Albert Msando akimuweka sawa Mh Zitto Kabwe juu la "CAG na Spika"

Sio kwamba ukiwa mtaalam mbobezi, basi wewe ni mtu usiyekengeuka huyo asad ni binadamu na alichokifanya kwa busara za kawaida si sahihi.
Kwa madaraka aliyonayo na kwa maoni aliyotoa, basi mbona asijiuzuru kama haridhiki na utendaji wa serikali au bunge kutotimiza wajibu wake.
Anasubiri nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kuna makosa na hayashughulikiwi akae kimya? Kwanini hamtaki kukosolewa? Mafanikio yatakuja vipi kila mtu akikaa kimya? Wew unaona sabufa yuko sahihi? CAG nae ni taasisi vile vile
 
Afike tu kwenye kamati bila ya kukosa!
Mimi najuwa wewe na mimi tungesema kama alivyosema CAG tungeitwa pale kwenye kamati tungekosa neno la kujitetea ila CAG anavyovingi sana vyakuwsonesha udhaifu wa bunge kwasababu amepeleka ripoti nyingi lakini kwa udhaifu wa bunge hawajazifanyia kazi ingekuwa ni wewe kamati ingekuuliza tuambie taarifa umezipata wapi na ndugai badala ya kujisahihisha kwenye kiti chake kama wajibu yeye anatumia mamlaka ya bunge kutumia nguvu kumwiita ili kakitaa akamatwe alafu aseme unaona bunge sii dhaifu ndiyo maana tumemkata ndiyo maana CAG akasema ule sii wito Bali ni Amri naye kama raia statii Amri bila shuruti na akifika mbele ya kamati sidhani hakosi maneno machache kuwajibu
 
Hivi kwanini huyu Emoro (Zitto Kabwe) anapenda sana kick za kijinga? Kwani hana washauri au wanampotosha tu huku wakimcheka kujua kwamba anajishusha hadhi ambayo hana?
 
Kweli akili nywele Upara umechemkaaa ukatoa majibu feki!! Kumtishia na pingu ni dalili za kumzuia asiweze kutekeleza kazi zake vizuri,hata kuitwa vile bila staha ni kutaka kumziba mdomo. Ingeandikwa barua ya kumhitaji maelezo lakini siyo kumwita tena kwa maneno yakibabe na kivitisho. Kuitwa kutoa ufafanuzi ni kawaida lkn kuitwa kivitisho haifai hatachembe. Mambo mengi yanafanywa na Rais wakati mwingine anaelekeza bunge lifanyeje na lipitishe sheria gani binafsi sioni jambo lamsingi lililoanzishwa na kushikiliwa na bunge hili zaif. Tukumbuke kutishia watu nao pia ni udhaifu
amri ile ilikuwa kama ni vita na CAG ni adui hapo tu kuitwa ni kawaida sana
 
Sio kwamba ukiwa mtaalam mbobezi, basi wewe ni mtu usiyekengeuka huyo asad ni binadamu na alichokifanya kwa busara za kawaida si sahihi.
Kwa madaraka aliyonayo na kwa maoni aliyotoa, basi mbona asijiuzuru kama haridhiki na utendaji wa serikali au bunge kutotimiza wajibu wake.
Anasubiri nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Assad hajiuzuru ...na bungeni haendi..tuone mtamfanya nini....Membe kakaza msuli wakafyata na sasa Assad...DHAIFU sio kosa la jinai..kwa nini Spika kakalia mafaili badala ya kuyapeleke PAC...viongozi wote wa Afrika ni 'mijizi'wasitake kujifanya malaika..
 
Mh. Zitto, tuwekane sawa kidogo; Suala la CAG na Spika lisiwe la ‘kisiasa’.

Nimesoma barua yako kwa Katibu Mkuu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Pia niliona umesema wewe na wabunge wenzako mmeamua kwenda Mahakamani ili kupata tafsiri kuhusu kinga ya CAG.

Nadhani umeamua kulitumia suala hili ‘kisiasa’ badala ya kusaidia kuliweka sawa kila mmoja alielewe. Hili usilifanye mtaji wa kisiasa.

Wengi tulitaharuki kumsikia Spika akitoa amri kwamba CAG aende akajieleze mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Taharuki ilikuwa kubwa kwa sababu Spika alienda mbali kidogo na kusema ingawaje Bunge halina polisi lakini linaweza kutumia pingu endapo mtu atakaidi amri ya kuitwa.

