Ama kweli magufuli kiboko apiga kambi daraja la simiyu

Quantum

Member
Oct 28, 2013
53
21
Nilikuwa natokea Musoma kwenda Mwanza juzi jioni pale daraja la Simiyu ambalo ni kiungo muhimu sana kwa barabara ya Mwanza - Musoma tuliposhuka kwa ajili ya ukaguzi, nilidokezwa na waliokuwepo ya kuwa Dr. Magufuli kapiga kambi akifuatilia ukarabati wa daraja hilo ambalo hivi karibuni limekuwa kero kwa watumiaji wa barabara hiyo.
photo 1.JPG
photo 2.JPG
 
jamaa mtambo wa utendaji kwenye hii nchi anafaa kuwa kiongozi amekuwa nguzo mhimu kwenye wizara yake na serikali kwa ujumla.
 
Kama kufanya hivyo ni sehemu ya kazi zake basi hakuna cha ajabu, unaitwa uwajibikaji.
 
Hapo labda alikua anakagua tu,napinga utumizi wa neno ama maneno 'apiga kambi'. Magufuli amepiga kambi hapa Nyakabindi tangu juzi akimsubiri Rais aje kuzindua mkoa mpya wa SIMIYU. Nyakabindi ni mbali sana na hapo darajani unapopataja wewe. Hata ninapotoa jibu hili jamaa yupo hapa anapiga kifungua kinywa. If anything tunaweza kusema 'Magufuli apiga kambi barabara ya Lamadi - Bariadi'
 
pengine waweza kuwa na ukweli - no idea!
 
Hapo labda alikua anakagua tu,napinga utumizi wa neno ama maneno 'apiga kambi'. Magufuli amepiga kambi hapa Nyakabindi tangu juzi akimsubiri Rais aje kuzindua mkoa mpya wa SIMIYU. Nyakabindi ni mbali sana na hapo darajani unapopataja wewe. Hata ninapotoa jibu hili jamaa yupo hapa anapiga kifungua kinywa. If anything tunaweza kusema 'Magufuli apiga kambi barabara ya Lamadi - Bariadi'
f19c62c4935fd59cec0cfc522dbd434d.jpg
 
Mnafiki tu huyo.. Anaonea kampuni uchwara kama yeye mwanaume awafate STRABAG akapige kambi..

Anaiogopa STRABAG kama ukoma baada ya kugundua kampuni ina mtaji kuliko serikali yake iliyomuajiri..

Amezoea kusumbua kampuni za kichina tu kisa hawana nguvu,,

Strabag wanafanya wanavyotaka serikali imeuchuna kama haioni vile
 
Kwa kua aliapa kuwatumikia wananchi hiyo ni moja ya kazi zake anazotakiwa kufanya.
 
Mbona siioni kambi yenyewe? Nilitegemea kuona tent, godoro, sufuria etc ili kuhalalisha maana ya kupiga kambi. Mtu amekaa mkao wa kutimka unasema amepiga kambi?
 
Mnafiki tu huyo.. Anaonea kampuni uchwara kama yeye mwanaume awafate STRABAG akapige kambi..

Anaiogopa STRABAG kama ukoma baada ya kugundua kampuni ina mtaji kuliko serikali yake iliyomuajiri..

Amezoea kusumbua kampuni za kichina tu kisa hawana nguvu,,

Strabag wanafanya wanavyotaka serikali imeuchuna kama haioni vile

Sidhani kama anawaogopa Strabag kumbuka alimtolea uvivu
Yule Mkandarasi wa Ndundu - Somanga;

http://issamichuzi.blogspot.com/2013/07/dkt-john-pombe-magufuli-amwondolea.html?m=1
 
Ok sawa anafanya kazi, sasa vipi kuhusu Morogoro Road ? ukweli tunateseka mfano leo asbh sijuii traffic waligoma au ! maana malori yote yalikuwa kwenye foleni ile saa 12.30 asbh sasa foleni ilianzia suka hadi ubungo, watu tumefika ofcn saa 4.30. hii ni sawa ? Basi akitoka huko simiyu aje apige kambi kimara/ubungo_Other wise ni mnafiki mkubwa.:lying:
 
Mbona siioni kambi yenyewe? Nilitegemea kuona tent, godoro, sufuria etc ili kuhalalisha maana ya kupiga kambi. Mtu amekaa mkao wa kutimka unasema amepiga kambi?

Siku hizi wa-TZ tuna utapiamlo, unyafuzi n.k. wa Kiswahili!!

Poleni sana vijana wa kizazi kipya a.k.a .com! Vijana wa Mulugo haooooo!! Mwandishi hakumaanisha kupiga kambi kwa kulala hapo hapo na kuweka magodoro. Rudi kwa mwalimu wako wa Kiswahili akufundishe maana ya misemo na matumizi ya lugha katika kuwasilisha ujumbe!! Enzi za mwalimu haya makitu yalikuwa yanatembea sana shuleni na mnapata muda wa kujadili darasani!!
 
Back
Top Bottom