Alex Ndeki (mzungu wetu) tumkumbuke

kwa kweli nimekumbuka mbali jamani longer wapi siku hizi na ndgugu yetu mkingule nasikia ni kanali wa jeshi makao makuu, longer yuko nmb dsm, maskini thomas ndulute alifariki kama miaka mitatu iliyopit ,nimecheka sana kuhusu hassan musa alianza ufisadi na mwalimu wa usafiri kutulangua tiketi za train na alikuwa analeta chachacha toka kigoma, jamani kama kuna mwenye mawasiliano na koplo wetu mashaka ndonde aziweke hewani contact zake msimsahau mwalimu kimalamashwi yuko wapi jamani

Ndugu yangu Talumba Mkiwa: Leo umenipa ripoti inayonisikitisha sana kwamba nae Ndulute alifariki dunia..namfahamu vyema jamaa nae alikuwa ni mmoja wa Viongozi wetu enzi zile za TS.Kuna mtu hapo awali amezungumzia Snake House.....Mimi nakumbuka Ghatundu.Hivi kuna mtu humu anajua maana haswa ya Ghatundu?Ilikuwa ukiingizwa mule kwenye kikao cha nidhamu unaona cha moto! Mwenyezi Mungu ampumzishe pema peponi Mzungu,Tutamkumbuka daima!
 
Koplo wenu Mashaka Ndonde ni mtu mzito siku hizi......Anapatikana sana pale Sinza.
Hata mimi namkumbuka makarateka Warioba,Afande huyu mtaalamu wa viungo alikuwa chachu katika kuchakachua utukutu sugu....... Ingawa alionekana mtulivu wakati akitoa somo la miondoko,ikiwamo ghost walk......Alikuwa akiwachenjia kinoma wateja wa gatundu
 
Ndugu zangu wapendwa hawa ndio wana TS waliojitokeza kwamba ni wana JF
1.Baija Balobi
2.Mwawado
3.Kinyamana
4.Kizimkazi
5.Kimatire
6.Tukutuku
7.Snake House
8.Talumba Mkiwa
9.Yomba Yomba
10.Mzawa Halisi
 
Narudi tena Jamvini kumkumbuka Alex Ndeki,Matunda yake tunayaona kina Masaburi sasa ni Meya wa Jiji la Dar, Wengi tuko ughaibuni tukikutana tunakuwa kama watoto wa mama mmoja.
 
Ndugu zangu wapendwa hawa ndio wana TS waliojitokeza kwamba ni wana JF
1.Baija Balobi
2.Mwawado
3.Kinyamana
4.Kizimkazi
5.Kimatire
6.Tukutuku
7.Snake House
8.Talumba Mkiwa
9.Yomba Yomba
10.Mzawa Halisi

Mimi pia ni mwana TS damu damu; nilikuwa kwenye Kizigo Jazz nyakati za Makongoro kwa muda na vile vile kwenye Brass chini ya Mmari wa Ujerumani na Mgandu (oh wonderful). Drum major wetu wa Brass nadhani Muturi au Kituri, sikumbuki jina sawasawa, na Fredrick ... somebody (jina la kihaya nalo silikumbuki)

Nilisumbuliwa sana na watu Gatundu wa ingawa sasa majina yao yameshanitoka, ila sintamsahau General Gimonge (ambaye wakati huo alikuwa Luteni) alivyowahi kutusumbua na nyota zake mbili na "Masiginecha ya Rais." Najua kuwa Colonel Tarimu (wa siasa) kastaafu ukuu wa mkoa, ila sina uhakika na Colonel Hiza aliishia wapi kwenye CCM ingawa nina taarifa kuwa Colonel Kisenge alishafariki na General Gimonge naye keshastaafu. Hao ndio walikuwa wakuu wa Gatundu wote wakiwa maluteni wakati huo, ingawa Tarimo na Hiza walipanda mapema na kuwa makapteni kwa vile tulipiga kwata nzuri sana ya Section Battle Drills mbele ya Waziri Mkuu Kawawa, ila wao ndo wakapata credit..
 
Du hiyo inaleta mshikamano hasa wako wengi sana sana wana TS kule kwenye FB kuna group kubwa la wana TS labda muwe mnapita pita nako kule maana kizazi ki kirefu sana sana...tangia 50's to date yaani mtashangaa watu ni wengi sana sana!!
 
