Ajali ya Precision Air: Wanasheria wa LEAT wameonesha njia, TLS wamelala kama pono!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
1) NAWASHUKURU SANA Wanasheria wa LEAT (Lawyers' Environmental Action Team) kwa hii Taarifa yao kwa Umma (ya tarehe 07.11.2022) iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa LEAT, Dr. Rugemeleza A. K. Nshala.

Hii ni kufuatia Ajali ya Ndege ya Precision Air iliyotumbukia majini jana asubuhi huko Bukoba. Watu 19 wanaripotiwa kufa na 26 kuokolewa (ingawa Ndege inaripotiwa kuwa ilikuwa na Watu 43)!

2) Mimi BJC naunga mkono Taarifa hii.

3) Ingependeza zaidi iwapo Taasisi mbalimbali Nchini (zenye ubavu, uthubutu na/au kujiheshimu!) nazo zingetoa Taarifa Rasmi kama hii kulaani Uzembe uliofanyika na kuisukuma "Serikali yetu sikivu" (bila kutumia nguvu!) walau ione aibu na kuchukua hatua zilizopendekezwa na LEAT na zingine stahiki.

Ingependeza hata "Hashtags" zikazagaa Mitandaoni ili hata Wananchi wa Kawaida washiriki kupaza sauti Mitandaoni.

4) Ni wazi Wanasheria wa LEAT wamekuwa waungwana sana kumung'unyamung'unya maneno lakini ni wazi kwamba kuna both:

a) Criminal Negligence!
b) Criminal Liability!

Mimi naongea kama "Bush Lawyer", lakini Wanasheria wanaweza kutusaidia kuliweka vizuri zaidi.

5) Hakika kuna Precedents nyingi Duniani. Hili liwekwe wazi kabisa ili wawajibishwe Watu kuanzia "Matawi ya Juu" kabisa.

6) Wanasheria wana Jukumu la Kufungua Mashtaka:

a) Kuwashtaki wanaostahili kushtakiwa.
b) Kudai Fidia kubwa sana kwa niaba ya, na kwa ajili ya, Waliokufa, Waliojeruhiwa (physically and emotionally), Familia zao na Watanzania kwa ujumla (na hasa Wakazi wa Bukoba na Mwanza)!

7) Kama Mahakama zetu zinazengua zitumike ama Mahakama ya Afrika Mashariki ama Mahakama za Kimataifa!

8) Nachoongelea sio "Uchochezi", bali ni Sehemu ya:

a) Utawala Bora.
b) Utawala wa Sheria. Tukumbuke Sheria ni msumeno, mbele unga nyuma unga!
c) Haki za Raia Kikatiba.
d) Haki za Binadamu.
e) Demokrasia.
f) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

9) Haya mambo ya kuchekeanachekeana na kugeuza Wananchi wote Mazuzu yakomeshwe kwa Msukumo wa Umma wenyewe! Ndio maana nimependekeza a Class Action Lawsuit!

10) Tusikubali kuendelea na huu "Mfumo wa Kulindana na Funika Kombe Mwanaharamu Apite"!!

11) Kwa kweli nimemkumbuka sana Mchungaji Christopher Mtikila...!

12) Nami naungana na Watanzania wenzangu katika Msiba huu mzito! Nawapa pole Wafiwa na Watanzania wote! Nawapa pole Majeruhi wote! Nawapa pole Precision Air!

13) TUNAMUOMBA MUNGU awapumzishe kwa amani Marehemu wote! Awaponye haraka wote Waliojeruhiwa (kimwili na kisaikolojia)!

14) TUNAMUOMBA MUNGU awafariji Wafiwa na wote walioathirika kimwili na kisaikolojia, ikiwa ni pamoja na Wananchi wa Kawaida walioshiriki Kishujaa katika Pilikapilika za Uokoaji, Majeruhi, Ndugu Jamaa na Marafiki!

15) Sitashangaa kuona, kama kawa, "Watetezi wa Chochote" wanaingia kazini haraka kujaribu kuzuia na kuhujumu any reasonable and needful Action! AIBU TUPU!

16) MUNGU IBARIKI TANZANIA!

BJC. DSM. 07.11.2022. 2130hrs.

NYONGEZA!
1) Natambua kwamba hatujui mambo mengi kuhusu Ajali hii. Mfano, Wananchi hatujui ni nini hasa kilichosababisha Ajali itokee. Hili tunaweza kulijua baada ya Wataalam Wabobezi wa Uchunguzi wa Ajali za Ndege kukamilisha Uchunguzi Huru na kutoa Ripoti Huru. Tuombee isifanywe Siri!

2) Bahati, baadhi yetu tunajua mengi kupitia Kipindi Maarufu Duniani kiitwacho "Air Crash Investigation". Watanzania tumeamka, hata kama Wataalam husika wanatuzengua!

3) Lakini ni wazi kabisa kwamba Serikali imeonyesha Udhaifu mkubwa sana katika Mfumo wa Uokoaji (au Kitengo cha Uokoaji), licha ya Ajali kadhaa zilizowahi kutokea Nchini (na kuua Watu wengi). Hili limeongelewa na LEAT na pia limeshuhudiwa jana na Nchi nzima na Dunia nzima. Aibu Kubwa ya Kitaifa! Hakika hii ni moja ya sababu za Hasira kubwa ya Wananchi.
--
 
Hii nchi litatengenezwa tukio, kufunika hii ajali ya ndege. Na kila kitu kitasahaulika.

Si unakumbuka zile hela za tetemeko huko huko Kagera?
 
Hii nchi litatengenezwa tukio, kufunika hii ajali ya ndege. Na kila kitu kitasahaulika.

Si unakumbuka zile hela za tetemeko huko huko Kagera?
za tetemeke CHADEMA walisema wanazitumia kujenga madarasa na zisihojiwe.
 
Back
Top Bottom