Aibu JK azindua kidaraja Morogoro

Safi kabisa hayo ndiyo mambo tunayotaka we ulitaka azindue daraja lenye ukubwa gani? kwa kijijini hilo ni daraja kubwa sana.
 
Wanaotetea uwepo wa JK hapo kuzindua hlo daraja wajiulize je ni gharama kiasi gani imetumika kumpeleka rais na ujumbe wake kwenda na kurudi hadi huko,pengine ingetosha kuwajengea shule au zahanati.
hatukatai kujengwa daraja ila kwenda had matombo mh mh mh ni matumizi mabovu ya pesa ndopo tulizonazo
Mkuu kweli ni gharama kwenda Matombo, pia ni busara kujengwa kwa zahanati ama hata shule, lakini ujue jukumu lake msingi ni kwenda kuwatembelea wananchi hasa vijijini na hata kushiriki nao katika majukumu yao ya kimaendeleo, haiji kichwani awe anakuja tu wakati wa kampeni na kuomba kura , inatakiwa ziara zake nyingi ziwe za vijijini ikiwa na hilo la kufungua miradi inayofanywa chini ya serikali anayoiongoza, daraja kuwa dogo ama kubwa nayo ni agenda lakini kwasasa tuone llile lililokwishaafanyika yaani daraja hilo na ziara yake kuwa vipo katika wajibu wake wa kuwatembelea wananchi vijijini na kuongea nao, hayo mengine ya ziada, fikiria kama tungeambiwa ameamua kuwatembelea watu wa Mtombo tu bila kufanya kitu chochote, tungeiwekaje hii?
 
A
Nakumbauka mwandishi wa JITAMBUE (Tehenan) aliwahi andika "katika kila jambo, ni vile utavyotaka kuliangali... ukiutaka uzuri wake basi utauona mwingi na ukitaka ubaya wake pia utauona mwingi tu!". hii ndio siasa, unapotaka kukosoa jambo ambalo wengi wanaliona zuri bado unaweza kupata ubaya mwingi pia jambo baya kama utataka kulisifu basi utapata uzuri wake mwingi tu... ni siasa lakini mwisho wa siku maisha lazima yaendelee..


Ndg yangu umenikumbusha mbali sana mwalimu wangu Marehem munga Tehenan,mungu amlaze mahali pema
Peponi
 
I hope hakuna "mtaalamu" pande ya pili ya daraja ambaye ililazimu kuwe na usafiri wa uhakika 24/7. Just curiosity....
 
Sasa kama hana kazi afanyeje? Mzee wa kusubiri misiba apate pa kwenda kumalizia siku.

Sniper

Yote yasemwe, lakini hapo kwenye red, inaonyesha huna nidhamu kabisa. Yeye ni binadamu kama wewe, misiba inamhusu kama wewe, sasa kwa nini wewe ukienda sawa, lakini Rais akienda unamwita mzee wa misiba, so sad.

Kuhusu kidaraja kufunguliwa na Rais sio tatizo kama alikuwa huko kwa shughuri nyingine. Kama hicho ndicho kilichompeleka, ni matumizi mabaya ya fedha za umma hasa katika kipindi hiki. Pesa ya msafara wake tungeweza jenga vidaraja vya disgn hiyo kama vitatu.
 
hamna kitu nia aibu kwa raisi wa nchi.. sasa Makamu wa Raisi na mawaziri husika wanafanya kazi gani?? au hata wasanii wakubwa wa nchi wanashindwa kupewa nafasi hyo??
 
nimekupata mkuu ishu ni kwamba shughuli anayoizindua unakuta inacost almost half ya budget ya msafara wa mkuu wetu huyo so wat shuld we praise the answer is nothing
 
Nchi ya ajabu kweli hii...FFU wa nini sasa? Yaani ukiona kiongozi hajiamini hadi kwenye issue kama hizi, ujue kwenye siriaz issues kama za peaceful demonstrations tutapigwa sana...
Mungu kama kakupa uhai, weka neno kuhusu zama hizi za makirikiri
 
Back
Top Bottom