Akipita mzungu karibu na uzio wa Ikulu hana kosa, ila apite mtu mweusi ni kosa na mateso juu

nampendayeye

Senior Member
Mar 24, 2015
125
71
Hiyo nimeishuhudia asubuhi ya leo. Mzungu kapita karibu kabisa na hawa maaskari wanaolinda Ikulu tena karibu kabisa na uzio eti anafanya mazoezi na wala hakuguswa wala kuulizwa. Wakati huo watu wengi weusi (naamini ni Watanzania) Bahati mbaya akikosea akapita upande huo huo atapewa adhabu kali kweli. Nimejiuliza maswali mawili.

1. Je! Watanzania tunabaguana? Na kama tunafanya hivyo sisi kwa sisi, Je! Tuendelee kuwalaumu wazungu kwa kutubagua?

2. Je hawa maafisa wetu wameambiwa wazungu wasiguswe waguswe wabongo tu? Au lugha ngeni inawasumbua? Tendeni haki kwa wote bila kuangalia rangi za watu!!!!.
 
Watanzania tunawaona wazungu ni miungu watu. Mfano mtu mweusi ukienda kushtaki polisi unazungushwa, lakini mzungu akienda kushtaki mara moja wanafuatilia. Hata pale airport, mimi sijawahi kuona mzungu anakaguliwa.
 
Mleta mada biashara ya utumwa ilituaribu sana kisaikolojia.
Bado Kuna wapumbavu wa nawaona watu weupe kama wazungu na wahindi, warabu, wachina kama miungu.
 
Aisayee... hapo kuna DHULUMA na UONEVU !! yaani wakikubamba wana kutesa na kukuadhibu bure..... just by passing far from yhe fence !!Very bad!! tena ni uhuni wa maaskari njaa!!
 
Huu ni uongo wa kiwango cha juu sana. Hakuna mtu aliyewahi kuzuiliwa kupita karibu na ukuta wa Ikulu. Mleta mada wewe wa wapi!?
 
Hiyo nimeishuhudia asubuhi ya leo. Mzungu kapita karibu kabisa na hawa maaskari wanaolinda Ikulu tena karibu kabisa na uzio eti anafanya mazoezi na wala hakuguswa wala kuulizwa. Wakati huo watu wengi weusi (naamini ni Watanzania) Bahati mbaya akikosea akapita upande huo huo atapewa adhabu kali kweli. Nimejiuliza maswali mawili.

1. Je! Watanzania tunabaguana? Na kama tunafanya hivyo sisi kwa sisi, Je! Tuendelee kuwalaumu wazungu kwa kutubagua?

2. Je hawa maafisa wetu wameambiwa wazungu wasiguswe waguswe wabongo tu? Au lugha ngeni inawasumbua? Tendeni haki kwa wote bila kuangalia rangi za watu!!!!.

wewe hujui kuwa mzungu anafananishwa na mungu? ili uamini hilo katika neno mzungu jaribu kuondoa herufi " z " je itabaki neno gani?
 
Wakati anapita mkuu wa hiyo kaya alikuwemo au yuko marekani?

Nauliza tu
 
Nazidi kujiuliza. Assume mimi ni mgeni Dar. Nimekosea nikapita pale. Wamenisimamisha nimetii nikasimama. Nikaomba samahani kwani nilikuwa sijui. Kwa nini wanitese? Mimi naona wanafanya makusudi ili tuichukie nchi yetu. Kama si makusudi kwa nini hata kibao cha katazo la kupita pale hamna??? Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu kabisa. Umenikamata napita bila kujua nimeomba msamaha, nikague kama una hofu na mimi alafu niache niende zangu siyo kunitesa.!!
 
Hiyo nimeishuhudia asubuhi ya leo. Mzungu kapita karibu kabisa na hawa maaskari wanaolinda Ikulu tena karibu kabisa na uzio eti anafanya mazoezi na wala hakuguswa wala kuulizwa. Wakati huo watu wengi weusi (naamini ni Watanzania) Bahati mbaya akikosea akapita upande huo huo atapewa adhabu kali kweli. Nimejiuliza maswali mawili.

1. Je! Watanzania tunabaguana? Na kama tunafanya hivyo sisi kwa sisi, Je! Tuendelee kuwalaumu wazungu kwa kutubagua?

2. Je hawa maafisa wetu wameambiwa wazungu wasiguswe waguswe wabongo tu? Au lugha ngeni inawasumbua? Tendeni haki kwa wote bila kuangalia rangi za watu!!!!.

Nilivyoona title tu nimecheka kwanza, mie mzungu koko
 
!
!
kuna tofauti kati ya kufanana na kuwa sawa
 
Watasumbuje wazungu wakati Muheshimiwa mwenyewe anachojua ni kwenda kwao kuomba na kusema Hawa wakubwa wana hela sana hawa nikuomba tu unapewa
 
Back
Top Bottom