Kwa upande wangu nadhani hakukuwa na sababu ya ‘tone’ aliyotumia Spika kwenye Press ile kwa kuangalia nafasi ya CAG kama ofisi. Na hapo ndio mwisho wa ‘kosa’ la Spika. Haya mengine unayakuza kwa sababu zako za kisiasa.

Maswali ya kujiuliza hapa ni 1. Je CAG ana kinga ya kutokuhojiwa kwa kauli inayosemekana imedhalilisha Bunge kwa mujibu wa Katiba’?. 2. Je Spika amekosea kupeleka suala hilo kwenye Kamati?

Hili sio suala gumu sana kama utaamua kuliangalia bila ushabiki. Majibu ya maswali yote ni HAPANA. CAG hana kinga na Spika hajakosea kulipeleka suala hilo kwenye Kamati kwa uchunguzi.

Zitto wewe kama Mbunge unajua fika hakuna mtu yeyote ambaye anaruhusiwa kulidharau Bunge au mwenendo wa Bunge au Kamati. Kosa hilo dhidi ya Bunge kwa kiingereza ni ‘contempt’.

Mtu yeyote isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano anaweza kuitwa na Bunge endapo atatenda kosa hilo. Hakuna mwingine mwenye kinga au ruhusa ya kutenda kosa hilo.

Kwa upande wa CAG Katiba haimlindi dhidi ya makosa au mashtaka yeyote isipokuwa tu kutokuingiliwa kwenye utekelezaji wa majukumu yake ya kisheria.

Maswali kwamba 1. Je kauli ya CAG kwamba Bunge ni dhaifu ni utekelezaji wa majukumu yake? na 2. Je kauli hiyo imelidhalilisha Bunge? Yatajibiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya uchunguzi na kumsikiliza CAG na Spika.

Majibu hayo hayawezi kupatikana bila CAG kwenda mbele ya Kamati. Na kwenda huko haimaanishi Katiba imevunjwa.

Nimalizie kwa kusema kwamba Mahakama au chombo kingine chochote ndani au nje ya nchi haiwezi kuzuia Kamati kutekeleza majukumu yake ya kisheria.

Kauli ya CAG kwamba Bunge ni dhaifu haipo kwenye ripoti yake yoyote. Hakuna ‘uchunguzi’ wowote alioufanya akitekeleza wajibu wake na kugundua kwamba Bunge ni dhaifu. Hajawahi kutoa taarifa rasmi kuhusu udhaifu wa Bunge. Angefanya hivyo angekuwa ametekeleza wajibu wake na asingeingiliwa.

Hakuna sababu yoyote ile kupindisha suala hili kwa sababu tu Spika alitumia kauli ya pingu au alitoa taarifa kabla ya wito wa Kamati. Masuala haya mawili hayaondoi ukweli kwamba CAG hana kinga dhidi ya kauli yake aliyoitoa alipohojiwa.

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iachwe ifanye uchunguzi na kuamua kama 1. Kauli hiyo ni udhalilishaji wa Bunge 2. Kauli hiyo ilitolewa wakati CAG anatekeleza majukumu yake.

Alberto Msando.
10.01. 2019
Ameshashiba huyo, naona ameongelea upande mmoja tu unaompa kula. Pole sana Albert Msando!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kubishana na wewe ni kupoteza nguvu ya taifa. Fanya umeshinda nenda kachukue buku saba zako kesho zikufae
Kumbe ulikua kwenye ubishani?Wewe ni mfuasi wa chadema, kujifanya huna upande wwt ni kutaka kuwafanya watu WAPUMBAVU. Hakuna aliye humu atakwambia Mimi niko neutral, wote wana itikadi zao.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Mh. Zitto, tuwekane sawa kidogo; Suala la CAG na Spika lisiwe la ‘kisiasa’.

Nimesoma barua yako kwa Katibu Mkuu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Pia niliona umesema wewe na wabunge wenzako mmeamua kwenda Mahakamani ili kupata tafsiri kuhusu kinga ya CAG.

Nadhani umeamua kulitumia suala hili ‘kisiasa’ badala ya kusaidia kuliweka sawa kila mmoja alielewe. Hili usilifanye mtaji wa kisiasa.

Wengi tulitaharuki kumsikia Spika akitoa amri kwamba CAG aende akajieleze mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Taharuki ilikuwa kubwa kwa sababu Spika alienda mbali kidogo na kusema ingawaje Bunge halina polisi lakini linaweza kutumia pingu endapo mtu atakaidi amri ya kuitwa.

