Aliyemuita Rais Magufuli kilaza, ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela

Sawa sie wengine ndo wapumbavu na vilaza ila yeye ni 'mtukufu genius'.
 
Baba yako anaweza kukuita wewe mpumbavu njoo hapa na ukaenda bila kusita je wewe unaweza kumwambia hivyo au unaweza kumwita hivyo?hembu tuwe na nizamu na wakubwa sio wa umri tu hata wa cheo
 
Mhasibu wa Shule ya Sekondari St Joseph, Elizabeth Asenga ametiwa hatiani kwa kosa la kumuita Rais John Magufuli kilaza.

Elizabeth ametiwa hatiani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa jamhuri kuthibitisha kosa.

Mhasibu huyo anadaiwa kuandika “hakuna rais kilaza kama yeye duniani” katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Hakimu Shaidi akitoa uamuzi wa mahakama, alimtaka mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh milioni tano au jela mwaka mmoja ambapo amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.

Chanzo: Mtanzania
Wamemuhukumu mwaka mmoja autoshi
 
Back
Top Bottom