Ajali mbaya ya basi la NBS - Igunga

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Leo majira ya saa 4.00 asbh kumetokea ajali mbaya ya basi la NBS linalotokea Tabora kwenda Arusha, basi hilo lilipasuka Taili la mbele na kugonga mti na kuung'oa na kisha kupinduka, hadi sasa kuna maiti sita zilizowasilishwa Mortuari na Dereve wa gari hilo pia ni marehemu ila bado maiti yake haijatolewa kwani amebanwa hadi basi hilo likatwe ndiyo atolewe
P1010544.JPG P1010546.JPG P1010547.JPG P1010547.JPG
 
Tunawapa pole sana wafiwa na tumwombe Mora awaponye majeruhi wote.Amen.
 
mbona mnatuchanganya, hapa hapa ndani kuna sredi nyingine inasema ajali hiyo ni ya basi la MOHAMED TRANS lililotokea Mwanza hebu wekeni mambo sawa
 
Mungu aziweke roho za marehemu wote mahali pema peponi.....AMEN; Majeruhi wote MUNGU awape uhai wapone haraka"

Samahani kuna jamaa katinga na thread hapa naye anasema basi la Mohamed Trans litokalo Mwz~Dar limepata ajali hapo Igunga na muda ni huo huo sasa ni kwamba kuna ajali mbili tofauti maeneo hayo au?
 
Mi nipo eneo la tukio basi lililopata ajali ni NBS kutoka Tabora Kwenda Arusha na hadi sasa maiti ni Saba
 
Very sorry, Mungu awape moyo wa uvumilivu ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu. Pia majeruhi wote wa ajali naombea kwa Mwenyezi Mungu wapate afya njema haraka, na vivyo hivyo, Roho za Marehemu zilale mahali pema peponi.
 
Poleni sana wahusika wote. Kama kawaida tutaanza kumsingizia MUNGU kwamba kazi yake haina makosa.
Haya ni yetu wenyewe maana tunawaruhusu TBS kufanya watakalo ikiwa ni pamoja na kuingiza matairi yasiyo na viwango na kila siku ajali nasi tanalalama tuu.
 
Nawapa pole wote waliopatwa na misiba na nawatakia majeruhi kila la heri na mungu awasaidie wapone haraka. HAYO NDIYO MATAIRI YANAYOINGIZWA NA EKEREGE (MKURUGENZI MKUU WA TBS).
 
Leo majira ya saa 4.00 asbh kumetokea ajali mbaya ya basi la NBS linalotokea Tabora kwenda Arusha, basi hilo lilipasuka Taili la mbele na kugonga mti na kuung'oa na kisha kupinduka, hadi sasa kuna maiti sita zilizowasilishwa Mortuari na Dereve wa gari hilo pia ni marehemu ila bado maiti yake haijatolewa kwani amebanwa hadi basi hilo likatwe ndiyo atolewe

Kwa taarifa mpya ni kwamba waliofariki wamefikia 13.
Source: Sunrise Radio Arusha.
 
Basi la kampuni ya nbs lililokuwa likitokea mkoani tabora kwenda arusha asubuhii limepasuka tairi la mbele na kuua watu 8 papo hapo majeruhi wengine wamepelekwa hosipitali ya igunga kwa matibabu. Iwapo unataka taarifa kwa kina unaweza andika jina la ndugu yako hapa na utaarifiwa hali yake.
 
Poleni watanzania.
Mungu awfariji wafiwa na azilaze roho za marehem pahali pema peponi.
 
Back
Top Bottom