Aliyemuita Rais Magufuli kilaza, ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela

Naona father house anazidi kumkingia kifua dogo wake leo hata ile Tume ya madili washapigwa pini kiaina

Ova
Habari za kuamka kamanda.
Hili suala sijalifuatilia kiundani mkuu. Naomba unipe nafasi kidogo nilifuatilie kabla sijatoa jibu.
Au kama unaweza tafadhali nipe hints kidogo "Tume ya maadili" kulikoni?
 
naona mahakimu wetu hawana kesi za kufanya za maana?
anyway.. zama za kilaza zitapita tu
 
Mhasibu wa Shule ya Sekondari St Joseph, Elizabeth Asenga ametiwa hatiani kwa kosa la kumuita Rais John Magufuli kilaza.

Elizabeth ametiwa hatiani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa jamhuri kuthibitisha kosa.

Mhasibu huyo anadaiwa kuandika “hakuna rais kilaza kama yeye duniani” katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Hakimu Shaidi akitoa uamuzi wa mahakama, alimtaka mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh milioni tano au jela mwaka mmoja ambapo amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.

Chanzo: Mtanzania
samahani kuna kitu sijaelewa hapa huyu Eliza alisema“hakuna rais kilaza kama yeye duniani” au alimtaja kwa majina yake kamili
 
Habari za kuamka kamanda.
Hili suala sijalifuatilia kiundani mkuu. Naomba unipe nafasi kidogo nilifuatilie kabla sijatoa jibu.
Au kama unaweza tafadhali nipe hints kidogo "Tume ya maadili" kulikoni?
Sawa ntasubiria taarifa zako kamanda

Ova
 
Sheria ya kipuuzi sana hii!!! Mbona Rais aliwaita vilaza wanafunzi wa UDOM? Inakuwaje sheria hii isimhusu na yeye?
Hii double standard Ipo siku kinachotafutwa kitapatikana!!! Sheria kandamizi kabisa hii.
 
NO ONE IS ABOVE THE LAW EVEN IF THE WORD PRESIDENT IS SUBSTITUTED TO MEAN 'THE KING'

Hon. Rtd. Judge Barnabas Samatta.
 
IMG-20171005-WA0006.jpg

Mhasibu wa Sekondari ya St.Joseph Cathedral anusurika kwenda jela miezi 12 baada ya kulipa faini Sh 5m baada ya kumuita Rais kilaza kwenye WhatsApp
 
Mhasibu wa Shule ya Sekondari St Joseph, Elizabeth Asenga ametiwa hatiani kwa kosa la kumuita Rais John Magufuli kilaza.

Elizabeth ametiwa hatiani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa jamhuri kuthibitisha kosa.

Mhasibu huyo anadaiwa kuandika “hakuna rais kilaza kama yeye duniani” katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Hakimu Shaidi akitoa uamuzi wa mahakama, alimtaka mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh milioni tano au jela mwaka mmoja ambapo amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.

Chanzo: Mtanzania
Na mkuu akituita wapumbavu jukwaani inakuwaje?
 
Back
Top Bottom