hili ni jambo ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa muda; nafahamu Dr. Idris na Dr. Dau wameshiriki vilivyo katika kufanikisha ujio wa benki hii kitu. Nadhani Dr. Idris ana nafasi katika utawala. Ni mafanikio ya aina yake nchini japo tayari kuna benki nyingine za kawaida ambazo zinatoa pia huduma kama hii sijui ushindani utakuwaje sasa.
 
alhamdulillah afadhal tutakua na benki isiyo kua na unyonyaji hamna riba.wote mnakaribisha nibenki inayofuata sheria za kiislam ila hata mkristo unaweza kufungua account

Tufahamisheni, kama benki haitozi riba inaweza vipi kuendesha shughuli zake za kila siku.
 
sasa na mikopo inatoa bila riba nije?sababu hilo ndilo lamuhimu sana..nikikopa 10Million baaaa ya 3yrs narudisha 10Million.hapo hata kesho nakuja..
 
Back
Top Bottom