Magari ya TANESCO yanasababisha ajali na kukimbia

pombe kali

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
223
439
Salam wana jukwaa,

Una hii kero nimeipata siku nyingi ila sikuwa na msukumo wa kuileta humu mpaka ilipokutana na mtu wangu wa karibu, haya magari ya ndugu zetu wa tanesco yale ya emergency huwa hawajui ni muda gani waendeshe kana kwamba kuna dharula.

Hii inapelekea gari lile kuendeshwa kidharula muda wote linapokuwa kwenye barabara za umma inasikitisha kwani kuna ripoti nyingi za watu kugongwa na magari haya na kusababishiwa ulemavu na hata pengine Vifo ila kutokana na uelewa mdogo wa jamii huwa wana Acha kufuatilia wakiamini kuwa gari ikishakuwa ya emergency ina uwezo wa kugonga kuua bila kuwa na taratibu zozote za kisheria 😢 ikiwemo kudai fidia.

Huu ujumbe naomba ifikie mamlaka zinazohusika ili iwatengenezee taratibu kali madereva wanaowaajiri na wawajibike kwenye ajali wanazozisababisha ikiwa ni pamoja na kusubiri askari aje na kutua taarifa za dereva na mmiliki wa gari kwa ajili ya kwenda mahakamani na fidia ya bima, maana sisi wananchi siku tukichoka tunautaratibu wetu ambao pengine hamtaupenda sana.

Hamuwezi kuwa mnauwa watu na kuwatia ulemavu kisha mnakimbia eneo la tukio kwa kigezo kwamba gari hii ni ya dharula.

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom