Nikufikiri nje ya box tu ndicho kitakachoepusha ajali. Nitatoa sababu 3 tu za muhimu:Hivi karibuni na hata siku za nyuma tumeshuhudia malumbano kati ya wamiliki wa mabasi ya abiria kwa upande mmoja na serikali (Polisi, Sumatra) kwa upande mwingine juu ya ulazima wa kufunga vidhibiti mwendo (Speed Governor) kwenye mabasi.
Wamiliki wa mabasi wanasema speed governor hazijasaidia kupunguza ajali za barabarani. Na zaidi wanaona msisitizo wa serikali wa kufunga speed governor unamsukumo wa kibiashara zaidi kuliko kupunguza ajali.
Je ni kweli speed governor hazisaidii kupunguza ajali? Kama hazisaidii, je nini kifanyike kupunguza ajali za barabarani?
------------
Ndg wanabodi Heshima kwenu..
Bila shaka vifo vingi vinavyotokea kwa kiasi kikubwa hivi sasa ni kutokana na ajali za magari barabarani hasa Mabasi..
Tunaipongeza serikali kwa hatua mbalimbali ambazo imekua ikichukua ili kukabiliana na Changamoto hii kubwa japo kwa kiasi kikubwa bado ajali ni janga kwa nchi yetu..
Kwa kua akili ni nywele na kila mtu anazake,nami pia naomba kuwashirikisha fikra nilizonazo kama ifuatavyo..
1)SERIKALI IANZISHE VYUO MAALUMU KWA AJILI YA MAFUNZO YA UDEREVA WA MAGARI YA ABIRIA PEKEE..
Serikali na sio vyuo binafsi vianzishe vyuo maalumu kwa ajili ya Madereva wa Abiria pekee...
Hii itasaidia kupunguza madereva wa Mtaani wanaopiga dayworker kisha baada ya Muda wanaendesha mabasi ya Abiria.
Nimesema vyuo maalumu na wala si VETA wala vyuo binafsi Kutokana na sababu kua sasa ,VETA na vyuo vingine binafsi vimekosa credibility yaani mtu yeyote anaweza pata leseni hata kwa magumashi ilimradi awe na pesa..
Lakini pia ili mtu A-qualify kusomea udereva wa magari ya abiria awe amesoma mpaka kidato cha nne na awe amefaulu ili kupata watu makini wanaojielewa na si kuokoteleza hadi STD VII kama ilivyo sasa.
2)KILA BASI LISAFIRI NA ASKARI WA BARABARANI ANGALAU MMOJA:
Sio lazima askari aanze mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari...kunaweza kua na utaratibu wa askari maalumu wa barabarani kupokezana kila wilaya ambako gari hiyo itapita..hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kum-control driver hivyo kufata sheria zote za barabarani kama inavyopaswa.
3)MISHAHARA YA MADEREVA IBORESHWE
Hii itasaidia watu wengi kuwa motivated na kupenda kazi ya udereva ma mabasi hivyo kupata watu wengi wanaoqualify,hii inamana mtu aiendeshe gari kwa kua ameona ndo sehemu ya kutokea bali udereva uwe tamanio la mtu mwenyewe.
Wapewe pesa ya kutosha na posho juu ili kumfanya Dereva afurahie kazi yake na kupunguza msongo wa mawazo..
4)MISHAHARA YA ASKARI WA BARABARANI IBORESHWE
Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa askari hawa kutoshawishika kuchukua pesa ndogondogo wanazopewa njiani hivyo kupelekea kufanya kazi zao kwa uaminifu na umakini wa hali ya Juu.
5)ASKARI WA BARABARANI WAPUNGUZWE
Wingi wa Askari wa barabarani waliopo hivi sasa haimanishi ni kuboresha utendaji na udhibiti wa ajali barabarani..unaweza kua na askari wachache na wakafanya kazi nzuri yenye zaidi,iwapo madereva hawataokotwa mitaani,wakalipwa pesa vizuri na askari nao wakalipwa pesa vizuri hakika makosa barabarani yatapungua kwa kiasi kikubwa..hii ina apply kwa madereva wa magari yote barabarani...
Iwapo adadi ya askari barabarani itakua ndogo itakua rahisi kuwa hudumia financially na kwa pesa nzuri zaidi.
Nashauri askari barabarani walipwe kuanzia milioni 1 kwa Mwezi.
Utitiri wa askari barabarani haimanishi ndio uimarikaji wa utendaji kazi.
6)UKAGUZI WA MABASI YA ABIRIA KABLA YA SAFARI UIMARISHWE..
Ukaguzi wa maramojamoja unaofanywa na askari wa barabarani kwa sasa unamapungufu makubwa..
Pawe na kikosi kazi maalumu ambacho kazi yake ni kukagua mabasi yote ya abiria siku moja kabla ya safari na gari hiyo iwe na alama kua imekidhi vigezo vya kusafirisha abiria kesho yake..Hii itasaidia hasa kupunguza ajali zitokazazo na uchovu wa magari yenyewe hasa yale yanayounga safari bila kupumzishwa..
ikiwa na pamoja na kumpima dereva kabla ya kuanza safari kama hatumii madawa ya kulevya wala kilevi chochote..
