Ahsante wana JF

Bin Maryam unataka kwenda wapi? au umejiunga na mtandao mwingine?hebu fafanua kidogo

Mitambo ikikatika sina uvumilivu wa kurudi Pugu Road. Mafundi mitambo JF inabidi kuandalia umezekano wa ku-implement fault tolerant ili JF iwepo 24/7.
 
Mitambo ikikatika sina uvumilivu wa kurudi Pugu Road. Mafundi mitambo JF inabidi kuandalia umezekano wa ku-implement fault tolerant ili JF iwepo 24/7.

Sawa bin Maryam,lakini nadhani administrators wanajaribu kufanyia kazi maoni tuliyowapa baada ya msukosuko ule wa polisi,manaake moja ya maoni tuliwaeleza kuwa tunahitaji kuwa na back up kadhaa au kuhamisha server files toka server ya zamani hadi nyingine itakayokuwa mahala pengine popote duniani ambako jf wapo,ili kukitokea tena matukio kama yale tuendelee kuwa hewani,hata kama laptop ya invisible na cmb zitachukuliwa.Administrators au mna jingine kama sio hili?

Naam tuliwaelewa kupitia klhnews jana.
 
Dunia haiendi hivyo. Kuna stats ambazo zinasaidia kukua kwa website yoyote mojawapo ni idadi ya wanachama.

Yeah, na website nyingine zinakuwa kwa sababu ya ubora wa wanachama. Hivyo wanachama ambao wanajiona kuwa siyo wavumilivu na hawako tayari kuonesha uvumilivu huo na kuchukuliana na mahangaiko ya website na wanaamua kuzira nadhani ni idadi ambayo website yoyote itafurahia ikipungua.
 
Heshima mbele wakuu, jamani kazi ni nzuri sana.... Naona leo imekuwa fasta kuashiria wembe umenolewa...... GOOD JOB WAKUU, MUNGU AWABARIKI NA KUWAONGEZEA JAMANI!!!!

Kwa wengine pia jamani mchezo umerudi tuendelee kurekodi na kucheza mizika kama inavyojiri.....

Mungu Ibariki Tanzania
 
Yeah, na website nyingine zinakuwa kwa sababu ya ubora wa wanachama. Hivyo wanachama ambao wanajiona kuwa siyo wavumilivu na hawako tayari kuonesha uvumilivu huo na kuchukuliana na mahangaiko ya website na wanaamua kuzira nadhani ni idadi ambayo website yoyote itafurahia ikipungua.

Mwanachama siku zote sio mvumilivu. Mbona ukuonyesha uvumilivu wako Darhotboard ?

Mwanachama ni kama mteja tu. Kinachotukalisha hapa ni kuwa admin wa JF wamejaribu kufanya kazi nzuri kuliko admin na Moderators wa Forum zingine za ki-Tanzania.
 
bado upo nilidhani ushafuta account..
 
Afadhali imerejea hewani.
Hakika nilikosa amani kama walivyo wanajumuia wengine, kuikosa JF hewani. Maana nilifungua. Nikafungua. Nikafungua but where.
Sasa nina amani.
Tuko pamoja
Pamoja tutaigeuza Tanzania kuwa yenye neema zaidi.
 
Wakuu nawapongeza sana kwa kazi ambayo najua ilikuwa ni ngumu ya kuiimarisha forum hii muhimu kwetu sote.

Napenda kuwapa salamu za pole za msukomsuko vijana wenzangu Max na mwenzie kwa zahama walizozipata kutokana na kushikiliwa na Polisi ambao inaonekana hawafanzi kazi yao ipasavyo ya kuwakamata wale wote wanaotajwa mpaka sasa kwa tuhuma za ufisadi na kukimbilia kutaka sifa kwamba wamekamata "vifaranga vya kuku" kwani kuku na majogoo yaliyobobea kwa rushwa, dhuluma na ufisadi bado wanapeta ama ndani ya uzio au mabarabarani.

Nami nikiwa mtaalam wa masuala haya naelewa ugumu wa kazi hii ambayo inahitaji muda mwingi, ujuzi na maarifa kuhakikisha lile daftari la wanachama na kabati letu "server", vinakuwa "safe".

Pia nimefurahishwa na jinsi JF admins wanavyojitahidi kufanikisha uimara wa JF unabaki palepale kwa hilo nawapongeza sana.

Kwa muda wote wa msukomsuko kwa forum hii ambao unaletwa na watu wasioelewa maana ya "online forums" nimekuwa nikifuatilia na kuona ni nani ataibuka bingwa katika masuala haya na hapa napenda kuwapongeza sana waheshimiwa Mwanakijiji na wenzake Invisible na wengine ambao wamekuwa wakikesha kuhakikisha forum hii maarufu inakuwa hewani kutokea mahali salama.

Masuala ya kufatiliwa na wanaojiita polisi au usalama wa taifa au serikali kwa ujumla haupingwi kwa ni uwezo wanaweza kuwa wanao (kama inawezekana) , isipokuwa ufatiliaji huo unawekwa mahali pasipo -Jambo Forums.

