Alikufa kwa zaidi ya dk 70. Moyo wake umepigwa shoti zaidi ya 15 ndio ukafanya kazi tena

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Nimesoma habari hii ambayo si ngeni kwa wanaofuatilia michezo hasa soka ya england . Ni kuhuus Mchezabi Fabrice muamba mwenye asili ya DRC aliyedondnoka uwanjani wakati wa mechi. Niichojiuiza je inawezeka huku kwetu wengi tunawazika au tutazikwa sababu ya kutokuwepo vifaa na huuma sahihi. Endelea kusoma maajabu ya muamba "kufufuliwa"


Bolton club doctor Jonathan Tobin has confirmed Fabrice Muamba's heart was inactive for 78 minutes following his cardiac arrest.

Muamba continues to show early signs of recovery in hospital, with the player telling Dr. Tobin he feels "fine".
Dr. Tobin visited Muamba on Tuesday evening, and on Wednesday spoke positively of his communication with the 23-year-old, who suffered a mid-game cardiac arrest at White Hart Lane on Saturday. "I'm glad to say that the early signs of recovery have continued," Dr. Tobin said.


"I went to see Fabrice last night. I went in and he said: 'Hi, doc.' I asked him how he was and he said: 'Fine.'

"I explained to him what had happened. That's the sort of level of communication I have had with Fabrice." The doctor admitted he broke down in tears in the corridor as the reality of the situation dawned upon him.


He explained that medics tried unsuccessfully to revive Muamba for 48 minutes before he arrived at the London Chest Hospital and that it then took another half an hour before Muamba's heart started beating again, after receiving a total of 15 shocks.


"In effect, he was dead in that time," said Tobin.Dr. Andrew Deaner, a Tottenham-supporting cardiologist, leapt from his seat in the crowd and rushed on to the field to help Muamba. Dr. Deaner, who is a consultant cardiologist at the London Chest Hospital, said he also been in contact with Muamba since he regained consciousness.


"If you're going to use the term miraculous, I guess it could be used here," he said.

"I whispered into his ear: 'What's your name?' He told me, and I replied: 'I understand you're a very good footballer.' He said: 'I try.'"


Dr. Deaner said he, too, had tears in his eyes after seeing Muamba's sense of humour returning so soon. He recalled how he had been watching the match with his brother when he saw the midfielder collapse.
He said to his sibling: "They're doing CPR. I should go and help." "Something sort of told me I should go down," he said. "The adrenaline starts pumping when you see a cardiac arrest."


He added: "Looking back, it wouldn't have been surprising if the guys there … said: 'Go away, we don't need anybody else.'"But Dr. Deaner was full of praise for how things were carried out. "If you were going to make a film to teach people how to run a complex arrest, this would have been the arrest to film because everything went as it should," he said. "


"One thing after another just went right. He's made a remarkable recovery so far. We don't want to get ahead of ourselves, but as things stand, I think his life is not in danger at this time. His neurological function is looking very good but it is early days."


Mtazamaji's comment/Question
Inasemekana tatizo alilokuwa nalo ni cardiac arrest na sio heart attack.
Je wataaalam wanweza kutuelewesha kwa lugha rais nini tofauti.
 
Jamani wataalamu wa afya mko wapi mtufafanulie tofauti kati ya hayo mawili? Mgomo ulishaisha, kwa tunaendelea kuwasubiri maana tunajua mtakuja.
 
Kuna maelezo marefu sana lakini nitajitahidi kufafanua kifupi na kwa lugha nyepesi kama mleta mada ulivyoomba na kama kuna mahali nitakuwa sieleweki au mtataka niingie kwa undani zaidi basi mnaweza kuniuliza ili twende pamoja:

Heart attack na Cardiac arrest ni vitu viwili tofauti kabisa,japokuwa mara nyingi heart attack ndiyo husababisha Cardiac arrest

Heart attack(myocardial infarction):kufa(infarction or necrosis) kwa baadhi ya chembechembe za uhai za moyo(myocardial cells or cardiac myocytes) kunakosababishwa na chembechembe hizo za moyo kukosa damu(Ischaemia) hivyo kupelekea kutopata hewa ya oksijeni ya kutosha na chakula cha kutosha(sukari).