Mimi pia ni mwana TS damu damu; nilikuwa kwenye Kizigo Jazz nyakati za Makongoro kwa muda na vile vile kwenye Brass chini ya Mmari wa Ujerumani na Mgandu (oh wonderful). Drum major wetu wa Brass nadhani Muturi au Kituri, sikumbuki jina sawasawa, na Fredrick ... somebody (jina la kihaya nalo silikumbuki)

Nilisumbuliwa sana na watu Gatundu wa ingawa sasa majina yao yameshanitoka, ila sintamsahau General Gimonge (ambaye wakati huo alikuwa Luteni) alivyowahi kutusumbua na nyota zake mbili na "Masiginecha ya Rais." Najua kuwa Colonel Tarimu (wa siasa) kastaafu ukuu wa mkoa, ila sina uhakika na Colonel Hiza aliishia wapi kwenye CCM ingawa nina taarifa kuwa Colonel Kisenge alishafariki na General Gimonge naye keshastaafu. Hao ndio walikuwa wakuu wa Gatundu wote wakiwa maluteni wakati huo, ingawa Tarimo na Hiza walipanda mapema na kuwa makapteni kwa vile tulipiga kwata nzuri sana ya Section Battle Drills mbele ya Waziri Mkuu Kawawa, ila wao ndo wakapata credit..
Huyo hapo juu ni hayati sasa,mwaka wa tatu sasa.
 
Huyo hapo juu ni hayati sasa,mwaka wa tatu sasa.

ED4.JPG

APUMZIKE KWA AMANI MZUNGU WA SIKONGE
 
Hi KITULA yupo wapi sasa hivi? mara ya mwisho kukutana naye ilikuwa 1980 akiwa Luteni makao makuu ya divisheni ya magharibi Tabora, na msaidizi wa kapteni Fara ambaye sasa ni brigedia generali. Anayejua wapi yupo nitashukuru saana

Kitula alistaafa jeshini yupo uraiani mimi nilikuwa ts toka 71 na akina Mwakyembe,Mahingila wa Brela,brigedia generali Kariongo,kanali Msechu na wengine nashukuru kaw kukkumbuka Ndeki naitwa Paul Seme
 
Tukumbuke na majina haya, Mbarara, Nyangala, puli, unyuka, umwamba, mapeople, walezi, ant lea, wacheuzi, wafaraguzi, kuengua, kimungumungu
 
Du ubarikiew kunikumbusha mbali,igawa nimechelewa sana kuchangia hoja hii nyeti kwa wa tabora boys. Emanule Ndomba nilikutana nae idm mzumbe 1994,Nsato ni OC CID kondoa.hamisi makala ni hakimu dodoma,Dendula mpwapwa,Mwl shendu head master dodoma bush,kitemangu(mlami) alistaafu,yule kota master(1982-83) jina nimesahau anauza samaki mtela,Masamaki tiagi kamishna TRA. wengine nakumbuka sura tu na jinsi walivokua wakifanya mbarara kwenye misosi. Nakumbuka yale magogo jikoni na mashoka mpini chuma,uchotaji maji ndoo 20 kitete..viboko vya Gatundu na yulle sir meja 'nikisema down unakwenda juu nikisema chini unakwenda chini'...dogolomanching badala ya double match..Snaake house haipo ni mijengo tu huko.
 
Mmenikumbusha mbali saana, kuna siku lile master parade la Jumamosi ilikuwa balaa maana bila kujua tukaona mwalimu mkuu anatinga na mama amefuatana naye. Baada ya muda anatangaza kuwa mama ana madai kuna njemba ilikuwa kwake usiku na imemega na kulala mbele bila kulipa ha haha. Tukaambiwa wote tutoe kofia, ohh mama akaanza kupita mpaka akmpata jamaa anywauy kwa heshima ngoja nihidhani jina lake.

But TS, was a model to be proud of it.

Hivi Eric Mwaijande yuko wapi??

Sasa mbona umeshamtaja jina lake
 
nilkuwa ts kuanzia mwaka 1971 mpaka1976 namkumbaka sana mwalimu Ndeki alinifundisha fizikia nacokumbuka alitengeneza kituo cha kurushia matangazo ya redio enzi hizo watu walishangaa sana,kuna mtu alimuulizia Kitula amestaafu jeshi wana ts wengine ni brigedia jenerali Kqriongo mkuu wa chuo cha monduli,waziri Mwakyembe,Mahingila wa brela,
 
Kweli mmewataja wengi sana products za Ndeki hata kaka zetu waliotutangulia wameonyesha kuwa pamoja nasi. Haya shime tumkumbuke Major General Hashim Mbina ex -TS aliyetutoka siku si nyingi.Amekuwa mstari wa mbele kutuunganisha na kujaribu kutuleta pamoja wana TS kokote kule tuliko.:panda:
 
Alexander Ndeki (Mzungu) wengi wetu tuliofanikiwa kuwa TS kipindi chake (1978 - 1986) tunamkumbuka huyu baba kwa mengi aliyotutendea hadi leo tukaitwa wana wa nchi.Basi tusimame wote japo kwa dakika moja tu tumkumbuke!!!Masaburi Upo?Neva Mkadala Je?Makongoro uko wapi?Daudi Salum, kina Ndalichako,Nshushu,Masista duu na wana Warsaw wote njooni basi kwa sala ya kumkumbuka shujaa wetu.
dah! huyu jamaa nilienda mbulu kijiji cha dongobesh nikapata historia yake, baada ya muda naona kwenye tv amefariki
 
Back
Top Bottom