Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 218
Ndugu zangu niko maeneo ya katikati ya jiji la DSM asubuhi hii tulipaki gari yetu Mtaa wa Jamhuri kwa dakika kama 40 hivi , tuliporudi tena tulikuta gari yetu imebadilishwa namba na pembeni yake ilipaki gari inayofanana na hiyo hiyo , Tukaamua kufikisha suala hili katika vyombo vya dola ila iligundulika kwamba kuna kikundi cha watu wezi wa magari wanafanya shuguli hiyo kwa kushirikiana na wenye breakdown maana yake ile gari baada ya muda inakuja kubebwa na breakdown na kupelekwa mafichoni .
Kwahiyo ndugu zangu muwe makini sana na aina hii mimi naiita mpya kabisa sijawahi kuona namba za gari kubadilishwa kwa muda mfupi hivi kama hili lililotokea asubuhi ya leo ,Imenishangaza sana kwa kweli