Ajira Serikalini mpaka mwaka 2017 mwezi wa pili

Status
Not open for further replies.
Ebu fikirieni nje ya box ; Mimi nimeacha kazi na Plan B kufanya kazi zangu binafsi ; staki kuajiriwa Mimi nataka kujiajiri

Utaweza kuamka muda unaotaka ! Utaweza kufanya mambo yako bila limitation yoyote

Kikubwa uvumilivu ; Haihitaji Presha hiii
 
YAH: KUKANUSHA HABARI ILIYOSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII IKIMNUKUU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA) MHESHIMIWA ANGELLAH J. KAIRUKI (MB), KUWA SERIKALI ITAANZA KUTOA AJIRA, KUPANDISHA VYEO NA KULIPA STAHIKI MBALIMBALI ZA WATUMISHI WA UMMA MWEZI FEBRUARI, 2017.
1. Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu Waziri wa Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza kutoa ajira, kupandisha Vyeo na kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma mwezi Februari, 2017. Chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Jamii Forum kupitia mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JF-Expert Member) na baadaye kusambazwa katika mitandao mingine.
2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inapenda kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha Umma. Hivyo watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.
3. Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha
2016/17. Malipo ya stahili za watumishi wa umma yatafanywa na Serikali kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.
4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa Umma, hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka husika.
5. Serikali kupitia taarifa hii inawaasa wananchi kuacha tabia ya kusambaza habari za uongo au zisizothibitishwa dhidi yake. Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu shughuli za Serikali.
Imetolewa na:
Florence Temba
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
24 Oktoba, 2016
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom