Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara akiwachongea wenzake kwa Rais watumbuliwe

Stress Challenger

JF-Expert Member
Feb 24, 2022
1,778
4,289


Tuna wakuu wa wilaya wapya, tuna wakurugenzi wapya lakini tuna wakuu wa idara ambao bado wapo kwenye mfumo uleule wa upigaji. Walikuwa wanawakandamiza wananchi na wanahujumu miradi ya maendeleo. Muheshimiwa Rais, bila kufumua hawa wakuu wa idara; wengine wame-overstay, watu wa manunuzi, watu wa mipango, watu wa uhandisi, hawa watu wa ma DMO wamekaa muda mrefu wametengeneza syndicate na suppliers.

Mheshimiwa Rais, Mkurugenzi wa Bunda leo kuna wakati anajifungia chumbani analia machozi. Kila ukimuelekeza fanya hivi anakutana na wakuu wa idara pale wanampotosha, wanam-mislead, wafanyi maamuzi. Mkurugenzi wa Tarime vijijini, anaingizwa mkenge na yeye, safu yote ya wakuu wa idara ndio walewale waliofisadi miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Rais, nakuomba na nimemuomba Mheshimiwa Waziri na ninashukuru na wewe yapo maelekezo umeyatoa, iko haja ya kufumua wakuu wa idara. Tumebadilisha wakurugenzi, Mheshimiwa Raisi umetusaidia, umetubadilishia wakuu wa wilaya, lakini wale watendaji wanaowasaidia wakurugenzi sehemu zote nilizozitaja wananuka rushwa, wana urasimu mkubwa, hawafanyi maamuzi na wanaendelea kukumbatia ile mifumo ya zamani.

Namuomba Mheshimiwa Waziri wangu wa TAMISEMI na tayari Mheshimiwa Rais umeshatoa maelekezo atusaidie jambo hili kwa haraka ili mkoa wa Mara ubadilike na wananchi waweze kupata maendeleo. Mara Oyeeee! Pale Butiama na kwenyewe tunatatizo hilo, kuna bwana fedha mmoja yupo pale, Mheshimiwa DC kila siku ananilalamikia. Pesa zinakusanywa, akiziomba anaambiwa nyingine zimetumika kabla hazijaenda benki. Bwana fedha amejaa kiburi, sasa sisi tuna mamlaka ya kuwaamisha ndani ya mkoa, lakini sasa tunaulizana na RAS, huyu anaharibu huku tukimhamisha ndani ya mkoa akaenda halmashauri nyingine hawa wanawasiliana, ataendeleza madudu yaleyale ya kule.

Kwaiyo Mheshimwa Rais, nakuomba sana mama yetu kipenzi msikivu, hili eneo la wakuu wa idara ambao ndio wanatengeneza Council Management Team iko haja ya kufumua na kufanya mabadiliko ili tuweze kupata utumishi uliotukuka kwa wananchi wetu na wananchi wapate maendeleo.

Mheshimiwa Rais nakushukuru tena, nikukaribishe sana Mara, asante sana kwa kunipa nafasi hii, Mara Oyeee!
 
Mkuu kuna mwenye kujua mfumo wetu wa sasa wa wakuu hawa wanawajibika kwa nani?,hivi hawa wakuu wa idara hawawajibiki kwa DED au DC?
 
Siasa za aina yake sana

RC akiwakomalia wasaidizi wake anakuwa na Roho mbaya akiwa pamoja nao anakuwa ameunda genge la upigaji

cha msingi uwe Chawa Platinum tu na kusaka pesa na kulowanisha lowanisha washauri wa Mamlaka za uteuzi
 
Self-Kujitumbua...

Shida alidhani bado yuko enzi za mwendazake..

Hapo ingekuwa enzi za mwendazake angemuona ni bonge la kiongozi na angemvimbisha kichwa haswaaa..

Ila nyakati zimeshamtupa mkono..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom