Alert: Tujihadhari matapeli mlimani city

Nashukuru sana mdau, kwa kweli me kosa langu lilikua ni kuwaamini hawa jamaa na pia nimeshafanya biashara mara nyngi tu hapo Mlimani City na sijawahi pata hii zarau na deals zote zilikuwa znaclose pia normally huwa naku na company ila jna niliku mwenyewe tu,naamini kabisa ktk yote ya uzembe,ujinga etc lakini lengo langu ni kujulisha wadau wengine na kuwapa tahadhari wasije fanya mistake kama hii yangu. Kiongozi ningependa kukujuza kwamba Wanaokosea si wote hawana akili ndo maana nikaleta hpa jamvini kwa ajili ya kukosolewa,kusaidiwa,kuelekezwa,na si kutusiwa ya nguoni,I wonder why other people don't understand my courage an desire to help others not be trapped foolishly like this. Thanks for your disappointment character though!!

Pole sana mkuu.Wapuuze watu wanojiona wanajua kila kitu dunia hii.Infact ulijitahidi kuwa suspicious mpaka kufikia kucheck number ya gari.Binafsi nisingeweza kufikiria kitu kama hicho.Unajua kama mtu hauna mentality ya uhalifu au haujawahi kusikia/kutokewa na matukio ya uhalifu wa aina hiyo inakuwa vigumu kuamini kwamba mtu mwingine anaweza kukufanyia uhalifu kwa hiyo utajikuta unamuamini mtu kwa muda mfupi tu mliofahamiana.Pole sana mkuu
 
Tatizo letu ni infatuations na Mlimamni City.......sijui kwa nini.........ukimwambia mtu tukutane MC anakuja baruti as if pale ni Peponi....mimi sipapendi kabisa....am not comfortable nikiwa pale...kila mtu kizungu kingi....baiskeli marufuku....bajaj haziingii yaani panazidi hata ikulu!..ila pole sana mpwa niliitamani sana ile ACER
 
pole nenda kariport police halafu uende offisi za tigo waombe wakube history ya hiyo namba huwa inawasiliana na nani na huyo aliejisajili kwa namba hiyo utaweza kuwatia hatiani hao wezi.
 
Kuna wakati waliibuka wezi wa simu wakijifanya wanunuzi wa magari, kama umetangaza kuuza gari anakupigia mnakutana anaikagua gari yako (very seriously) kiasi ya kukutoa mashaka na kuamini ni mnunuzi halisi, kisha anakwambia mwende Bank (posta mpya ama millenium) njiani anakuomba simu aweke line yake(atasingizia yake imeisha charge) mkifika anashuka na simu yako ndo keshaenda! Wana JF tuwe makini and suspicious of everything kama tusivowaamini viongozi wa ccm kwenye kila inshu ya kitaifa i.e mikataba
 
Mimi naomba tuipokee taarifa hii kwa tahadhari na sio kwa kumlaumu kama hatujawahi kutapeliwa.Maana hata wengine wakiwa na kitu cha manufaa wataogopa kupost sasa.
pole sana ila sikushauri kabis auende kwa MGANGA WA KIENYEJI YEYOTE KWANI HAPA UTAZIDI KUWA MJINGA.WEWE WAOMBEE TU MUNGU ATAFANYA NJIA.
 
Yaani,nimeapa nitakufa no hwa jamaa,nshukuru data zangu zote zpo ktk external. Nimeongea na wale maaskari wa parking wanasema jana yke kuna dada kalambwa million 5 alikua ananunua gari toka kwa watu wa design hiyo. Thanks Mkuu.

Cha kufanya hapo ndugu tuma kama elfu ya tigo pesa kwenye namba hiyo itakupa details za huyo mtu yaani jina, namba ya kitambulisho chake na mahali kilipotolewa hizo ni baadhi ya information za kuanzia na akipatikana mpige picha yake na uitoe ha jf. Pole sana ndugu yangu Mungu takusimamia
 
aisee pole sana mkuu
hata mm yangenikuta loh
wengine wanakuja kabisa na bahasha imejaa na kuiacha kwa gari au kukukabidhi
kukutoa hofu na kuazima simu yako au kama una gari wanaacha kwa gari lako kabisa,aisee makubwa
 
wanaokulaumu hawajui kuwa vitu hivi hutokea mara nyingi tu watu wanalizwa kwa njia mbali mbali lakini wewe fanya utafiti tu utakutana nao tena siku moja na wataumbuka. Mimi mwaka 1991 wengine humu hawajazaliwa nikiwa nimehitimu Form 4 nilienda mkoana Kagera. wakati narudi nikakutana kwenye meli na vijana wa Iyungo Sec wakiwa wanaenda likizo, wakati huo mwanza Tiketi za Treini kuja Dar Mgogoro.

