Mjanja M1
JF-Expert Member
- Oct 7, 2018
- 4,005
- 14,039
Jina lake halisi ni Benedict Michael Mwakanyamale, lakini wengi katika Jiji la Arusha hasa eneo la Mbauda wanapenda kumuita Chuma. Huyu ndiye muombolezaji aliyeshambuliwa kwa kupigwa ngumi ya uso na mmoja wa watu walionekana kama ni walinzi waliokuwa wakilinda msafara uliobeba mwili wa Waziri Mkuu mstaafu, hayati Edward Lowassa.
“Yalikuwa ni mapenzi tu kwa baba yetu Lowassa,” haya ni maneno ya Benedict Michael Mwakanyamale (43), aliyeshambuliwa jana kwa kupigwa ngumi wakati akiomboleza msiba wa Waziri Mkuu mstaafu, hayati Edward Lowassa.
“Mimi ni mkazi wa hapa Mbauda na hadi kutoka pale barabarani yalikuwa ni mapenzi tu kwa baba yetu tukitaka kumpa heshima za mwisho baada ya kutupambania sana vijana enzi ya uhai wake. Lakini, badala yake nikaambulia kofi la kwenye taya. Kwa sasa najiandaa kwenda Ngarash kushiriki mazishi yake, ili kumpa heshima anayostahili,” amesema Chuma.
“Yaani kupigwa kwangu hakuzuii kabisa kwenda msibani maana sijaumia hivyo, hainikatishi tamaa na hii ni falsafa yetu makamanda wote majasiri, lazima niende msibani kutoa heshima za mwisho kwa mzee wetu,” ameongeza
Source: Mwananchi