Kwa upande wangu nadhani hakukuwa na sababu ya ‘tone’ aliyotumia Spika kwenye Press ile kwa kuangalia nafasi ya CAG kama ofisi. Na hapo ndio mwisho wa ‘kosa’ la Spika. Haya mengine unayakuza kwa sababu zako za kisiasa.

Maswali ya kujiuliza hapa ni 1. Je CAG ana kinga ya kutokuhojiwa kwa kauli inayosemekana imedhalilisha Bunge kwa mujibu wa Katiba’?. 2. Je Spika amekosea kupeleka suala hilo kwenye Kamati?

Hili sio suala gumu sana kama utaamua kuliangalia bila ushabiki. Majibu ya maswali yote ni HAPANA. CAG hana kinga na Spika hajakosea kulipeleka suala hilo kwenye Kamati kwa uchunguzi.

Zitto wewe kama Mbunge unajua fika hakuna mtu yeyote ambaye anaruhusiwa kulidharau Bunge au mwenendo wa Bunge au Kamati. Kosa hilo dhidi ya Bunge kwa kiingereza ni ‘contempt’.

Mtu yeyote isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano anaweza kuitwa na Bunge endapo atatenda kosa hilo. Hakuna mwingine mwenye kinga au ruhusa ya kutenda kosa hilo.

Kwa upande wa CAG Katiba haimlindi dhidi ya makosa au mashtaka yeyote isipokuwa tu kutokuingiliwa kwenye utekelezaji wa majukumu yake ya kisheria.

Maswali kwamba 1. Je kauli ya CAG kwamba Bunge ni dhaifu ni utekelezaji wa majukumu yake? na 2. Je kauli hiyo imelidhalilisha Bunge? Yatajibiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya uchunguzi na kumsikiliza CAG na Spika.

Majibu hayo hayawezi kupatikana bila CAG kwenda mbele ya Kamati. Na kwenda huko haimaanishi Katiba imevunjwa.

Nimalizie kwa kusema kwamba Mahakama au chombo kingine chochote ndani au nje ya nchi haiwezi kuzuia Kamati kutekeleza majukumu yake ya kisheria.

Kauli ya CAG kwamba Bunge ni dhaifu haipo kwenye ripoti yake yoyote. Hakuna ‘uchunguzi’ wowote alioufanya akitekeleza wajibu wake na kugundua kwamba Bunge ni dhaifu. Hajawahi kutoa taarifa rasmi kuhusu udhaifu wa Bunge. Angefanya hivyo angekuwa ametekeleza wajibu wake na asingeingiliwa.

Hakuna sababu yoyote ile kupindisha suala hili kwa sababu tu Spika alitumia kauli ya pingu au alitoa taarifa kabla ya wito wa Kamati. Masuala haya mawili hayaondoi ukweli kwamba CAG hana kinga dhidi ya kauli yake aliyoitoa alipohojiwa.

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iachwe ifanye uchunguzi na kuamua kama 1. Kauli hiyo ni udhalilishaji wa Bunge 2. Kauli hiyo ilitolewa wakati CAG anatekeleza majukumu yake.

Alberto Msando.
10.01. 2019

Hakika Alberto ameeleza kitu ambacho ni sahihi kabisa. Nina hakika Zitto na baadhi ya wanaolikomalia hili jambo wanaelewa ila wanajaribu kulitumia kwa namna yenye manufaa kwao kama wanasiasa. Pamoja na kwamba Ndugai alivuka mipaka na kutumia lugha ambayo haikutarajiwa kutumiwa na mtu kama yeye dhidi ya CAG lkn pia haindoi haki ya spika kutofurahishwa na kauli ya CAG kuwa mhimili unaoongozwa na spika ni dhaifu (tena ktk vyombo vya habari vya nje ya nchi).
Na kitendo cha Zitto kuanza kulikuza na kulisambaza nje ya mipaka (akilalamika na kushitaki akiigiza kana kwamba anamtetea CAG ) hata kabla ya CAG kuhojiwa na kujua mwenendo wa tukio lenyewe nu UPUUZI MTUPU. Zitto angalau hata angesubiri kuona kitakachotokea baada ya CAG kukutana na kamati ya bunge na kujua kilichoamuliwa kabla ya kuanza kusambaza barua za mashitaka na malalamiko nje ya nchi. Halafu anataka tumwamini kuwa anastahili kuwa Rais wa nchi huru, kakosea!
 
