Umemtaja Rais Kikwete, nikakumbuka kapata msiba mwingine, ina maana akitoka South anapitiliza hadi Mwanza. Aiseeh!
Mzee Mwanakijiji ni kweli tukio la wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuua si la kuungwa mkono hata siku moja!! Kwa hili la #Mabina kulikuwa na chuki ya muda mrefu sana kati ya wale wananchi kwa kesi hiyo ya shamba. Hasira yao ikakolezwa na yeye kufyatua risasi ovyo na kumuua mtoto mdogo ambae naona watu wengi hapa jamvini hata hawamuongelei!! Kwa hali hiyo sidhani kama hiyo hasira (ya matukio ya kuwatishia kuwapiga risasi mara kwa mara na hili la kumuua mtoto leo) kulikuwa na mtu wa kui-control.Tukio hili ni tukio la kulaaniwa kama yalivyo matukio mengine ambapo wananchi wamechukua sheria mkononi na kuua watu wengine. Ni tukio ambalo pia linahoji tena na tena jinsimfumo wetu wa haki na usalama ulivyo. Kitendo kama hiki kinatokea kwa kiasi kikubwa (kama vitendo vingine vya mob justice) pale ambapo wananchi wanaona wamekata tamaa na kuwa mfumo wa haki hauwapi nafasi ya kupata haki kwa haraka na bila ya kulazimika kutoa rushwa.
Ni kitendo kisichopaswa kupongezwa hata chembe kwani japo leo kinaweza kuonekana kimetokea kwa mtu asiyependwa na baadhi ya watu siku moja kitatokea kwa wale wanaopendwa na wote tutapigwa na mshangao. Tusikubali utawala wa mbwa kala mbwa...
"kazulumu" ndio nini?Sasa na wewe zuzu nenda kazulumu ardhi ya wanyonge uone moto wake....Tutaku-Mabina fastaaa
Mkuu ongea vitu unavyokuwa na uhakika navyo alie uwawa sio mto kama unavyo koleza ni kijana, we unasimuliwa na kusoma kwenye mitandao me tukio nimelishuhudia.Mzee Mwanakijiji ni kweli tukio la wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuua si la kuungwa mkono hata siku moja!! Kwa hili la #Mabina kulikuwa na chuki ya muda mrefu sana kati ya wale wananchi kwa kesi hiyo ya shamba. Hasira yao ikakolezwa na yeye kufyatua risasi ovyo na kumuua mtoto mdogo ambae naona watu wengi hapa jamvini hata hawamuongelei!! Kwa hali hiyo sidhani kama hiyo hasira (ya matukio ya kuwatishia kuwapiga risasi mara kwa mara na hili la kumuua mtoto leo) kulikuwa na mtu wa kui-control.
Mkuu ongea vitu unavyokuwa na uhakika navyo alie uwawa sio mto kama unavyo koleza ni kijana, we unasimuliwa na kusoma kwenye mitandao me tukio nimelishuhudia.
sasa itakuwaje.
Huyu jamaa kiukweli alikuwa mbabe sana kwa sisi tulioko mwanza ndo chamoto chaka tuna kijua.
Hata hicho kifo tu nihaki yake sitahili wala sio mpango wa shetani anabishana na nguvu ya umma, amebakia mwenzake anaitwa matata.
Kama ni kweli, basi hii ni mbaya sana! Wangempeleka katika vyombo vya sheria jamani.