7)SUMATRA WASIFANYE KAZI KWA MATUKIO PEKEE
SUMTRA Wasisubiri kupaza sauti katika kuwaambia umma kua nauli zitapanda kutokana na bei za mafuta kuongezeka,na wasisubiri mpaka matatizo yatokee ndo wajitokeze kwa waandishi wa habari kama wanavyofanya hivi sasa.SUMATRA Ifanye kazi yake ipasanyo na isifanye kazi kisiasa...
Nimesema ni mawazo tu sio msaafu wala Biblia unaweza kosoa au kuboresha kwa Mtazamo chanya ili kutoa mawazo sahihi kisha yafanyiwe kazi na mamlaka husika.
Karibuni kwa Mawazo chanya pia.
-----
Huu ndo ukweli pekee niliowai kukutana nao kuhusu ajari nchini. Asante kwa kuhalalisha nilichokuwa naamin siku zote ingawa sijafika ulaya. Umetenga tafiti zenye kachumbari ya kisiasa na utafiti halisia. Nitaongeza nyama kwenye hoja hii nikitulia.Mchango wangu wa kupunguza ajali ni kujifunza kwa wenzetu. Mimi nimebahataika kusafiri nchi mbali mbali za nje kusini mwa bara letu la Afrika na Uingereza, Uholanzi na Marekani. Kwa wenzetu hawa wana magari mengi kuliko sisi ingawa pia barabara zao ni bora zaidi kutokana na uchumi wao. Lakini wamepunguza sana ajali kwa kutenganisha barabara kwa kuwa waligundua kuwa asilimia kubwa za ajali zinatokana na ku-OVERTAKE (kulipita gari lililoko mbele yako kwa spidi kubwa, kabla ya kurudi upande unatakiwa uwe unakutanan na gari lingine linatoka upande wa pili. Barabara kuu za wenzetu (Highways) zote zimetenganishwa, magari yanakwenda upande moja tu hukutani na gari linalotoka upande wa pili. HILI PEKEE LIMEPUNGUZA AJALI KWA ZAIDI YA ASILIMIA 65. Ni kweli kuwa na barabara zilizotengwa ni GHARAMA KUBWA lakini tukianza kidogo-kidogo tutajikuta tuna Highway za kweli za upande moja tu. Hapo ndipo tutaweka SPEED CAMERA barabarani na alama zinazoonyesha kuwa mbele yako kuna Camera angalia mwendo wako, ukizidisha speed iliyowekwa UTAIKUTA FAINI NYUMBANI KWAKO WALA HUHITAJI KUWA NA ASKARI WENGI BARABARANI. Huo ndio ustaarabu wa wenzetu. Sisi, ninaona tunawatesa sana askari wetu ambao ni wachache kudhibiti mwendo kila siku barabarani. Huo ndiyo mchango wangu kwa leo.
uzunguni tunakoishi sisi amini usiamini nina four years sijaona wala kusikia ajali popote yani kiufupi hakuna ajali za kiboya boya, magari yanaogopa watu jamaa akiona unaonesha nia ya kuvuka barabara anasimama mbali kabisa ili uvuke bila hofu , huku uzunguni ukisababisha ajali ikathibitika wanachukua leseni yako huendeshi tena gari maisha kama umeua na kama umejeruhi jamaa wanatunza leseni yako miaka mitano hadi kumi na unamlipa uliemgonga na mkweche wako pesa ndefu si madafu , magari yote barabarani ni yaliyo katika hali nzuri na trafiki wako serious na roho za watu wanazithamini kama wanavyothamini roho zao na roho za familia zao wake zao na watoto wao na hawacheki na kima, hawaangalii sura na hawachukui rushwa , ajali nyingi za bongo ni miongoni mwa sifa za nchi masikini iliyojaa barabara mbovu , magari mabovu , trafiki wengi wasiojali thamani za roho za watu masikini na wajinga lukuki wanaoendesha kwa kasi magari wasiyoyamiliki , magari wanayoendesha kwa sifa, ushamba na ulimbukeni! Trafiki huku wana kazi kubwa kusaka madereva walevi wakikudaka umelewa unaendesha hakuna mjadala wala rushwa leseni inaenda kabatini na adhabu za kulipa faini na kutoendesha gari zinakuhusu kulingana na amount ya alcohol ni kuanzia mwaka mmoja hadi mitano hushiki usukani sheria inakata hata baba yako awe mfalme wa Uingereza unakwenda na maji, umaskini shida sana! Tukiendelea ajali zitaisha! Wahusika muonesheni waziri hii comment, we waste time to discuss ajali wajinga na walevi kibao wamejaa road nyuma ya usukani!
Ok baadhi uko ushauri wako unafaa ,ila nyongeza na kusisitiza leseni za udreva ziwe recorded ikitokea dreva anasababisha ajali kwa uzembe wake Mara mbili afutiwe leseni yake na asiluhusiwe kupata leseni nyingine ,2-ajari zilizo jeruhi au kuua Sheria iwe kali zaidi na viwango kuhusu faini iongezeke na Sheria itamke majeruhi alipwe fidia kuanzia 6 mil-12mil na bima isihuke kulipa kwa kuwa Kuna usumbufu mwingi na wenye magali huwa na viburi kwa kuamini bima itadaiwa ,walipe wao na gali litaifishwe kabisa kukomesha jeuri za wamiliki baadhi wasio na utu hasa pindi gali zao zikisababisha ajari ,
Sent using Jamii Forums mobile app