Alikuwa rafiki yangu

Hold on

JF-Expert Member
Feb 7, 2023
455
1,025
Good morng Tanzanian

Nina shemeji yangu mke wa kaka yangu ambae alikuwa rafiki kwangu tuna shauriana mengi sana mazuri na wakati mwingine kaka yangu akimkosea bas huja kwangu kulalamika nami namtuliza nampa ushauri mzuri na kweli akifwata ana solve vizuri tu

Shida imeaza soon kuna tajiri mtoto kwenye familia yetu na muita ivyo kwasababu umri wake ni mdogo sana sasa kageuka kuwa rafiki yake na baadae ananisagia kunguni kwa ndugu yangu huyo ili aonekane mwema na haya ni baada ya yeye kulamba asali

Dogo anampa hela za nauli na mboga sasa juzi tulikutana tukapiga story baada ya muda nikamuaga nikasema nasepa na mpigia simu dogo ni msalimie ndio anaza kunipa story za shem anasema kuwa wewe unanisema vibaya

Mm bila kujiuma meno nikasema ni kweli kwani ww unajali marafiki kuliko ndugu zako mama yako kila siku analalamika kisa ww kila mtu ankulalamikia wewe unaona good

Akakata simu huyu ndugu yetu ukienda kumsalimia anataka uvae vizuri sana ukivaa kawaida kama ukimkuta na wageni hakutambulishi, aliumwaga akawa amelazwa pale agakhan mama akawa ameenda akamshushua eti umevaaje ivyo mbona ujasuka (alikuwa kasuka twende kilioni) mama hakusema kitu pale kwasababu hospital

Lakini pia ikifika hatua ndugu anamwambia nimekwama nisaidie anakuchamba kwaza na hela unaweza usipate ila rafiki akisema ako na shida chap anatuma pesa

Sasa kinacho nikela ni huyu shemeji huyu namuona kama mgombanish nisha mkataa leo morng kapiga simu nimemjibu majibu ya mkato mkato analalamika sasa
 
Formula ni moja tu ya maisha "CHA MTU MAVI" ukilijua hili hutopata tabu ya kuvalishwa suti ili upate hela ya kula.

Hapa haijulikani nani hasa kakukera zaidi na kipi hasa kilichokukera;

  • Rafiki/shemeji yako kuvunja urafiki na wewe na kukusema vibaya
  • Ndugu yako kujua kuwa umemsema vibaya
  • Maringo ya ndugu yako.

Kwa kifupi jifunze kukinai na nafsi yako na kutofuatilia sana mambo ya watu.
 
Shida huna hela tafuta hela kwa uchungu. Watu wenye hela hawana majungu majungu sisi makapuku tuna majungu sana. .
 
Back
Top Bottom