Ajali Ubungo Riverside

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Sijaipata vema, ila ni ajali mbaya, watu watatu wamekufamo na wengine bado wamekwama mu-gari.
Source: East Africa Radio
 
Ninasikitika kuawaarifu kua kuna ajali mbaya imetokea Ubongo Riverside ambapo gari aina ya lori limeacha njia na kugonga watu.

Kwa uchache inasemekana maiti 20 zimeokotwa eneo la ajali.

Habari zaidi zitawajia hivi punde
 
Nimepita hapo sasa hivi, inatisha. Nilivyoona ni kama lori la mafuta lilikuwa linatokea Ubungo, limepanda kingo za katikati ya barabara na kugonga magari kadhaa yaliyokuwa kwenye foleni upande wa pili wa bara. Sikuweza kuhesabu watu waliokufa lakini kwa haraka nimeona kama miili miwili hivi ikiwa imefunikwa barabarani
 
Mola awalaze pahala panapostahikhi maiti wote wa ajali hiyo .

Poleni sana
 
Mhhhhh!!!!!!!!!!hiii sasa balaaaaa,kila kukicha ajali ajali ajali,mungu awalaze mahali pema.
 
Kuna taarifa kwamba kuna ajali imetokea river-side pale ambapo lori limepoteza mwelekeo na kugonga magari mengine manne na kisha kudondokea daladala lilojaa abiria..watu wamefariki huku wengine wakikatika vichwa...harakati za kuwanasua zinaendelea
source:Clouds fm
 
Hizi ajali za barabarani sasa jamani! Magari mabovu yanaruhusiwaje kutembea barabarani? Na madereva wasiokuwa na leseni wamejaa tele mitaani!
 
Poleni watanzania wenzetu mliopoteza ndugu zenu na kwa wale waliopona kifo na kuumia nawatakia nafuu,Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu.amina.
 
kuna gari kubwa la tera limeangukia daldala karibu 3, na kuna watu wamekandamizwa, roli hilo lilishindwa kukata kona............ waliopo jirani watujuvye kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom