Habari waungwana,
Leo wakati nasoma gazeti, nimeona habari ambayo nimehisi itawapendeza na inaweza kuwa na manufaa kwenu nikaona niwaletee.
=====
Takriban Zaidi ya wahitimu 5,000 kutoka vyuo vikuu tofauti nchini hapa, wanatarajiwa kuajiriwa na kampuni za Kichina hapa nchini na Uchina katika fani mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na makamu mkuu wa chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Profesa Florence Luoga, ambapo amejulisha kuwa, Chuo hicho (UDSM) (Taaluma) kwa kushirikiana na taasisi ya China ya Confucius watafanya maonesho kwa pamoja na vijana watakaojitokeza ili kufanya uchambuzi wa kuwabaini watakaoajiriwa.
Maonesho hayo yatafanyika June 18 na 19 mwaka huu kwa kushirikiana na kampuni 100 za kichina zinazofanya shughuli zake nchini hapa.
Aidha, mtaalamu wa lugha ya Kiswahiili UDSM , Profesa Aidin Mtembei, amewataka wahitimu wote kuhudhulia maonesho hayo bila kujali chuo aliposoma, huku wakifika na nakala za wasifu wao (CV), picha, na vyeti vya taaluma zao walizosomea tayari kwa kurahisisha zoezi la mchujo.
Chanzo: Mwananchi