"Ali Hassan Mwinyi" Humble and Wise

Hivi ile hazina ya dhahabu iliyonunuliwa na BOT miaka ya mwishoni mwa miaka ya 80 na mwanzoni mwa 90 ilienda wapi ? kuna muda Gavana Ndulu alidai siku hizi wanaweka akiba kwa Dola/Euro ambao ni wendawazimu ukiona bei ya dhahabu inavyopanda kila kukicha.
 
'...humble and wise'... IPTL hivi tunalipa bei gani vile kwa siku?!
Ufisadi wa msafara wake kwenda mkutano wa Rio de Janeiro...
Kuuzwa maeneo gani vile?
Hivi pale ikulu kuliwahi kuwa na ndege aina ya tausi halafu ikawaje?
 
Bila kujali kuwa madirisha yalikuwa na nyavu za kuzuia mbu na wadudu wengine kuingia au la, Mwinyi alifungua madirisha tukapata hewa lakini tuling'atwa na mbu na sasa tunaugua malaria sugu. Kupona ni bahati sana na inaweza kuchukuwa generations kupata dawa ya kutibu malaria sugu! Wise?
 
...Mwinyi mwaka 1985 ulipoingia ulikuta BoT kumekauka hakuna hazina ukaanzisha utaratibu wa kununua Gold ili kuwa hazina ya Taifa

...Ulikuta watu wako hawana nguo, vyombo, TV, (maisha ya kijima) ukaruhusu (ruksa) biashara halali watu wenye uwezo wakaanza kufanya biashara taifa likapata neema watu wakaneemeka

...Shule ulikuwa lazima "UCHAGULIWE" ukaruhusu shule binafsi watu wengi tukasoma...kumbe wengi tulikuwa tunafaulu..bana (umeondoa pazia la ujinga na ubaguzi wa ki-elimu

...Wote wanaondika hapa JF ni kazi yako, uliruhusu passport kutolewa siyo kwenda East na West pia..watu tukasafiri tukasoma, tukapata maarifa..

Ali Hassan Mwinyi you are humble and WISE.

* Ukaanzisha AZIMIO LA ZANZIBAR - KUVUNJA SHERIA ZA VIONGOZI WA NCHI NA KUPINGANA NA AZIMIO LA ARUSHA

* Ukaruhusu Wafanya Biashara kugombea Ubunge na kuruhusu Viongozi serikalini kumiliki Ardhi Mali wakati wakiwa Madarakani

* Ukaruhusu Uhuru zaidi wa DINI hivyo kualika dini mbalimbali na pia kuashiria dini zingine kuwa na mrengo mkali

* Yeah Serikali ikaanza kununua Dhahabu halafu kuuza hazina yote ya Dhahabu iliyokuwa nayo iliyokuwa inaifanya fedha za nchi isishuke thamani

* Ukaruhusu Biashara Haramu Ndani ya Ikulu ikiongonzwa na Mama Ruksa; watu wakawa wanapitisha Bidhaa Airport Dar kama karanga

* Ukamleta Mwanao kumpa ubunge na kuhakikisha Azimio la Zanzibar pia liliua JKT; Mwanao alisoma nje kwahiyo hata kulazimishwa kwenda JKT

* Ukakifanya CCM chama cha kirafiki na kindugu

* Shule Tumejenga lakini; Yeye Mwinyi na Kikwete na Viongozi woote sasa wanapeleka Watoto Wao Nje ya Nchi; na ELIMU YETU IMESHUKA

* Mwanzo WA UFISADI, ARDHI LOLIONDO KUCHUKULIWA NA WAARABU N.K

* ULITUGAWA kwa UDINI
 
Mtayasema mengi na kujaribu kulazimisha kufafanisha viongozi wetu lakini Nyerere amesimama peke yake..

KATIKA KUMU ENZI NYERERE TUMEJIFUNZA MIMI?

Ni rahisi sana watu kupanga siku za maadhimisho ya mwalimu Nyerere na hata kubishana ni siku gani iliyo bora zaidi. Ni rahisi pia kupitia hotuba za mwalimu ukazisoma na kumbua mazuri mabaya na usia kama kioo cha utabiri na matukio mengi yanayotuhusu kama jamii, lakini haitakuwa na maana yoyote ikiwa hujajifunza lolote kutokana na uongozi wake na ukatumia mafundisho yake kuwa msingi wa mtazamo, msimamo na mwelekeo wa Tanzania uitakayo..

Binafsi yangu yapo mengi sana nilojifunza, pamoja na kwamba watu wameandika vitabu, wengine hata kumuiga sauti ktk mazungumzo yao, na wengi zaidi kutumia mifano yake ktk simulizi za hoja zao ili zipate mshiko..Lakini kubwa zaidi ambalo mimi nalikubali kwa mwalimu ni ujumbe wake unaohusu zaidi Utajiri wa roho...ile HADHI ya kuwa huru na mwenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kuthamini UTU bila kushawishika na mataifa au utajiri wa mtu, bila kujali rangi, kabila au jinsia.. Waswahili husema - Maskini Jeuri, lakini tafsiri haswa ya fikra na mtazamo wa mwalimu ilikuwa na malengo ya wananchi kuwa na ROHO ya KITAJIRI japokuwa ni MASKINI wa mali.

