Alicho-jionea Naomi Campbell!

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,845
7283d1262001582-alicho-jionea-naomi-campbell-scan0002-copy.jpg

scan0002 - Copy.jpg
scan0001 - Copy.jpg

...Maisha bora kwa kila mtanzania, Inawezekana!
(Mods, nimeshindwa kuikuza hii pic, ...click attachment for larger version)
 
certainly ilikuwa BORA MAISHA kwa watanzania walio wengi!ofcourse hawezi kudisplei feelings zake that much straight,lakini her perceptions EXPLAINS
 
mamawee! hapa ndo tunamuona gavana anajenga nyumba yake kwa 1.4bil, hawa watu wapo kwenye nchi iliyojaa madini ya kila aina, ardhi yenye rutuba na rasilimali kibao. Tena wanae mbunge wao mwenye afya na raha tele kila siku. Viongozi kibao wamewazunguka watu hawa, viongozi wasiokera, wasio na huruma hata kidogo.

mbaya sana.
 
...Nemesis, mbunge atajali wapi ikiwa ana privileges za kutibiwa Grade One Muhimbili, South Africa, India au Ulaya kwa pesa ya kina mama hao ambao wengi wao hapo utakuta ni house wives, mama lishe, nk?

Mawazo yangu yananiambia tumeuzoea sana umaskini kiasi kwamba hizi shida machoni mwa wengi ni kitu cha kawaida tu, au utawasikia wengine wakijipa moyo ati kina mama wanaozalia huko vijijini wana hali duni kuliko hii...
 
Hawa Watanzania wanajitakia wenyewe.

Uchaguzi ukifika wanapata Tshirt za kijani na njano.

Akina mama wanapata Kanga na mwisho wote wanakula Pilau.

Wakitoka hapo ni CCM tu. Miaka 40 badi hamjafunguka macho.

Mwisho mtu unasema ACHA WAFU WAWAZIKE WAFU WENZAO.
 
Alafu kuna watu (should read mijitu) wanakuja hapa kumtetea gavana kujenga nyumba ya TZS 1.4 billioni, vipaumbele vyetu sijui viko wapi.
 
Mwingine natetea ununuaji wa magari sijui mia ngapi vile????? Kifua mbele, eti "chama chetu ni kikubwa, bla bla bla......"

Ila kofia, khanga na tshirts si tunachukua wenyewe (should not read to mean everyone but those who do take them), wacha watuchore kwa miaka mingine 100.

Tuamke!
 
Hawa Watanzania wanajitakia wenyewe.

Uchaguzi ukifika wanapata Tshirt za kijani na njano.

Akina mama wanapata Kanga na mwisho wote wanakula Pilau.

Wakitoka hapo ni CCM tu. Miaka 40 badi hamjafunguka macho.

Mwisho mtu unasema ACHA WAFU WAWAZIKE WAFU WENZAO.

Hii yote inasababishwa na upungufu wa uelewa kuhusu haki muhimu za msingi katika maisha ya wao kama wananchi.

Alafu kuna watu (should read mijitu) wanakuja hapa kumtetea gavana kujenga nyumba ya TZS 1.4 billioni, vipaumbele vyetu sijui viko wapi.

Kuna gap kubwa sana ya uelewa wa mambo na hii yote inatokana na kubadilishwa kwa curriculum ya siasa ama somo la siasa kutopewa nguvu kamili katika mashule kuelimisha wananchi waendeo shule. When are we going to have this revolution jameni.
 
Mmmmmhhhhhh ningekuwa mimi (kama siwezi kusaidia kubadilisha haya maisha) nisingethubutu kugombea hata udiwani achilia mbali huo urais na ubunge!! Hii ni laana, 2 days before 2010.
 
Mmmmmhhhhhh ningekuwa mimi (kama siwezi kusaidia kubadilisha haya maisha) nisingethubutu kugombea hata udiwani achilia mbali huo urais na ubunge!! Hii ni laana, 2 days before 2010.

...Huwezi jua, labda ndio njia mbadala kuwatishia kina mama wafuate 'nyota ya kijani'.
 
Halafu cha kusikitisha zaidi utakuta wamama hawa hawa ndio wanaishabikia ccm ati! ni ajabu na kweli.
 
Hiyo ilikuwa Temeke-DSM, angeenda huko vijijini akajionee wajawazito wakizalishwa kwa mwanga wa kandili tena baada ya kutembea kilometa za kutosha kuitafuta hiyo huduma.
 
Back
Top Bottom