Ajali Kyaka, Kagera: Basi la Sabuni na gari ndogo ya Kanisa yagongana, Watu wapoteza maisha

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,904
10,384
Ajali mbaya imetokea eneo la Bugorora Kyaka leo, inahusisha Basi la kampuni ya Sabuni lililokuwa likitokea Karagwe na Land Cruiser ya Kanisa.

Taarifa za hawali zinasema watu si chini ya watano wamepoteza maisha kwenye eneo la tukio.

11813388_760691810708462_2873074362703542337_n.jpg

Basi la Kampuni ya Sabuni linalofanya safari kati ya Kagera na Mwanza limegongana na gari ndogo aina ya Land Cruiser iliyokuwa na mapadre na masista katika eneo la Bugorora nje kidogo ya Kyaka wilayani Misenyi mkoani Kagera.

Basi hilo nambari za usajiri T650 BFI na Cruiser T166 AGU ambapo waliotajwa kupoteza maisha kwa taarifa za awali ni Padre Onesmo Kahabwa na Michael Mwelinde pamoja Sista Magret Tadebe ambao ni wa Parokia ya Katoke waliokuwa wakitokea Rulenge wilayani Ngara.


Picha baadhi zinatisha hivyo sitaziweka.
 
Poleni sana wafiwa,muwe na miioyo ya subira,na waliyoumia twawaombea wapone,madereva wajitahidi kuwa makini.
 
Hizi barabara sasa zinaupita hata ukimwi jkwa kuua, nadhani baada ya malaria ndizo zinafuata.
Habari ya kusikitisha sana!
 
CHACHU OMBARA katika ubora wake tena....! inaelekea huwa unaoteshwa nini?ajali nyingi wewe ni wa kwanza kuripoti!
 
Wale wa #TeamPicha nimeweka moja yenye maadili,ambazo nilikuwa nazo mwanzo kiukweli hazikuwa na maadili maana zingewavunjia heshima marehemu.

RIP watumishi wa Mungu.
 
Hiyo kona naifahamu imekaa vibaya sana. Huyo jamaa wa Land Cruiser atakuwa alikula sana upande wa mwenzie ndo yakatokea yaliyotokea.

Poleni sana wafiwa!
 
Back
Top Bottom