Nimesoma vitabu vingi vya mwalimu na mara nyingi nimekuwa nikijiuliza ujasiri ule kaupata wapi? ni shule gani ilomfundisha maswala mazito yenye uzalendo ambao sii rahisi kwa viongozi wengine kuufuata hali kazi waliyokabidhiwa na wananchi ni ile ile, mamlaka ni yale yale lakini wameshindwa hata kujiwekea legacy ambayo itawakumbuka kwa mafundisho ama matendo yao. Africa nzima tuna viongozi wachache sana wa mfano wa mwalimu na wote ambao wanakubalika leo, ni wale waliojenga Utaifa wakaweza kuzitajirisha nyoyo za wananchi kwa kuwapa imani ya thamani ya UTU wao. Namkumbuka Abdi Nassar wa Misri, Kwame Nkurumah wa Ghana na SekoToure wa Guinea ambao kamwe hawatasahaulika kwa misingi walioiacha ktk ujenzi wa imani zetu..

Leo hii, Tanzania yetu imejaa watu na viongozi ambao hawana kabisa Utajiri wa roho, maamuzi na matendo yao ni ya kitumwa zaidi ya wakati tuliotawaliwa. Tumezidi kutokomea ktk lindi la umaskini wa roho kiasi kwamba juhudi zote za mwalimu na waasisi wengine wa Uhuru wa mwafrika katika ujenzi na utambulisho wa UTU wetu zimepotea kwa kasi kubwa sana na hivi sasa tumerudi ktk Utumwa na umaskini wa roho kiasi kwamba adui mkubwa wa mwafrika ni mwafrika mwenzake, ni jirani yako ni rafiki yako na pengine hata ndugu yako!.

Na athari za umaskini wa roho unajitokeza wazi - roho mbaya, watu wamekuwa wabinafsi, Uzalendo ni utamaduni uliopitwa na wakati, kati ya watu 10 wanane hawaaminiani, na hakuna mtu anataka kuaminiwa isipokuwa kuogopwa. Tumeipoteza FAITH kwa sababu hatujui tunakwenda wapi, hatuna dira ya kitaifa wala haihitajiki. Umaskini wa roho umeondoa trust, hope and Belief ya UTU wa Mtanzania kiasi kwamba tumechukua utajiri wa Mali kuwa kigezo cha Tanzania mpya...Na hakika UFISADI ni matunda ya umaskini wa roho kwa sababu hakuna mtu hatari sana kama maskini wa roho anapokabidhiwa mamlaka ya kushika mali..Maskini wa roho huongozwa na vitu vitatu Ignorance, greed and selfishness.
Ni bora ukutane na Tajiri maskini wa roho, kuliko kukutana na maskini wa mali na roho...
 
Mbona thread za nyerere na wanaomuabudu ziko nyingi huko hebu tupe nafasi tujadili watu wengine huyo kwetu ni kichefuchefu
 
* Ukaanzisha AZIMIO LA ZANZIBAR - KUVUNJA SHERIA ZA VIONGOZI WA NCHI NA KUPINGANA NA AZIMIO LA ARUSHA

* Ukaruhusu Wafanya Biashara kugombea Ubunge na kuruhusu Viongozi serikalini kumiliki Ardhi Mali wakati wakiwa Madarakani

* Ukaruhusu Uhuru zaidi wa DINI hivyo kualika dini mbalimbali na pia kuashiria dini zingine kuwa na mrengo mkali

* Yeah Serikali ikaanza kununua Dhahabu halafu kuuza hazina yote ya Dhahabu iliyokuwa nayo iliyokuwa inaifanya fedha za nchi isishuke thamani

* Ukaruhusu Biashara Haramu Ndani ya Ikulu ikiongonzwa na Mama Ruksa; watu wakawa wanapitisha Bidhaa Airport Dar kama karanga

* Ukamleta Mwanao kumpa ubunge na kuhakikisha Azimio la Zanzibar pia liliua JKT; Mwanao alisoma nje kwahiyo hata kulazimishwa kwenda JKT

* Ukakifanya CCM chama cha kirafiki na kindugu

* Shule Tumejenga lakini; Yeye Mwinyi na Kikwete na Viongozi woote sasa wanapeleka Watoto Wao Nje ya Nchi; na ELIMU YETU IMESHUKA

* Mwanzo WA UFISADI, ARDHI LOLIONDO KUCHUKULIWA NA WAARABU N.K

* ULITUGAWA kwa UDINI

Ukaleta usawa katika dini waliokutangulia walikuwa wanaamini anayeweza kufanya kazi serikali lazima awe mkatoliki tu..

Yes ukaamua kubadilisha azimio la arusha kwakuwa lilikuwa gandamizi na la kibaguzi..lilikuwa linanya'anya mali za watu na kuua enterprnueal skills..

Yes you are great and humble
 
Back
Top Bottom