Cardiac arrest:
Kusimama/kusimama ghafla kwa mzunguko wa damu mwilini kunakosababishwa na kushindwa kwa moyo kudunda(contract effectively)

Mara nyingi heart attack ndiyo chanzo kikuu cha cardiac arrest.Lakini pia cardiac arrest inaweza kusababishwa na magonjwa mengine kwa mfano moyo kujaa maji(cardiac tamponade),mapafu kujaa hewa(tension pneumothorax),damu kukosa sukari ya kutosha(hypoglycemia),madini ya potassium kuwa kidogo au kuwa mengi mwilini(hypokalemia/hyperkalemia) nk.Hivi vyanzo vyote vinasababisha cardiac arrest kwa kuharibu ile pattern ya mkondo wa umeme wa moyo unaosababisha moyo kudunda ili uweze kusukuma damu.Kwa kitaalam hii hali inaitwa arrhythmia.
Kuna aina nne za arrhythmia zinazoweza kusababisha mzunguko wa damu mwilini kusimama(cardiac arrest).Nazo ni;Ventricular fibrillation,Asystole,Pulseless electrical activity na pulseless ventricular tachycardia(samahani sijui kiswahili chake!)

Matibabu ya cardiac arrest yanategemea chanzo cha cardiac arrest na ni lazima yaanze haraka ili kumuepusha mgonjwa na kifo au uharibifu wa ubongo wa kudumu(permanent brain damage).Matibabu yanaweza kuwa;massage ya moyo(chest compressions) na kumpatia mgonjwa hewa ya oksijeni,defibrillation,pacing na dawa.Huyo mchezaji inaelekea alipata ventricular fibrillation au pulseless ventricular tachycardia ndiyo maana alipata hizo 'shocks' from a defibriillator.
Shock actually ni umeme ambao unatibu/ondoa sasa ile arrhythmia iliyosababisha moyo usimame na hivyo kuufanya moyo uanze kufanya kazi tena.Atakuwa na bahati sana kwa kupona na kama hatakuwa na brain damage yoyote kwa muda wote huo ambao moyo ulisimama na kufanya damu isifike kwenye ubongo.

Defibrillators ni muhimu sana ingewezekana na sisi tungekuwa nazo walau AED kila mahala penye mkusanyiko wa watu wengi kama sokoni,kwenye viwanja vya mpira,airport nk na pia walau tungetoa mafunzo ya basic life support labda kwa kila mwanafunzi wa sekondari au darasa la saba,kwa sababu naamini kuna vifo vingi tu vya ghafla watanzania tunakamatana uchawi na majini kumbe sababu yake ni cardiac arrest
 

cardiac arrest ni pale moyo unaposimama kabisa kufanya kazi. Hii inaweza kuwa kusimama kusambaa kwa umeme ndani ya moyo au kusimama kusukuma damu au vyote viwili kwa pamoja. Huweza kusababishwa na hyothermia, HYPOXIA, hypovolemia,toxins, cardiac tamponade, tension pneumothorax, hypo/hyperkalemia,heart attack nk( sory kwa kuandika medical terms,kiswahili maneno mengi:) Kurudisha uhai wa mtu huyu inahitaji kufanya cardiopulmonary resucitation au defibrillation. Heart attack ni pale sehemu ya misuli ya moyo inapokosa oksijeni na kuacha kufanya kazi lakini zile zinazopata zikiendelea. Hii husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu ya moyo ya sehemu hiyo. Kwa sababu sehemu za moyo hutegemeana hii inaweza kusababisha moyo kusimama kabisa.
 
this must be another miracle. After 70min and he still regains consciousness.
 
Salaaaaaam wana JF
Tatizizo kubwa katika nchi zetu ni:

  1. kukosa commitment, vifaa na wataalam.
  2. Kutojua umuhimu. Kwa Mwamba iliwezekana kutokana na umuhimu wake katika timu yake.
 
Salaaaaaam wana JF
Tatizizo kubwa katika nchi zetu ni:

  1. kukosa commitment, vifaa na wataalam.
  2. Kutojua umuhimu. Kwa Mwamba iliwezekana kutokana na umuhimu wake katika timu yake.

3.Madaktari wetu wengi yanapotokea matukio kama haya wanakuwa wako gesti au bar so wanashindwa kuwahi kutoa huduma
4.Na hata kama wako karibu kutokana na uvivu wa kusoma hujikuta wanaanza kupekua mavitabu kujikumbusha notes za chuo zinasemaje juu ya tatizo hilo
5.Hata wakiwahi bado wanakuwa busy na kushika shika simuna kutuma meseji kuagiza kilo 2 za kitimoto na ndizi 4 ili akitoka hapo aende kula na ndovu mbili baridiiiii
 
...............