Wahusika wote wajue kwamba hapa sio uwanja wa fisi kwamba watu wanabwabwaja tu na kuyumbayumba kwa ulevi wa 24/7, bali hapa ni mahali pa watu wenye upeo mpana tena wa kujua nini kinaendelea jinsi ya kuchambua, ni wakti gani kiwe tayari na kiwekwe jamvini.

Mwisho, napenda kuungana na wanachama wenzangu wote popote pale walipo duniani tuzidi kutoa maoni kwa nguvu zote na kuchangia mijadala mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa imewaamsha wananchi wenzetu wa Tanzania na kwingine, kuona mambo na midubwana mbalimbali ya ajabu inayofanzwa na watu waliopewa dhamana ya kuongoza.
 
Afadhali imerejea hewani.
Hakika nilikosa amani kama walivyo wanajumuia wengine, kuikosa JF hewani. Maana nilifungua. Nikafungua. Nikafungua but where.
Sasa nina amani.
Tuko pamoja
Pamoja tutaigeuza Tanzania kuwa yenye neema zaidi.

Hii nayo ilihitaji thread mpya?!?!?!?!?!?
 
Pongezi kwa waraghibishi, wanachama na wapenzi wote wa JF. Nina udadisi kidogo-ilisemwa polisi waliomba radhi, lakini nimeshangaa hivi karibuni tamko la polisi likisema hakuna aliyekamatwa sababu ya JF, wala wahakuifunga JF na wala wahakuwa na nia ya kuziba uhuru wa maoni( nadhani nilisoma kwenye KULIKONI). Ni wakati wa kutaka tamko rasmi la IGP Mwema kuwaomba radhi Mike na Mac

http://www.chadema.net/habari/2008/habari4.php

Harakati ziendelee!

JJ
 
Mnyika point nzuri sana; na tumekuwa katika mazungumzo na CPJ na ninatumaini Polisi watatoa tamko lao mapema kabla hatua za kisheria dhidi yao hazijachukuliwa. Wasidhani kumwachilia mtu kimya kimya kunamaliza hoja.

a. Kitendo cha kumkatama mtu na kumhoji kwa masaa karibu ishirini bila warrant au amri halali ni kitendo cha kiunyanyasaji na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu.

b. Kitendo cha wao kuwahusisha vijana hawa na mtandao wa ughaidi siyo tu kumewachafulia majina yao bali pia kumesababisha wakose nafasi nyingi za kuaminiwa na hivyo kufanya maisha yao kuwa magumu pasipo ulazima wowote.

c. Kitendo cha Jeshi la Polisi kuchukua mali za vijana hawa kuziangalia, na kuzifanyia uchunguzi pasipo amri yoyote ya wao kufanya hivyo ni kinyume cha Katiba na kinaangilia mawasiliano ya mtu na kuvunja sheria.

d. Kitendo cha Polisi kuwashikilia vijana hawa kilisababisha hali ya wasiwasi, hofu, maumivu, hofu, woga, usumbufu kwa ndugu jamaa na marafiki; kilisababisha nyumba ya mmoja wao kuingiliwa na kuibwa vitu baada ya kujulikana hayupo nyumbani hasara ya karibu shilingi milioni 50!

e. Mmoja wao alikuwa anafuga kambwa kadogo kadogo ambako kalitoweka hadi leo hakajapatikana na inadaiwa kalipigwa mawe na mzoga wake kukutwa kawe karibu na "Stendi ya Basi". Mnyama huyo na mlinzi wa nyumbani alifanyiwa hivyo baada ya Polisi kumshikilia mwenyewe. Uchungu wa kufiwa na kambwa hako kakali umesababisha huzuni na uchungu ambao unakadiriwa kufikia shilingi milioni 10.

Baada ya kuangalia hayo yote na kwa vile jeshi la Polisi na serikali hawajaomba radhi na kusema kuwasafisha vijana hawa hadharani na kuahidi kutokuwanyanyasa tena kunasabisha a pending lawsuit ambapo madai ya karibu shilingi milioni 70 ya madhara (damages) yatadaiwa na shilingi milioni 200 ya adhabu (punitive).

Ila wakiamua kuomba radhi mapema wiki ijayo, we'll rethink some of our options na kujaribu kusettle for "undisclosed amount".
 
Kaka

Umenena vyema. Nami nitafunga bakuli langu kwa sasa kuhusu suala hili. Wasipoomba radhi ndani ya wiki moja, nyie songeni mbele. Na mkitaka msukumo wa kisiasa kuhusu suala hili nitautoa kwa dhati kama mwanachama mtiifu wa JF. Nawatakieni heri

JJ
 
Wana JF tusimsahau Mac na Ndoa yake mnamo July.........Mac tuko pamoja Mkuu
 
Wana JF tusimsahau Mac na Ndoa yake mnamo July.........Mac tuko pamoja Mkuu

Duuh, naona bakuri la mchango litapitishwa si punde! .......lol

...Lakini inabidi tujue huyo ni mke wa ngapi bana... maana hatuchelewi kusikia mwezi december anaona mke wa tatu :) lol, vijana wa siku hizi nuksi mkuu wangu... kabla haujakaa vizuri tunaweza sikia kuna ubatizo wa mtoto wa kwanza, na baadae tukaletewa taarifa kuwa kijana wake wa nne katoka jandoni sherehe mwezi wa nane..... ;)
 
Back
Top Bottom