Ajali MV Nyerere: Waziri Mkuu amsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa TEMESA kupisha uchunguzi. Aunda Tume ya uchunguzi

Kumbe hela za kujenga kivuko kipya kikubwa kuliko MV Nyerere zipo,sasa tatizo lilikuwa ni nini mpaka haya yote yatokee?
 
Kufuatia ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere iliyotokea tarehe 20 Septemba, 2018 katika ziwa Victoria, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Temesa, Mussa Mgwatu kupisha uchunguzi.

Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliivunja Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Bodi hiyo iliyo chini ya Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali Mstaafu Mhandisi Mabula Mashauri ilivunjwa kuanzia tarehe 23 Septemba, 2018 wakati kamati ya uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea na uchunguzi wa ajali hiyo iliyotokea Mwanza.

Kutokana na ajali hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa ameunda Tume ya watu 7 kuchunguza ajali ya MV Nyerere ikiongozwa na Jen. Mstaafu, George Waitara na Mbunge wa Ukerewe, Mkundi

Ameagiza kutangazwa zabuni ya kutengeneza kivuko kipya cha Ukara-Bulogora kitakachobeba abiria zaidi ya 200 na uzito tani 50

Nadhani serikali ilifahamu kuwa kivuko kilichokuwepo hakikidhi matumizi, wangetengeneza toka zamani kivuko kipya nadhani ajali isingetokea, au wangeruhusu watu binafsi waongeze nguvu kwa kuleta vivuko sidhani kama ajali ingetokea. Naiasa serikali iwahusishe zaidi watu binafsi ili walete vivuko na meli ili kupunguza kero ya msongamano wa watu na mizigo huko visiwani
 
Nawakumbusha tu tuendelee kutoa michango yetu kwa ajili ya wahanga. Mwenye account maalumu ya kutuma fedha aweke hapa watu tuchangie. Mnara wa kumbukumbu pamoja na ukuta kuzunguka makaburi ni moja ya hitajio. Tujitokeze kwa wingi.
 
Jamaa atakuwa amemaindi kuona TAMESA hawaja wahi peleka ikulu gawio la faida kwa gavurumenti wakati wanavyo vyombo vya kibiashara kama MV hizi
 
Hatua nzuri.wanazochukua.
safi sanaa.
waangalie na suala la Zanzibar kusafiri usiku kwenye boti.ni hatari sanaa..
Majanga ya MV nyerere yametokea SAA 8 mchana tena m 50 kufika nchi kavu.wameshindwa kuokoa watu.
JE IKITOKEA BAHARINI TENA USIKU KATI KATI.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtangaza

Jenerali Mstaafu George Waitara kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza ajali ya
Mv-Nyerere na kutoa mwezi mmoja ili tume hiyo itoe majibu na mapendekezo juu ya hatua ambazo serikali inapaswa kuzichukua.

Akizungumza na wananchi wa Ukara Waziri Mkuu amesema serikali inaendelea na hatua za awali za kuhakikisha inawachukulia hatua waliosababisha ajali hiyo na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.


“Hatua za awali zilishachukuliwa tulishakamata wale wote ambao waliruhusu watu kujaa, na uchunguzi unaendelea, tumeunda tume iliyojaa wataalamu na vyombo vya dola ilitubaini nani hasa muhusika, tume ina watu saba na inaongozwa na Jenerali Mstaafu George Waitara.Nimewapa mwezi mmoja ili kutoa taarifa ya tukio hilo .”

Source: millard ayo
maja-660x400.jpg
 
Mimi nilijua ni huyu mbunge wa tume ya uchaguzi ndo ataongoza uchunguzi...!
 
kila kitu kipo wazi, sidhani kulikuwa na haja ya kuunda tume!!

vivuko vinajaza watu, mabasi yanajaza watu, malori yanabeba watu na mizigo lukuki kwenye na kurudi minadani, taratibu zipo wazi ila hakuna anayezifuata.....tuunde tume tena hapa wajemeni?
 
Upumbavu mtupu wa Africa huku anakamata watu, huku unaachishwa watu Kazi, huku una anda tume la kuchunguza, "what a confussion" kwahiyo una hukumu watu kabla hata kesi ijabainishwa, hayo ni maajabu ya nchi yetu.....kwanza wanachunguza nini hata mama angu huku kijijini anajua sababu ya ajali na ninani awajibishwe sasa ma proffesor wanini? kama sio matumizi mabaya ya pesa ya umma....basi watumie majibu ya tume ya meri Mv Bkb ya 1998 sababu ni zilezile na ziwa nililelile....lakini ukweli ni kwamba viongozi wetu ni wa sani
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtangaza
Jenerali Mstaafu George Waitara kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza ajali ya
Mv-Nyerere na kutoa mwezi mmoja ili tume hiyo itoe majibu na mapendekezo juu ya hatua ambazo serikali inapaswa kuzichukua.
Akizungumza na wananchi wa Ukara Waziri Mkuu amesema serikali inaendelea na hatua za awali za kuhakikisha inawachukulia hatua waliosababisha ajali hiyo na watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
“Hatua za awali zilishachukuliwa tulishakamata wale wote ambao waliruhusu watu kujaa, na uchunguzi unaendelea, tumeunda tume iliyojaa wataalamu na vyombo vya dola ilitubaini nani hasa muhusika, tume ina watu saba na inaongozwa na Jenerali Mstaafu George Waitara.Nimewapa mwezi mmoja ili kutoa taarifa ya tukio hilo .”

Source: millard ayoView attachment 876235
Napata Ukakasi sana kila ninaposikia mstaafu anaongoza tume, au ni mwenyekiti wa bodi, nk. Ni vizuri wastaafu wa aina hiyo wawe ni wale ambao wana utaalamu wa ziada, Hata hiyo bodi ya Ushauri ya TEMESA iliyovunjwa ilikuwa chini ya mstaafu je, ubora wake ulitosha kuisimamia TEMESA?. Kuna mambo yanahitaji walio na uwezo wa kufikiri, kubuni, n.k. Bodi na tume isiwe ni sehemu ya kulea wastaafu. Tunataka uzembe huu ukome na siyo kuwaridhisha waathirika au Taifa.

Tukumbuke pamoja na tume, wananchi wanafahamu ukweli ulivyokuwa siku zote. Nimesikia hata kujaza abiria ilikuwa ni sehemu ya kujipatia kipato cha ziada kwa watendaji wa TEMESA na waendeshaji wa kivuko. Je jenerali Waitara ana uwezo fulani wa ziada ktk mambo ya usafiri au vyombo vya majini? Kama ni ndiyo natoa heko. Kama sivyo, itakuwa ni kutegemea wajumbe wengine watoe michango na wanaweza kumbabaisha na kusema mambo ya ajabu. Nina hakika kuna watu sasa hivi wanalinda nafasi zao.

Mwisho naomba Patriot niwe sehemu ya tume hiyo. Hapo ndo tutaelewana na wapiga dili kwa gharama ya maisha ya watu.
 
Mbunge wa Ukerewe alishapiga kelele ya matatizo ya kivuko hicho bungeni ila kwa sababu kelele hizo zilitoka kwenye mdomo wa mbunge wa upinzani mlipuuza, maisha ya wanyonge yamepotea ndo mnajitutumua kuunda tume. Sijui mnachunguza nini. Uwe mpinzani uwe CCM wote wanamtetea mtanzania huyo huyo.
 
Back
Top Bottom