Ajira zote za serikali zigawiwe kuanzia ngazi ya kata?

kitene

New Member
Sep 18, 2021
1
2
Nitoe maoni bila kuwa na uhakika wa kufanyiwa kazi. Inajulikana kuwa kila mwaka nchi yetu inazalisha vijana wazuri wanao weza kutumikia umma. Wahitimu hawa hotokea pande zote, mijini na vijijini.Kuhusu nafasi za ajira kidogo zinazo patikana, basi zigawiwe kuanzia ngazi ya Kata zote za tanzania ili dhamira ya kuelimisha watoto wa tanzania izae matunda kwa wote.
 
Ajira ni changamoto sana,nà zikitolewa,baadhi huambatana na sifa ambazo si za msingi,mfano;kuwa na sifa ya ukada.Wengine sisi hatujihusishi na vyama vya siasa,inakua changamoto.
 
Hiyo ngumu sana, Kila mwaka wahitimu wasiopungua 100,000 wa cert Hadi digrii humwagwa kitaa na wanaohitajika ni pungufu ya 20,000 Kwa kada zote.

Kwa Leo Kila kitongoji kina jobless mwenye digree, Kijijini kwetu kina jobless Kila familia mwenye digree za education, sociology, law na engineering.

Wadangaji, barmaid, boda, makonda , wapiga debe, saidia fundi, wachoma chips, madalali na wasusi Wana digrii.

Kuanzia mwakani na waganga wa jadi watakuwa na dgr
 
Nitoe maoni bila kuwa na uhakika wa kufanyiwa kazi. Inajulikana kuwa kila mwaka nchi yetu inazalisha vijana wazuri wanao weza kutumikia umma. Wahitimu hawa hotokea pande zote, mijini na vijijini.Kuhusu nafasi za ajira kidogo zinazo patikana, basi zigawiwe kuanzia ngazi ya Kata zote za tanzania ili dhamira ya kuelimisha watoto wa tanzania izae matunda kwa wote.
Ajira ya pilot, ajira ya daktari, Engineer. Unataka kata? Are You serious? Utumishi wanafanyisha interview kwa weledi mkubwa sana kupitia secretariat ya Ajira. Hata mtoto wa maskini mwenye uwezo anapata ajira sehemu yoyote Tanzania hii. Watu washindanishwe mwenye uwezo aajiriwe.

Hii si nchi ya kijamaa. Sera zetu ni jitihada zako ndo zitakuokoa. Na ndo itakayo chochea maendeleo ya nchi kwani watu watakuwa wabunifu zaidi

Ukipunguza competition unapunguza ubunifu na moja kwa moja unaathiri maendeleo
 
Nitoe maoni bila kuwa na uhakika wa kufanyiwa kazi. Inajulikana kuwa kila mwaka nchi yetu inazalisha vijana wazuri wanao weza kutumikia umma. Wahitimu hawa hotokea pande zote, mijini na vijijini.Kuhusu nafasi za ajira kidogo zinazo patikana, basi zigawiwe kuanzia ngazi ya Kata zote za tanzania ili dhamira ya kuelimisha watoto wa tanzania izae matunda kwa wote.
Utoto na upuuzi
 
Haya mawazo tuyapinge, ajira kwenye utumishi wa umma zibaki kuwa za ushindani na zisizo na upendeleo. Tukianza haya mawazo, itaenda kwamba sasa zigawiwe kifamilia(royal families), kikabila, kichama nk

Kibaya zaidi hata zikigwiwa kwa kwa familia fulanifulani, bado hazitatosha baada ya muda fulani. Hivyo, the most priviollage ndo watakaopata pekee hata ww hutapata.
 
Back
Top Bottom