Defibrillators ni muhimu sana ingewezekana na sisi tungekuwa nazo walau AED kila mahala penye mkusanyiko wa watu wengi kama sokoni,kwenye viwanja vya mpira,airport nk na pia walau tungetoa mafunzo ya basic life support labda kwa kila mwanafunzi wa sekondari au darasa la saba,kwa sababu naamini kuna vifo vingi tu vya ghafla watanzania tunakamatana uchawi na majini kumbe sababu yake ni cardiac arrest

Mkuu hili somo la First aid na basic life support ni muhimu lifundishwe primary na sekondary kwa leve tofauti.

BTN
Aksante sana kwa maelezo matamu .Nimesikia pia mtu anasema kijana kama muamba kwa umri wake kiafya hawezi kupata heart attack. Yeye andai heart attack inatokea kwa rika fuani tu na ni umri mkubwa.

Na ile dini nyingine wanavyokimbilia kuzika si ndio balaa....

Acha uchokozi..
 
Mkuu hili somo la First aid na basic life support ni muhimu lifundishwe primary na sekondary kwa leve tofauti.

BTN
Aksante sana kwa maelezo matamu .Nimesikia pia mtu anasema kijana kama muamba kwa umri wake kiafya hawezi kupata heart attack. Yeye andai heart attack inatokea kwa rika fuani tu na ni umri mkubwa.

Mkuu Mtazamaji:Ni kweli heart attack mara nyingi hutokea kwa 'wazee' hasa kwa sababu ya kujazana kwa mafuta(cholesterol hasa aina ya cholesterol iitwayo LDL=low density lipoprotein) kwenye mishipa yao ya damu inayopeleka damu kwenye moyo(coronary circulation) na hivyo kuifanya mishipa hii izibe,hivyo ishindwe kupeleka damu kwenye moyo.

Vilevile uzee pia unaambatana na mgandamizo mkubwa wa damu(high blood pressure/hypertension)na mabadiliko ya structures za moyo na mishipa ya damu mwilini na kuifanya ipoteze ile character yake ya kutanuka(elasticity),pia kutokuwa smooth,kuwa na bends(tortuous) hivyo kuliongezea hili kundi mazingira hatarishi ya damu kuganda(thromboembolism) na kuiziba mishipa ya damu na kuifanya ishindwe kupeleka damu kwenye moyo.

Lakini si kweli kwamba kundi hilo tu ndilo linaloweza kupata heart attack.Mtu wa umri wowote anaweza kupata heart attack.Hata watoto wachanga wanaweza kupata heart attack.
Kumbuka heart attack ni kufa kwa chembechembe za uhai za moyo kunakosababishwa na kukosa damu kama nilivyosema pale juu.
Hivyo kuna mechanisms 3 zinazoweza kupelekea mtu kupata heart attack.

1)Kupungua kwa supply ya damu kwenda kwenye moyo
2)Kuongezeka kwa mahitaji ya damu katika moyo.Hapa inawezekana kabisa supply ikiwa nzuri tu,lakini kwa vile demand imeongezeka,basi cells nyingine za moyo zinaweza kukosa damu ya kutosha
3)Mechanisms zote mbili hapo juu zinaweza zikatokea kwa pamoja

Mechanism ya kwanza ndiyo mara nyingi inasababisha heart attack.Inawezekana mishipa ya damu ikaziba,hivyo kushindwa ku supply damu ya kutosha kwenye moyo.Hapa inawezekana ni kwa sababu ya yale mafuta(cholesterol) niliyosema,ama trauma/ajali kwa mfano inayoharibu mishipa ya damu hivyo kufanya moyo kukosa damu(utaona hapa sasa hata kijana au mtoto anaweza kupata heart attack),magonjwa ya mishipa ya damu kwa mfano Kawasaki disease yanaweza kusababisha heart attack hasa kwa watoto,upungufu wa damu mwilini(severe anemia) pia inaweza kusababisha heart attack,mshipa mkubwa wa damu unaotoa damu kwenye moyo na kuisambaza mwilini kuwa mwembamba(severe aortic stenosis)unaweza pia kusababisha heart attack katika umri wowote,nk nk

Nisikuchoshe kwa maelezo marefu mkuu,ila kama utapenda naweza kuendelea kuzielezea mechanisms zilizobaki katika post nyingine
 
Back
Top Bottom