Basi katika maongezi wale vijana wakaniambia kuwa kuna mwezao ana ticketi ya Dar lakini yeye anaishia Mwanza. Basi ilikuondokana na foleni nikaomba wamweleze ili ninunue ticketi hiyo. Basi kweli nikauziwa ticketi hiyo kama Tshs 1,000/= (Third Class) kama nakumbuka vizuri. Wakanikabidhi, tukaendelea na story hadi Mwanza.

Kufika Mwanza kila mtu akashika njia yake, Mimi nikaenda Railways kuwekewa Namba ya kiti. Nikiwa hapo wakanijia wale washikaji watatu na kunieleza kuwa wamekusanya ticketi zao wakapewe namba (tiketi walikatiwa na shule kama kikundi ), mimi mara moja nikawapa yangu wakaingia ndani. Basi tukakaa hadi kwenye saa nne wakiwa pale pale station.

Kwenye saa nne na nusu hivi akaja jamaa mmoja ambaye naye ni Mwanafunzi wa Iyungo na kuniambia kuwa wale jamaa ni wahuni wameuza tiketi yangu kwa watu wengine, nakumbuka jina la jamaa lilikuwa LUGAITIKA ama jina kama hilo. Basi nikaanza kuwatafuta jamaa wale walipokuwa wameweka mizigo yao HOLAAAAAAAAAAAA!

Nikakubali matokeo nikaanza jitihada nyingine za kupanga foleni nikiwa na imani kuwa kama wakinipa basi nitauza ile ticketi nyingine. Nikabahatika tena kukutana na vijana wa Azania kwani mimi nilisoma hapo. Wakaniorodhesha katika majina kwenda kwa Stesheini master kupewa ticketi. Kwenye saa tano na nusu nikanunua ticket nyingine kama Tsh 950/= hivi.

Jioni saa 12 wakati wa kupanda treini kwenda Dar nikakuta nipangiwa BEHEWA moja na wale jamaa. Kuwauliza wakakosa la kusema. Njia nzima wakawa kama mabubu, baada ya kumweleza POLISI aliyepita hapo juu ya ishu hiyo wakaruka kuwa hawanijui.( ingawa huyo jamaa RUGAITIKA aliwakomalia sana wakaruka kuwa hawanijui). Polisi akasema inakuwa ngumu kuwatia hatiani watu wale, hivyo nikubali matokeo ndicho kizazi cha matapeli

LENGO hasa la kueleza yote haya ni kilichofuata: Mwaka 1997 nikakutana na mmoja wao akiwa Ass. Lect UCLAS, Ukweli aliona aibu sana na ilikuwa ghafla sana mpaka alinisalimia SHIKAMOO wakati tuko umri sawa ama ananizidi. Aliona aibu sana na akanifuata na kunieleza kuwa hakuhusika katika utapeli huo. Ukweli Tsh 1,000/3= 350/= ilimtesa sana jamaa yule. Wa pili naye ni wakili ambaye kila nikikutana naye unaona wazi wazi anakosa amani / raha kwa ile Tsh 350/=, Juzi tulikutana kwenye harusi ambapo dada/jamaa yake kaolewa na mjomba wangu ukweli wakati wa utambulishho aliona aibu sana kwa ile hela ndogo. Wa tatu sijawahi kumwona ingawa siku moja nilikutana na mtu kama yeye Bukoba mjini akageuza direction mara moja na kuelekea alikotoka.

Hivyo kama alivyoshauri mjumbe hapo juu usitumie nguvu sana ila taratibu peleleza utakutana nao, siku moja na unaweza amua cha kufanya kumbuka wao hawatakaa wachukue tahadhari ni wezi tu wewe jipange
 
Back
Top Bottom