Sio kwamba ukiwa mtaalam mbobezi, basi wewe ni mtu usiyekengeuka huyo asad ni binadamu na alichokifanya kwa busara za kawaida si sahihi.
Kwa madaraka aliyonayo na kwa maoni aliyotoa, basi mbona asijiuzuru kama haridhiki na utendaji wa serikali au bunge kutotimiza wajibu wake.
Anasubiri nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Matamanio yenu ni kuona profesa anajiuzuru iliKwani haiwezekani kwamba amesema Bunge ni dhaifu kama njia nyingine ya kulikumbusha liache huo udhaifu?
 
Hakika Alberto ameeleza kitu ambacho ni sahihi kabisa. Nina hakika Zitto na baadhi ya wanaolikomalia hili jambo wanaelewa ila wanajaribu kulitumia kwa namna yenye manufaa kwao kama wanasiasa. Pamoja na kwamba Ndugai alivuka mipaka na kutumia lugha ambayo haikutarajiwa kutumiwa na mtu kama yeye dhidi ya CAG lkn pia haindoi haki ya spika kutofurahishwa na kauli ya CAG kuwa mhimili unaoongozwa na spika ni dhaifu (tena ktk vyombo vya habari vya nje ya nchi).
Na kitendo cha Zitto kuanza kulikuza na kulisambaza nje ya mipaka (akilalamika na kushitaki akiigiza kana kwamba anamtetea CAG ) hata kabla ya CAG kuhojiwa na kujua mwenendo wa tukio lenyewe nu UPUUZI MTUPU. Zitto angalau hata angesubiri kuona kitakachotokea baada ya CAG kukutana na kamati ya bunge na kujua kilichoamuliwa kabla ya kuanza kusambaza barua za mashitaka na malalamiko nje ya nchi. Halafu anataka tumwamini kuwa anastahili kuwa Rais wa nchi huru, kakosea!
Kuliacha hili la spika liende hivi hivi ni kuiingiza nchi katika shimo ambalo haitakuwa rahisi kulondoa tena. Usichoelewa mi kwamba sasa hivi nchi iko katika crisis unapozungumzia fedha za nchi, matumizi yake ni ya hovyo haijawahi kutokea hata kama mnashangilia bombadier. Tukiruhusu tu kila anayesema kuwa Bunge ni dhaifu aitwe kuhojiwa tutakuwa tunapanua goli la mali ya umma kutumika isivyo huku bunge la ndugai likiendelea na huo udhaifu. jambo la msingi hapa tukubaliane tu kwamba kama udhaifu halijawahi kuwa kosa la jinai wala kashfa, ndugai awe mtulivu na badala yake aliondoe bunge katika hilo la udhaifu. Achana na akina Msando ambao wanatafuta kila fursa inayoweza kupatikana kwa ajili ya matumbo yao wala sio kwa ajili ya nchi!
 
Nimefurahi tu umehoji maswali ya msingi ambayo hata mimi nilijiuluza na kila mwenye kufikiri anapaswa kujiuliza hasa matumizi ya neno dhaifu.

Ukweli ni kwamba, hata kumuita mtu dhaifu sio kosa la jinai na si tusi hata kwa sheria za nchi yetu na Bunge kupitia hiyo kamati yake halina mamlaka ya kumuhukumu mtu kwa kuliita dhaifu unless mwanasheria Ana Henga hakusema ukweli kuhusu matumizi ya hilo neno kisheria(nimeweka link ya alichokisema hapo chini).

Nilitaraji wewe kama mwanasheria utuonyesha ni kwa mujibu wa sheria gani ya nchi yetu neno dhaifu ni tusi,kashifa au ni dharau pale linapotumika dhidi ya mtu mwingine au dhidi ya taasi fulani.

Ni imani yangu, tafsiri ya neno "dhaifu" ndio inapaswa kuwa msingi wa hili jambo na neno hilo likioonekane si kosa,basi mjadala mzima unakuwa umeishia hapo na hakuna hata haja ya kuhangaika na Ibara za katiba zinasema nini.

Ana Henga: Neno "dhaifu" sio tusi na wala si kosa la jinai - JamiiForums
Suala hapa ni general situation ya alichokimaanisha CAG juu ya Bunge. Tatizo letu tuliowengi humu tunabwabwaja tu coz labda halituhusu directly.

Ndugai ndio aloshika kikali, hivyo, muacheni apambane maana yeye ndo anajua madhara ya Kauli hiyo kwa Taasisi yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom